Mbozi: Mwanafunzi ajinyonga kufuatia adhabu aliyopewa baada ya kuiba begi la mwanafunzi mwenzake

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Mwanafunzi Magreth Kayuni (15) wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Vwawa iliyopo wilayani Mbozi mkoani wa Songwe, amekutwa amejinyonga jikoni leo asubuhi kufuatia adhabu ya kupigwa na bibi yake baada ya kuiba begi la mwanafunzi mwenzake.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mdogo wa marehemu, Abraham Kalinga, amesema mapema leo asubuhi walipoamka bibi yao alimuagiza apike maharage, huku yeye akifanya kazi ya kufagia uwanja, marehemu Magreth Kayuni baada ya kupika maharage aliaga kuwa anaenda kuchota maji na ndipo alipofikia uamuzi wa kujinyonga.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Seleman Mgala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limewastua wakazi wa eneo hilo ambapo amesema tukio kama hilo halijawahi kutokea mtaani hapo na hiyo ni mara ya kwanza.
 
Afadhalu ameji kill mwenyewe kuliko angewekea familia yote sumu ya panya
 
Serikali inabidi iongeze juhudi kwenye afya ya akili..
Depression,anxiety n.k are real.
Unaweza kumshangaa mtu kujinyonga lakini huo ni ugonjwa kama malaria na typhod..
Unaweza kukupata hata wewe..
unachozungumza ni kweli kabisa..stress mbaya sana
 
Najaribu kuunganisha dots kuhusu matukio haya mawili nashindwa kupata muafaka!
 
Nikajua labda adhabu hiyo alipewa na mwalimu.

Huyo bibi ni noma. Yaani hadi mjukuu anaamua kujinyonga?

Ila nahisi roho ya mauti illikuwa imeshamwandama. Adhabu ikawa ni sababu tu. Yamkini huyo bibi angeongeza kumwadhibu angemuua:D
 
Wanaona wazee wao kuuana ni jambo LA kawaida hata watoto hawaoni hatari ,saikolojia muhimu sana ,
 
Kwa kuwa ameahakutwa haina shida maana atazikwa tuu mbaya ni ike asingeonekana kabisa
 
Tatizo letu humu kuna mahakimu na kuna askari magereza na hata wanaojifanya kuamua roho itoke lini na kwa sababu zipi
Kutoa majibu na kuchangia ili mradi tu mtu kasema eti kajinyonga basi ndio linakuwa hitimisho
Utakuta hapo ndio mwisho kuwa alijiuwa kwa ajili ya adhabu ya begi
Lakini kwa kuwa huwa hakuna uchunguzi na mahakimu wamo kwenye jamii basi tena
Kama kauwawa na kunyongwa bado sababu ni hiyo kajiuwa.
Waswahili wanaficha mengi sana na wengine huwa wanauwa wazazi wao au waume au wake lakini kwa kuwa hakuna postmodern watu wanaweka msiba na kulia sana na kuzika
 
UMASKINI mbaya sana, alitamani begi hana uwezo kaamua kuiba, kukosa upendo na malezi ya wazazi yalimjaza sonona, inawezekana bibi alikuwa mkali kupitiliza kwa kuona analemewa na mzigo wa kulea wajukuu.. Mungu anafahamu ulivyoishi anajua akuweke wapi mtoto.
 
Kwahiyo alivyoadhibiwa ndio kuna uhusiano gani na kuamua kujinyonga sasa, it doesn't make sense? Kwahiyo alivyojinyonga ndio anataka bibi yake ajute kumchapa? Au kwamba iwe fundisho kwetu kwamba mtu akiiba asiadhibiwe?
 
Wazazi,walezi walimu na jamii kwa ujumla wake,muwe makini sana katika kuhukumu na kutoa adhabu kwa mtu yoyote.Awe mtoto,kijana wa kati,mtu mzima hata mzee.Kila adhabu iwe ya kupiga,kusoma au yoyote ile itolewe kwa tahadhari kubwa sana.
 
Serikali inabidi iongeze juhudi kwenye afya ya akili..
Depression,anxiety n.k are real.
Unaweza kumshangaa mtu kujinyonga lakini huo ni ugonjwa kama malaria na typhod..
Unaweza kukupata hata wewe..
Mkuu well said Depression na anxiety inachukuliwa kama tatizo la kawaida tu kumbe ni issue serious sana kwenye jamii yetu.
 
Back
Top Bottom