Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
Du! huyu naye ni kiongozi by 2010???? Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo! Wakuu are we really serious?
Mbunge adai kufanyiwa vitendo vya kishirikina jimboni
Hussein Semdoe, Kilindi
MBUNGE wa Jimbo la Kilindi katika Mkoa wa Tanga, Beatrice Shelukindo amesema amekuwa akifanyiwa vituko mbalimbali vya kishirikiana wakati wa ziara za kutembelea wananchi na hivyo kushindwa kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi.
Shelukindo alidai kila anapoanza ziara ya kuwatembelea wananchi wake vijijini, hukumbana na vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na gari yake kuharibika mara kwa mara katika mazingira ya kutatanisha na wakati mwingine kunusurika kupata ajali baada ya gari lake kuparamia miti
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara, wakati akihutubia wananchi katika vijiji vya kata za Saunyi na Mswaki wilayani Kilindi juzi Shelukindo, aliwataka wachawi hao, kufanya dawa ili akubaliwe kila jambo analoliomba serikalini kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo hilo kama kuboreshea miundombinu mbalimbali katika eneo hilo.
"Kuna jambo linalonishangaza kila ninapotaka kufanya ziara hapa jimboni, yanaibuka mambo ya ajabu, hivi karibuni nilikuwa nikiwahi kikao mjini Songe, lakini gari yangu ikazimika ghafla, lakini likawaka na nilipofika jirani na mji huo, gari likaharibika tena, nikapanda basi la kwanza nalo likaharibika, nikapanda la pili nalo pia liliharibika na nilichelewa kikao kile.
Jamani ndugu zangu uchawi hauna faida yoyote tubadilike ki fikra ili tuelekeze nguvu zetu katika kufanya kazi zetu za maendeleo pamoja na kusomesha watoto wetu, lakini kuendekeza ushirikina ni kupotoka kimaendeleo," alisema Shelukindo.
Mbunge huyo aliwaomba wazee na waganga wilayani hapa kumsaidia kufanya dawa ili aweze kuwahi vikao mbalimbali vya kusaidia maendeleo ya wilaya hiyo, badala ya kufanya dawa ili achelewe, kama wanavyomfanyia.
Alisema ni aibu kwa baadhi ya wakazi wa Jimbo hilo la Kilindi kuendekeza vitendo hivyo vya kishirikina ambavyo vimekithiri na kudai kuwa sasa vimepitwa na wakati.
"Ndugu zangu niwaeleze hali halisi ilivyo, mimi nimepata majaribu mengi yanayohusiana na ushirikina, niliyowaeleza ni baadhi tu. Kama isingekuwa kumuomba Mungu sasa hivi tayari ningeshafukiwa kaburini na ingebaki mifupa,"alisema huku akionyesha kusikitishwa na hali hiyo.
Source: Mwananchi