Mbu anauma au anadunga?

GodHaveMercy

Member
Apr 25, 2010
35
2
Mara chache chache, nimekua nikiwafuatilia akina Kibonde na Gadna, Clouds FM, ktk kipindi chao kinachoanza karibu kila siku jioni. Siku moja waligusia utofauti wa matumizi na utofauti wa maana ya maneno kati ya lugha moja na nyingine, au sehemu moja na nyingine. Hapo ndipo waligusia kuwa, wakati huku Tanzania bara tumezoea kusema "nimeumwa na mbu", kumbe kule kwa wenzetu, Zanzibar ni tofauti. Kule utasikia "nimedungwa na mbu". Bado sina uhakika nani yupo sahihi kati ya mtanzania bara na mzanzibar. Naomba mwenye kufahamu animegee. MBU AUMA AU ADUNGA??? Kiswahili hicho!
 
nakuomba leo ukirudi nyumbani,usipulize dawa ya mbu wala usitumie neti halafu usijifunike shuka. KESHO ASUBUHI NITAKUULIZA MBU ANAUMA AU ANADUNGA?
 
Vyote kwa vyote, malaria haiwezi kukingwa kwa matamasha, makongamano na show zinazohudhuriwa na wanamuziki ambao hawana hata ujumbe wa kuelimisha jamii juu ya malaria

MALARIA INAKUBALIKA PALE TU UNAPOENDELEZA MATAMASHA
 
Kwanza si kweli kuwa kule zanzibar wanatumia kudungwa na mbu.Najuwa kuwa nimetafunwa na mbu linatumika zaidi.Sijui lipi ni sahihi kati ya kudungwa,kuumwa na kutafunwa.
Hata hivyo kwamba kule zanzibar wanatumia kudungwa,inategemea ulizungumza na watu wa ngapi na wazaliwa wa vijiji gani,kwani wapo wamakonde pia ambao ndio hutumia "nimenung'wa na mumbu".
 
Vyote kwa vyote, malaria haiwezi kukingwa kwa matamasha, makongamano na show zinazohudhuriwa na wanamuziki ambao hawana hata ujumbe wa kuelimisha jamii juu ya malaria

MALARIA INAKUBALIKA PALE TU UNAPOENDELEZA MATAMASHA

Mungu akubariki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom