Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,496
- 41,003
Viongozi wa upinzani mmefanya mengi, mmepitia mengi na magumu, na kwa kuyapitia hayo, bila shaka mmejifunza mengi.
Kinachonisikitisha na nadhani kuwasikitisha walio wengi, ni kushindwa kutambua nguvu ya UMOJA. Timefundishwa toka shule za msingi, tuna misemo na nahau zinazoelezea umuhimu na nguvu ya Umoja.
Ukilinganisha vyama vya upinzani na CCM, vyama vya upinzani ni wanyonge. Kuna msemo usemao:
"Fimbo ya mnyonge ni UMOJA"
Kwa nini hamtaki kuitumia fimbo hii kumtandika anayewaonea Goliath?
Goliath ana umbile kubwa, ana jeshi, ana polisi, ana TISS, ana TV na redio, ana viwanja kila kona, kubwa zaidi ana mamlaka. Utamshindaje wewe mwenye umbile dogo, huna mamlaka ya kumwamrisha hata sungusungu? Ina maana hamjui:
"Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"?
Ninachoshindwa kuwaelewa viongozi wa upinzani:
Kwa nini hamuungani? Kwa nini hamshirikiani na kushikamana?
1) Je, ni ubinafsi?
2) Tamaa ya madaraka na ukubwa?
3) Ni kushindwa kuielewa nadharia ya umoja?
4) Ni kukosa maono?
Nina hakika, hata haya tunayoyapitia na kuyaona sasa, ni kutokana na udhaifu wa vyama vya upinzani katika kutengeneza umoja wenye nguvu. Na adui yenu hana wasiwasi nanyi, hana mashaka nanyi ya kuwafanyia chochote kwa sababu anajua hamjashikamana.
Kwa kawaida, dhuluma huleta umoja lakini hapa kwetu haiwi - kwa nini?
Mimi nilitarajia, hata kwenye hili la kujitoa kwenye huu mchakato mchafu wa uchaguzi wa serikali, vyama vya upinzani kama vile CHADEMA, ACT, NCCR, CHAUMA, n.k. vingetoka kwa pamoja, na kutoa kauli ya pamoja, na kuamua kuchukua hatua za pamoja kuliko kila chama kutoa kauli kikiwa pekee yake.
Miaka yote hii - Mbowe, Zito, Rungwe, Mbatia, mmeshindwa kujenga umoja wenye nguvu, umoja ambao ni tishio? Kuwa na chama zaidi ya kimoja, ni jambo jema maana inaweza kutokea kama kilichoitokea CUF, halafu options zikakosekana.
Ushauri wangu, mzee Hashim Rungwe, wakutanishe vijana wako ili kujenga alliance yenye nguvu. Alliance itakayoonekana kama ni chama kimoja cha siasa chenye idara za CHADEMA, ACT, NCCR, CHAUMA, n.k. Matamko yote, maelekezo yote yatolewe na hii alliance. Punguzeni nguvu za vyama vyenu ili mpeleke nguvu kwenye alliance.
Na alliance itoke na tamko moja
"Sisi ni wamoja. Akishambuliwa mmoja, tumeshambuliwa wote. Akifungwa mmoja kwa kuonewa tumeonewa wote. Akidhulumiwa mmoja tumedhulumiwa sote"