Mbunge aanza na ahadi ya elimu kwa masikini............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,974
2,000
Mbunge aanza na ahadi ya elimu kwa masikini
Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 8th December 2010 @ 21:40

OFISI ya Mbunge Jimbo la Arusha, imeanza kuinua watoto wanaoshindwa kuendelea na masomo, kwa kuunda Kamati ya Maendeleo ya Jimbo itakayoratibu watoto zaidi ya 600, ili waendelee na masomo ya sekondari, ifikapo Januari 2011.

Hayo yamesemwa Desemba 8 na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kwa tiketi ya Chadema,
Godbless Lema, wakati alipokuwa akizungumzia mikakati yake ya maendeleo ambayo kipaumbele ni elimu.

Alisema mkakati huo ni moja ya ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni, katika kuhakikisha watoto wa familia duni na masikini, wanaendelea na msomo yao ya elimu ya sekondari bila kukwama.

“Mimi nimekaa ofisini kwa siku chache, katika watu kumi na nane waliofika ofisini kwangu, mahitaji makubwa kwao ni elimu, hivyo nimeona ipo haja kuanza haraka kulishughulikia hili kwa kuunda kamati maalum ya kuratibu,” alisema Lema.

Alisema wataanza na watoto 500 na lengo la ofisi yake ni kuwawezesha watoto 1,000 au zaidi, kulingana na mahitaji ya watoto yatakavyokuwa.

“Lakini ili kufanikisha hili, imenipasa kuandaa matembezi ya hisani kwa kushirikiana na
kamati yangu ya watu wasiozidi 15, yatakayofanyika Desemba 17 mwaka huu, ili tupate fedha za kuwasaidia watoto hawa,” alisema Lema.


Alisema kitu kikubwa anachokiona siyo kukosekana kwa fedha bali mwamko wa watu kusaidia elimu ni mdogo, hivyo kwa kuanzia, ataonesha njia, ili watu walenge katika masula ya maendeleo, badala ya kuchangiana michango mikubwa katika harusi za kifahari.

Katika wajumbe wa kamati hiyo, mbunge huyo amezingatia elimu, jinsia, vigezo vya uwajibikaji, kuheshimika mbele ya jamii, uwezo wa uelewa na uhamasishaji, michango ya wateuzi katika kazi za kijamii na sifa zao kwa jamii bila kujali itikadi zozote za kisiasa.

Alisema kazi ya kwanza ya kamati hiyo ni kuunda na kusimamia kamati ndogo itakayoratibu mfuko wa elimu wa jimbo na kuandaa mchakato wa uwazi wa upatikanaji wa watoto na kusimamia upatikanaji fedha.

Ili kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo, kutakuwa na kasha la uchangiaji kwenye kila hoteli ili watu washiriki kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,974
2,000
Alisema mkakati huo ni moja ya ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni, katika kuhakikisha watoto wa familia duni na masikini, wanaendelea na msomo yao ya elimu ya sekondari bila kukwama.

"Mimi nimekaa ofisini kwa siku chache, katika watu kumi na nane waliofika ofisini kwangu, mahitaji makubwa kwao ni elimu, hivyo nimeona ipo haja kuanza haraka kulishughulikia hili kwa kuunda kamati maalum ya kuratibu," alisema Lema.

Nionavyo mimi tatizo ni namna gani mafanikio ya ahadi kama hizi hufanyika tathmini yake.........au tutapima kutokana na waheshimiwa watakavyokuwa wakijipima..................utendaji wao wenyewe.........................
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
safi!miaka 49 iliyopita kama kila mbunge angefanya hivyo tungekua hatuna mbumbu hata mmoja!kazi kuwazia majumba yao dar tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom