Mbuge wa wadi ya Mwanyanya (CCM) kwa 19% anamwakilisha nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbuge wa wadi ya Mwanyanya (CCM) kwa 19% anamwakilisha nani?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by lifeofmshaba, Apr 21, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MAAJABU YA DUNIA MBUNGE WA WADI MWANYANYA KUINGIA BUNGENI KWA 19%?
  CCM wanatamba kwa ushindi kama huo

  Ni sawa na asilimia ya 19% ya wapigakura (walipaswa kupiga kura watu 4,059 na yeye kapata kura 807 ni kura kidogo kuliko baadhi ya madiwani.

  Watu kutopiga kura ni ujumbe tosha kwa mbunge mteule kutokuwa na mvuto kwa jamii anayoiwakilisha,

  Kwa wenye hekima huyu ni mshindi aliyeshindwa ( ni wakati sasa katiba kuwakataa wabunge kama hawa wasiokubalika wanakotoka)

  Sekreterieti mpya ya ccm ilikwenda Zanzibar kutafuta kura 807, hii ni aibu kwa ccm kutokana na nguvu waliyotumia kwenye huo uchaguzi mdogo

  CCM wanadhani wamepata kura 807 kwa sababu wamevua gamba ya kwamba sasa wanakubalika na wananchi kwa kupata kura 807 katika ya kura 4059 za wanaositahili kupiga kura.
  Watanzania kama tusipo amka na kujua umuhimu wa kura zetu basi tutaendelea kupata wabunge kama HAMZA KHAMIS JUMA, hiyo 19% ni ya watu

  waliojiandikisha kupiga kura kama tukifanya utafiti zaidi unaweza kubaini kwamba huyo mbunge kachaguliwa na watu chini ya asilimia 10, kwa maana nyingine ruhusa yake kuwakisha hiyi jamii ni kama haipo kabisa.

  Hapa ndio naona KATIBA inatakiwa kuweka kikwazo cha asilimia za ushindi wa wabunge kwa kuzingatia watu wanaopaswa kupiga kura na kura alizopata mbunge, yawezeka kabisa watu kutopiga kura ni aina ya kuwakataa wagombe wote waliopo katika mchakato, Katiba inatakiwa kuwatema wabunge walipata mwitikio mdogo kwenye majimbo yao wakati wa
  uchaguzi ili kuongeza nguvu ya umma katika uwakilishi kwenye hilo jengo la kutunga sheria.

  Kwa misingi hiyo wagombea wataamasishwa watu kwenda kupiga kura badala ya kununua kadi zao ili wasipige kura, hii itawakomesha ujanja wa wachache wanaofikilia kupunguza idadi ya wapiga kura kwa vitisho na hira ndio njia ya kushinda uchaguzi.

  Mimi nina hakika kama kila mtu hatapewa nafasi ya kusimama mbele ya sandukula la kura pale sirini hawezi kuiuza nafasi yake,

  Watanzania huu ni wakati wa kwenda kupiga kura, serikali haiwezi kuwaamasisha kupiga kura maana hiyo ni moja ya mikakati yake kuendelea kubaki madarakani, nchi zote zenye maendeleo ni kwa sababu wanaheshimu na kuthamini sana kura zao, kura ni kila kitu, ni huduma zote za jamii na maendeleo ya nchi. kura ina thamini kuliko hiyo kazi unayofanya, maana kama bunge na serikali wakiingia watu wenye uchu kama ilivyo sasa watakula mali zote unazozalisha kila siku na ulizozalisha kwa muda mrefu.

  SOURCE: lifeofmshaba.com
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ndio maana wakifika bungeni wanakwenda kushangilia chama , maana wanajua wananchi hawana mapenzi nao
   
 3. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Si mchezo naona tunawapotosha watu, aliyechaguliwa siyo mbuge bali ni diwani wa mwananyanya ambayo imo katika jimbo la Mtoni kama sijakosea na mbuge wa mtoni ameshachaguliwa zamani.Juu ya yote hayo but 19% ni ndogo sana
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Je unafahamu kanuni ya uchaguzi inasemaje kuhusu kutangaza mshindi.

  .....inasema bayana kuwa mshindi atakuwa yule aliyepata kura nyingi za ndio..... huyo attangazwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa ni mshindi.

  Sasa huyo atawawakilisha watu wote wa hapo mwanyanya.

  kama wangetaka basi wangekwenda wote na kupiga kura ya hapana kisha mambo yangekuwa shwari kwao
   
 5. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wewe unadhani kwa nini mwitikio wa kupiga kura unakuwa mdogo kiasi hicho, pili nimesema hapo kwenyepost sheria ze ndi mbovu na wawakilishi kama hawa wamebaka uwakilishi wa majimbo, kwa nini tusiwe watafiti, watu kutopiga kura inatoka na mambo mengi, vitisho na wajanja kununua kadi zao, wengine wanapata shida kupata majina ya katika vituo vyao na huu ni ujanja wa ccm ili kushika hatamu, ni vizuri umegundua hiyo sheria ya uchaguzi inausika kutulete uozo wa wabunge
   
 6. SONGEA

  SONGEA Senior Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa kinachotakiwa kujadiliwa si uhalali wa kiogozi huyo (mbunge/diwani). Cha kujadili ni sheria iliyotumika.
   
 7. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  huyo ndio point yenyewe mkuu
  kuna watu wanaingia bungeni vigezo duni
  sasa kama huyo watu hao waliomchagua na idadi ya watu katika jimbo lake weka na wale wasionasifa za kupiga
  kuna huyo ni mwakilishi wa jimbo kweli?

   
Loading...