Mbuge Kibamba Issa Mtemvu anza na changamoto hizi

luirhu

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
800
412
Mh. Mbunge Issa Mtemvu kwanza nakupa pongezi kwa kushinda jimbo hili la kibamba hakika unastahili.

Wananchi wa maeneo ya Kiluvya Gogoni/Hondogo wanakuomba uanze kushughulikia changamoto zifuatazo:

1. Barabara za mitaani zianze kujengwa Kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa DMDP, wananchi wanakumbusha kuna ahadi ya km 111 za lami kutoka DMDP chondechonde maeneo hayo yasikose.

Hiyo ndio changamoto kubwa Kwa wakazi hao ukiifaanikisha utakuwa umejiwekea heahima kubwa Na rekodi isiyo futika.
Kazi inaendelea. Muda ndio huu
 
Hata njia ya Kibamba mji mpya haifai kabisaa nachelea kusema hakuna jipya litakalo fanyika zaidi ya kuleta gredar na kusesa bara bara bila ya kuweka njia stahiki za maji ya mvua mitaro. Nikawaida yetu wana Kibamba kujichangisha kurekebisha sehemu korofi huku serekali ikiwa inaona na kupiga kimya, tungojee muda utasema.
 
Mleta post. Unajuwa kazi ya mbunge nini? Kama unajua, taja tatu.
 
Wananchi wanahitaji kuona kero zao za mda mrefu zinatatuliwa sio maneno matupu, Mbunge anao wajibu wa kutafuta ufunbuzi juu ya kero za wananchi wake,
Mbunge ndio kuunganishi kati ya wananchi na serikali kuu. Naamini Mtevu anaweza kuzishughulikia na kutatua kero za wananchi wake wa jimbo la kibamba na kwa kuanzia maeneo ya kiluvya Gogoni/Hondogo
 
Mh. Mbunge Issa Mtemvu kwanza nakupa pongezi kwa kushinda jimbo hili la kibamba hakika unastahili.

Wananchi wa maeneo ya Kiluvya Gogoni/Hondogo wanakuomba uanze kushughulikia changamoto zifuatazo:

1. Barabara za mitaani zianze kujengwa Kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa DMDP, wananchi wanakumbusha kuna ahadi ya km 111 za lami kutoka DMDP chondechonde maeneo hayo yasikose.

Hiyo ndio changamoto kubwa Kwa wakazi hao ukiifaanikisha utakuwa umejiwekea heahima kubwa Na rekodi isiyo futika.
Kazi inaendelea. Muda ndio huu
Kuna mziki uko Kwa Musuguli hadi Kifuru kupitia Bwaloni Nguzo,top city hadi kwa Hunju.Hii barabara Ni kama inaelekea kwenye Mali za Mjerumani kule Nyumbanitu.
 
Huyo mbunge ni wa hovyooo hana akili wala creativity yaani wana Kibamba tupambane na hali zetu tuuu
 
Kwanza kabisa awalipe fidia wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwa kisingizio Cha barabara wakati barabara haijafika huko zilipokua. Rekebisha uonevu huu kwanza kwani wote wanajua kilicho waponza Ni CHADEMA.
 
Imbombo Ngafu ,CCM inabidi walete maendeleo sana maana kwasasa wapinzani hakuna ambao walikuwa wanachelewesha.
 
Majimbo yote yaliyo kuwa yamekaliwa Na wapinzani maendeleo yalisuasua sana; mfano jimbo la kibamba Mnyika alikaa miaka 10 hakuna CHA maana alicho fanya,
Hata km 1 ya lami Kwa ufadhi wa DMDP hakuna, naamini MHE Isa Jumanne Mchomvu antaweka historia ya maendeleo ktk jimbo la kibamaba
 
Kuna Lori bwalon limepinduka na kuzima barabara mbunge aende kulitoa.
 
Kuna Lori bwalon limepinduka na kuzima barabara mbunge aende kulitoa.

Kuna uji wa volkano unatokota huko kunduchi mbunge akazuie volcano?!!!
Kwa hiyo asiambiwe Mbuge wakati yeye ndiye muwakilishi wa wananchi, lazima mbunge ataarifiwe kero za wananchi kisha yeye akishirikana na wanachi pamoja na serikali na wadau wa maendeleo pamoja na wataalamu ili watatue kero husika.
 
Mleta post. Unajuwa kazi ya mbunge nini? Kama unajua, taja tatu.

Civics form two. Akiweza ningeshangaa maana hata baadhi ya Wabunge wengi nao hawajui kazi na mipaka ya majukumu yao. Wapowapo tuu
 
Changamoto yoyote amabayo inagusa jamii ktk eneo husika na ikakosa utatuzi au inahitaji kushughulikiwa na mamlaka za juu lazima mbunge afahamushwe ili sio ajenge yeye bali aweze kuliwasilisha serikali Kuu au Kwa wadau wa maendeleo na kutatua,
Kwa msingi huo Mbunge wa kibamba ndg. Mtevu anao wajibu wa kutatua kero hiyo ya barabara Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo
 
Msumi kwenda Mbezi barabara Ni makorongo na mahandaki matupu, maji hakuna pia. Aanze kutembelea maeneo ya Jimbo lake aone changamoto za Jimbo lake maana yuko kimya Kama hayupo. Stendi kubwa ipo mbezi Ni aibu barabara za pembezoni kuwa katika Hali mbaya namna hiyo
 
kweli bara bara maeneo hayo ni mbovu sana kuanzia maeneo ya kituo cha polisi gogoni hadi maeneo ya hondogo ni mashimo ya kutisha, Mbunge wa eneo hilo mhe.Isa Mtevu ndio muda wake huu sasa wa kuanza kumaliza kero hizo, kama ulivyo sema yeye kama muwakilishi wa wananchi awabane DMDP waelekee maeneo hayo sasa maana yamesahaulika sana
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom