Mbuga 3 za Tanzania zaingia kwenye vivutio 25 bora duniani: Serengeti yaongoza, Mlima Kilimanjaro nafasi ya 12 na Mbuga ya Tarangire nafasi ya 14

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania imechaguliwa kuwa mshindi wa vivutio vya utalii duniani na kampuni ya Tripadvisor.

Tuzo hizo hutolewa na kampuni hiyo inayoshushughulika na kutoa mrejesho wa mahoteli na vivutio mbalimbali duniani.

Hifadhi tatu nchini Tanzania zimeibuka kidedea kati ya hifadhi 25 zilizotajwa kwenye tuzo hizo Serengeti ikishika nafasi ya kwanza duniani Hifadhi ya Masai Mara ya nchini Kenya imeshika nafasi ya tatu huku mbuga ya wanyama Tarangire ikishika nafasi ya 14 na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12.

Akizungumza na BBC Dira ya dunia Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Tanzania Dkt Damas Ndumbaro amesema tuzo hiyo ni yenye umuhimu mkubwa kwa Serengeti na secta ya utalii nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

"Tuzo hii tumepata ushindi kutokana na kazi nzuri tunayo ifanya ya kuhifadhi mbuga hii maarufu ya Serengeti,lakini pia na huduma bora ukiwa Serengeti unaweza ukaona Wanyama kwa urahisi na vizuri zaidi"

Serengeti pekee kwa mwaka hupokea wastani wa wageni laki tatu na nusu hadi laki tano ambao huja kushudia maajabu yaliyoko kwenye eneo hili ambalo ni urithi wa dunia ikiwa na na ukubwa wa kilomita za mraba 14750 kila mwaka hushuhudia mamilioni nyumbu ambao wanahama kutoka hifadhi Masai mara nchini Kenya ambayo nayo kwenye tuzo hizi imeshika nafasi ya tatu. Utalii kama zilivyo sekta nyingine kote duniani umeathirika na uwepo wa maradhi ya Covid-19.

Mamlaka ndani ya hifadhi zimejiwekea mkakati maalumu kuhakisha wageni wanakuwa salama muda wote wawapo hifadhini ikiwa ni Pamoja na kuweka kituo cha ukusanyaji wa sampuli, kwa ajili ya upimaji wa virusi vya corona ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti mamlaka zinasema lengo ni kuharakisha upimaji lakini pia kuwapatia muda wakutosha wageni kuwa hifadhini.

Mhifadhi mkuu wa Serengeti Masana Mwishawa anasema kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kituo hicho maalum ndani ya hifadhi hukusanya sampuli ambazo hutumwa kwenye maabara ya taifa jijini Arusha kila siku na wageni kutumiwa majibu na vyeti vyao vya uthibitisho kwa njia ya mtandao.

Tanzania imekuwa ikikosolewa kwakutotoa hadharani takwimu za maambukizi ya virusi vya corona nchini humo toka ilipofanya hivyo mwezi aprili mwaka 2020 na hata msimamo wake juu ya chanjo ya maradhi hayo ambayo inaendelea kutolewa maeneo mengine duniani.

Kwa sasa Serengeti inasheherekea ushindi wake katika kipindi hiki kigumu duniani huku ikiendelea kujizatiti kuhakikisha usalama wa wageni wake jambo ambalo linawapa watalii Imani ya kuendela na mipango yao ya kutembelea mbuga za wanyama Tanzania na hata visiwa vya Zanzibar.

Chanzo: BBC swahili

-====

Tumewakeeeera majirani wa Maasai Mara
 
Ndio yale yale, vivutio mnavyo bora kuzidi mataifa yote lakini nyie ni wale wale tu, umaskini unazidi kutamalaki na kushindwa kiuchumi na viinchi vidogo vidogo kama Kenya. Madini mnayo ya kumwaga, ardhi kubwa mara mbili ya Kenya, yaani kweli haupewi vyote, uchague moja kati ya ubongo na raslimali.
 
Serengeti imekua hifadhi bora duniani au Africa? Mimi nilivyosikia imekua hifadhi bora kwa Africa na sio duniani kama ulivyoandika.

Pamoja na yote hongera sana kwa Serengeti.
 
_117380648_a300b493-8838-42cb-bebf-543b67c4c81a.jpg

Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania imechaguliwa kuwa mshindi wa vivutio vya utalii duniani na kampuni ya Tripadvisor.

Katika tuzo hizo ambazo hutolewa na kampuni hiyo inayoshushughulika na kutoa mrejesho wa mahoteli na vivutio mbalimbali duniani.

Hifadhi tatu nchini Tanzania zimeibuka kidedea kati ya hifadhi 25 zilizotajwa kwenye tuzo hizo Serengeti ikishika nafasi ya kwanza duniani Hifadhi ya Masai Mara ya nchini Kenya imeshika nafasi ya tatu huku mbuga ya wanyama Tarangire ikishika nafasi ya 14 na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12.

Akizungumza na BBC Dira ya dunia Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Tanzania Dkt Damas Ndumbaro amesema tuzo hiyo ni yenye umuhimu mkubwa kwa Serengeti na secta ya utalii nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

"Tuzo hii tumepata ushindi kutokana na kazi nzuri tunayo ifanya ya kuhifadhi mbuga hii maarufu ya Serengeti,lakini pia na huduma bora ukiwa Serengeti unaweza ukaona Wanyama kwa urahisi na vizuri zaidi"

Serengeti pekee kwa mwaka hupokea wastani wa wageni laki tatu na nusu hadi laki tano ambao huja kushudia maajabu yaliyoko kwenye eneo hili ambalo ni urithi wa dunia ikiwa na na ukubwa wa kilomita za mraba 14750 kila mwaka hushuhudia mamilioni nyumbu ambao wanahama kutoka hifadhi Masai mara nchini Kenya ambayo nayo kwenye tuzo hizi imeshika nafasi ya tatu. Utalii kama zilivyo sekta nyingine kote duniani umeathirika na uwepo wa maradhi ya Covid-19.

Mamlaka ndani ya hifadhi zimejiwekea mkakati maalumu kuhakisha wageni wanakuwa salama muda wote wawapo hifadhini ikiwa ni Pamoja na kuweka kituo cha ukusanyaji wa sampuli, kwa ajili ya upimaji wa virusi vya corona ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti mamlaka zinasema lengo ni kuharakisha upimaji lakini pia kuwapatia muda wakutosha wageni kuwa hifadhini.

Mhifadhi mkuu wa Serengeti Masana Mwishawa anasema kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kituo hicho maalum ndani ya hifadhi hukusanya sampuli ambazo hutumwa kwenye maabara ya taifa jijini Arusha kila siku na wageni kutumiwa majibu na vyeti vyao vya uthibitisho kwa njia ya mtandao.

Tanzania imekuwa ikikosolewa kwakutotoa hadharani takwimu za maambukizi ya virusi vya corona nchini humo toka ilipofanya hivyo mwezi aprili mwaka 2020 na hata msimamo wake juu ya chanjo ya maradhi hayo ambayo inaendelea kutolewa maeneo mengine duniani.

Kwa sasa Serengeti inasheherekea ushindi wake katika kipindi hiki kigumu duniani huku ikiendelea kujizatiti kuhakikisha usalama wa wageni wake jambo ambalo linawapa watalii Imani ya kuendela na mipango yao ya kutembelea mbuga za wanyama Tanzania na hata visiwa vya Zanzibar.
 
Hao ni mabeberu, ni waongo. Hawana jema na sisi.

Usiwaamini hata kidogo.

Ndugu zetu wa damu ni wachina.
 
Ndio yale yale, vivutio mnavyo bora kuzidi mataifa yote lakini nyie ni wale wale tu, umaskini unazidi kutamalaki na kushindwa kiuchumi na viinchi vidogo vidogo kama Kenya. Madini mnayo ya kumwaga, ardhi kubwa mara mbili ya Kenya....yaani kweli haupewi vyote, uchague moja kati ya ubongo na raslimali.
Wivuuuuuuuuu

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
SERENGETI IMEKUA HIFADHI BORA DUNIANI AU AFRICA? MIMI NILIVYOSIKIA IMEKUA HIFADHI BORA KWA AFRICA NA SIO DUNIANI KAMA ULIVYOANDIKA.
PAMOJA NA YOTE HONGERA SANA KWA SERENGETI.
Ni duniani tyu kwani huko duniani hawajaskia ......halafu ndo wanakuja hao wazungu kutalii huku nchi njema ya maziwa na asali ......so hii ni kwadunia yote .....sio africa tyuu
 
Ndio yale yale, vivutio mnavyo bora kuzidi mataifa yote lakini nyie ni wale wale tu, umaskini unazidi kutamalaki na kushindwa kiuchumi na viinchi vidogo vidogo kama Kenya. Madini mnayo ya kumwaga, ardhi kubwa mara mbili ya Kenya....yaani kweli haupewi vyote, uchague moja kati ya ubongo na raslimali.
Sio kwa Pombe
 
Back
Top Bottom