Mbunge adai kufanyiwa vitendo vya kishirikina jimboni

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
30
Points
135

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 30 135
Du! huyu naye ni kiongozi by 2010???? Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo! Wakuu are we really serious?

Mbunge adai kufanyiwa vitendo vya kishirikina jimboni

Hussein Semdoe, Kilindi

MBUNGE wa Jimbo la Kilindi katika Mkoa wa Tanga, Beatrice Shelukindo amesema amekuwa akifanyiwa vituko mbalimbali vya kishirikiana wakati wa ziara za kutembelea wananchi na hivyo kushindwa kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi.

Shelukindo alidai kila anapoanza ziara ya kuwatembelea wananchi wake vijijini, hukumbana na vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na gari yake kuharibika mara kwa mara katika mazingira ya kutatanisha na wakati mwingine kunusurika kupata ajali baada ya gari lake kuparamia miti

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara, wakati akihutubia wananchi katika vijiji vya kata za Saunyi na Mswaki wilayani Kilindi juzi Shelukindo, aliwataka wachawi hao, kufanya dawa ili akubaliwe kila jambo analoliomba serikalini kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo hilo kama kuboreshea miundombinu mbalimbali katika eneo hilo.

"Kuna jambo linalonishangaza kila ninapotaka kufanya ziara hapa jimboni, yanaibuka mambo ya ajabu, hivi karibuni nilikuwa nikiwahi kikao mjini Songe, lakini gari yangu ikazimika ghafla, lakini likawaka na nilipofika jirani na mji huo, gari likaharibika tena, nikapanda basi la kwanza nalo likaharibika, nikapanda la pili nalo pia liliharibika na nilichelewa kikao kile.

Jamani ndugu zangu uchawi hauna faida yoyote tubadilike ki fikra ili tuelekeze nguvu zetu katika kufanya kazi zetu za maendeleo pamoja na kusomesha watoto wetu, lakini kuendekeza ushirikina ni kupotoka kimaendeleo," alisema Shelukindo.

Mbunge huyo aliwaomba wazee na waganga wilayani hapa kumsaidia kufanya dawa ili aweze kuwahi vikao mbalimbali vya kusaidia maendeleo ya wilaya hiyo, badala ya kufanya dawa ili achelewe, kama wanavyomfanyia.


Alisema ni aibu kwa baadhi ya wakazi wa Jimbo hilo la Kilindi kuendekeza vitendo hivyo vya kishirikina ambavyo vimekithiri na kudai kuwa sasa vimepitwa na wakati.

"Ndugu zangu niwaeleze hali halisi ilivyo, mimi nimepata majaribu mengi yanayohusiana na ushirikina, niliyowaeleza ni baadhi tu. Kama isingekuwa kumuomba Mungu sasa hivi tayari ningeshafukiwa kaburini na ingebaki mifupa,"alisema huku akionyesha kusikitishwa na hali hiyo.


Source: Mwananchi
 

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,139
Likes
2,496
Points
280

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,139 2,496 280
I hope alikuwa anatania tu kujaribu kujikosha na tabia yake ya kuchelewa!
 

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
3,302
Likes
1,136
Points
280

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
3,302 1,136 280
Du! huyu naye ni kiongozi by 2010???? Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo! Wakuu are we really serious?
Ukitaka kumjua mtu aljiyechuja ni aina hii ya viongozi. Kwani huyu mama huko ni kwao mila na tamaduni za kwao anazifahamu na hao wanaotaka kugombea jimbo hilo ni wa kwao na yeye yuko kwenye seat hivi sasa. Wasiwasi wa nini kama anakubalika???

Unajua kuna aina ya wabunge ambao ni wapiga kelele sana bungeni Hivyo kuwafanya wajulikane sana kitaifa lakini kwenye majimbo yao hakuna kitu cha maana wanachokifanya na mara nyingi huwa wanatumia miaka 4 kutumbua dar na dodoma na nje ya nchi na mwaka 1 hutumia jimboni na inapofikaribia kipindi cha uchaguzi hulialia kama fisi.

Hivi kama wewe ni mbunge na jimboni kwako unakubalika wasiwasi wa nini??? Wananchi hivi sasa wameelimika sana na hawadanganyiki na fix za kisiasa hivyo kama hufikii vigezo vyao watakutimua tuu.
 

Pengo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2009
Messages
579
Likes
3
Points
0

Pengo

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2009
579 3 0
Aende kwa marehemu Mandondo kule atapata ujinga wote anaoutaka,ila pepo hatokuwa nayo iwapo umauti utamkuta kabla ya kutubu!
 

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
11,938
Likes
1,169
Points
280

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
11,938 1,169 280
Si ameokoka huyu? Mbona sasa asitumie nguvu za wokovu kuushinda uchawi. Dada Beatrice umenisikitisha kwa hili maana nilijua wewe uu mlokole wa kikweli. Hutakiwi kuogopa kama una Yesu wako. Kemea kwa jina la Yesu na utashinda.

Ukweli ni kwamba Tanga ni mkoa unaojulikana kwa aina zote za uchawi na nguvu za jiza ila pia Wilaya ya Kilindi ndiyo yenyewe.
 

Bramo

JF Bronze Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
9,674
Likes
2,743
Points
280

Bramo

JF Bronze Member
Joined Oct 21, 2009
9,674 2,743 280
Kajuaje karogwa kama na yeye si mchawi...

Kaziii kwei kwei.. CCM na Sheikh Yahya Hussein
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,732
Likes
12,290
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,732 12,290 280
Magazeti hayaaminiki tena, ingekuwa si hivyo ningeona inconsistencies katika kauli za mbunge kuomba kufundwa halafu hapo hapo kujitia mtu wa dini.
 
Joined
Dec 20, 2009
Messages
35
Likes
0
Points
0

Samat

Member
Joined Dec 20, 2009
35 0 0
Kama ni mtu wa mungu ataamini vipi ushirikina? kwa upande mwingine anawaomba wachawi wamsaidie... nae anahusika kwa njia fulani. Kuamini ni kushiriki!!
 

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
13,651
Likes
6,284
Points
280

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
13,651 6,284 280
Ushirikina ni mojawapo ya sera za chama cha cha mafisadi, hatuwashangai ,kwani hata ofisi kuuubwa kuliko zote nchini imeingia kwenye upuuzi huu wa kutumia wachawi kutisha watu wasigombee nafasi hiyo. Hivi hamkumbuki kilichotokea kwa mgombea wa chama hicho kule mwanza mwaka 2005? Hakika tutayasikia mengi.
 

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
21,829
Likes
137
Points
160

TIMING

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
21,829 137 160
Hii ndiyo level ya imani za giza ilipofika, sasa maalbino wetu watapona? watoto wetu watapona? kwa imani hii unadhani wakazi wa kilindi ni watu wa namna gani? Na huyu mama ana dini?

Mungu ibariki tanzania
 

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Messages
7,728
Likes
25
Points
135

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2008
7,728 25 135
Wabwanga ya kweli haya??


Kwa lipi moja haya anayosema Mbunge au hiyo imani yake ya kishirikina?
Kwa mie sioni ukweli wa hilo lakwanza na nashangazwa na hili la pili, Hata Shelukindo nae? Hata hivyo huyo si CCM au la kwani CCM kule Ikulu si mnajuwa ya Sheikh Yahya na maombi kwa timu ya Ivory Coast.
 

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
2
Points
35

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 2 35
Mwaka huu, we acha tuuu! tutaskia mengi sana. Mbunge Beatrice anajiandaa kupambana na Aisha kigoda katika jimbo la kilindi, wawili hao hawaivi sasa hivi nasikia kila mmoja anamtuhumu mwenzake ni mchawi, ama kweli ukistaajabu ya tanga...!
 

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
6,635
Likes
635
Points
280

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
6,635 635 280
Kwa nnavyoijua Tanzania, sishindwi kushangaa, kwamba hiyo kitu ina ukweli!
Huyu mama keshafulia kwa lugha ya siku hizi ya mjini, kwahiyo hayo yote anayosema hayanaukweli maji yamezidi unga huko jimboni kwake na sasa anatafuta sababu za kupata sympathy ya wapigakura!!
Mbunge anaeamini ushirikina hawezi kuwaletea watu maendeleo afadhali wananchi wa Kilindi wamtose aende akaimbe ngonjela!!
 

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
30
Points
135

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 30 135
Huyu mama keshafulia kwa lugha ya siku hizi ya mjini, kwahiyo hayo yote anayosema hayanaukweli maji yamezidi unga huko jimboni kwake na sasa anatafuta sababu za kupata sympathy ya wapigakura!!
Mbunge anaeamini ushirikina hawezi kuwaletea watu maendeleo afadhali wananchi wa Kilindi wamtose aende akaimbe ngonjela!!


Quote:
SMU
12n2_01on.gif


I hope alikuwa anatania tu kujaribu kujikosha na tabia yake ya kuchelewa!


Mkuu ukweli naomaanisha ni kuwa "haya maneno yalisemwa na huyu mama" na hii ni baada yah SMU kuweka benefit of doubt kwamba huenda ni
spinning ya mwandishi.
 

Forum statistics

Threads 1,190,580
Members 451,229
Posts 27,675,890