Mbowe, Zitto na Mbatia mnashindwa wapi?

Viongozi wa upinzani mmefanya mengi, mmepitia mengi na magumu, na kwa kuyapitia hayo, bila shaka mmejifunza mengi.

Kinachonisikitisha na nadhani kuwasikitisha walio wengi, ni kushindwa kutambua nguvu ya UMOJA. Timefundishwa toka shule za msingi, tuna misemo na nahau zinazoelezea umuhimu na nguvu ya Umoja.

Ukilinganisha vyama vya upinzani na CCM, vyama vya upinzani ni wanyonge. Kuna msemo usemao:

"Fimbo ya mnyonge ni UMOJA"
Kwa nini hamtaki kuitumia fimbo hii kumtandika anayewaonea Goliath?

Goliath ana umbile kubwa, ana jeshi, ana polisi, ana TISS, ana TV na redio, ana viwanja kila kona, kubwa zaidi ana mamlaka. Utamshindaje wewe mwenye umbile dogo, huna mamlaka ya kumwamrisha hata sungusungu? Ina maana hamjui:

"Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"?

Ninachoshindwa kuwaelewa viongozi wa upinzani:

Kwa nini hamuungani? Kwa nini hamshirikiani na kushikamana?

1) Je, ni ubinafsi?
2) Tamaa ya madaraka na ukubwa?
3) Ni kushindwa kuielewa nadharia ya umoja?
4) Ni kukosa maono?

Nina hakika, hata haya tunayoyapitia na kuyaona sasa, ni kutokana na udhaifu wa vyama vya upinzani katika kutengeneza umoja wenye nguvu. Na adui yenu hana wasiwasi nanyi, hana mashaka nanyi ya kuwafanyia chochote kwa sababu anajua hamjashikamana.

Kwa kawaida, dhuluma huleta umoja lakini hapa kwetu haiwi - kwa nini?

Mimi nilitarajia, hata kwenye hili la kujitoa kwenye huu mchakato mchafu wa uchaguzi wa serikali, vyama vya upinzani kama vile CHADEMA, ACT, NCCR, CHAUMA, n.k. vingetoka kwa pamoja, na kutoa kauli ya pamoja, na kuamua kuchukua hatua za pamoja kuliko kila chama kutoa kauli kikiwa pekee yake.

Miaka yote hii - Mbowe, Zito, Rungwe, Mbatia, mmeshindwa kujenga umoja wenye nguvu, umoja ambao ni tishio? Kuwa na chama zaidi ya kimoja, ni jambo jema maana inaweza kutokea kama kilichoitokea CUF, halafu options zikakosekana.

Ushauri wangu, mzee Hashim Rungwe, wakutanishe vijana wako ili kujenga alliance yenye nguvu. Alliance itakayoonekana kama ni chama kimoja cha siasa chenye idara za CHADEMA, ACT, NCCR, CHAUMA, n.k. Matamko yote, maelekezo yote yatolewe na hii alliance. Punguzeni nguvu za vyama vyenu ili mpeleke nguvu kwenye alliance.

Na alliance itoke na tamko moja
"Sisi ni wamoja. Akishambuliwa mmoja, tumeshambuliwa wote. Akifungwa mmoja kwa kuonewa tumeonewa wote. Akidhulumiwa mmoja tumedhulumiwa sote"
Ili waungane nilazima kuwe na nia Moja na kusiwe na unafiki.
Siasa zaidi yakuwa ajira huku kwetu hazina Malengo mengine
 
Wanaosema watashiriki uchaguzi hawajui chochote kuhusu madhila wanayokutana nayo wanaogombea wa vyama vya upinzani wanaogombea ndiyo maana hawa wapinzani wasio na mgombea hata moja wanasema watashiriki kumbe hawajui hata kinachendelea
 
Kuna haja ya kuwakumbusha ajenda ambazo zitawapa hamasa wananchi kujiandika kwanza kwenye uchaguzi mkuu 2020.

Mimi narusha karata ya kwanza. Nayo ni mabadiliko ya kisera ktk ofisi ya Ofisi ya mpepezi mkuu wa makosa ya jinai, kuwa Sera kandamizi ya kumkamata na kumshitaki mtuhumiwa pasipo kuwapo na ushahidi, au kama ushahidi haijakamilika.
 
Labda ungetwambia Maalim Seif amefanya nini?

Kwa wapenda mabadiliko waliamini kwa kuwa Maalim Seif alikuwa sehemu ya Ukawa na alipingana na Lipumba juu ya CUF kuachana na UKAWA, sisi wapenda mabadiliko tuliamini kuwa kwa kutoka kwake CUF basis angejiunga na CHADEMA kuwahibitisha watz kuwa CHADEMA hakuna tatizo. Lkn kwa kujiunga kwake chama kidogo ACT, ni sawa na kuwathibitishia watz kuwa ile hofu iliyomfanya Prof Lipumba aachane na UKAWA, kweli IPO. Lkn kwa kuwa hofu hiyo haipo, zaidi ya ubinafsi na kuangalia matumbo na vyeo, kitendo chake cha kujiunga na ACT ameidhoofisha kambi ya upinzani. Na huko sasa yy kama kiongozi mwandamizi, kwa kuwa uchaguzi huu ni wa watanganyika, basi yy so sehemu ya business yake, atatia neno iwapo tu jambo hilo linahusu znz tu
 
Viongozi wa upinzani mmefanya mengi, mmepitia mengi na magumu, na kwa kuyapitia hayo, bila shaka mmejifunza mengi.

Kinachonisikitisha na nadhani kuwasikitisha walio wengi, ni kushindwa kutambua nguvu ya UMOJA. Timefundishwa toka shule za msingi, tuna misemo na nahau zinazoelezea umuhimu na nguvu ya Umoja.

Ukilinganisha vyama vya upinzani na CCM, vyama vya upinzani ni wanyonge. Kuna msemo usemao:

"Fimbo ya mnyonge ni UMOJA"
Kwa nini hamtaki kuitumia fimbo hii kumtandika anayewaonea Goliath?

Goliath ana umbile kubwa, ana jeshi, ana polisi, ana TISS, ana TV na redio, ana viwanja kila kona, kubwa zaidi ana mamlaka. Utamshindaje wewe mwenye umbile dogo, huna mamlaka ya kumwamrisha hata sungusungu? Ina maana hamjui:

"Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"?

Ninachoshindwa kuwaelewa viongozi wa upinzani:

Kwa nini hamuungani? Kwa nini hamshirikiani na kushikamana?

1) Je, ni ubinafsi?
2) Tamaa ya madaraka na ukubwa?
3) Ni kushindwa kuielewa nadharia ya umoja?
4) Ni kukosa maono?

Nina hakika, hata haya tunayoyapitia na kuyaona sasa, ni kutokana na udhaifu wa vyama vya upinzani katika kutengeneza umoja wenye nguvu. Na adui yenu hana wasiwasi nanyi, hana mashaka nanyi ya kuwafanyia chochote kwa sababu anajua hamjashikamana.

Kwa kawaida, dhuluma huleta umoja lakini hapa kwetu haiwi - kwa nini?

Mimi nilitarajia, hata kwenye hili la kujitoa kwenye huu mchakato mchafu wa uchaguzi wa serikali, vyama vya upinzani kama vile CHADEMA, ACT, NCCR, CHAUMA, n.k. vingetoka kwa pamoja, na kutoa kauli ya pamoja, na kuamua kuchukua hatua za pamoja kuliko kila chama kutoa kauli kikiwa pekee yake.

Miaka yote hii - Mbowe, Zito, Rungwe, Mbatia, mmeshindwa kujenga umoja wenye nguvu, umoja ambao ni tishio? Kuwa na chama zaidi ya kimoja, ni jambo jema maana inaweza kutokea kama kilichoitokea CUF, halafu options zikakosekana.

Ushauri wangu, mzee Hashim Rungwe, wakutanishe vijana wako ili kujenga alliance yenye nguvu. Alliance itakayoonekana kama ni chama kimoja cha siasa chenye idara za CHADEMA, ACT, NCCR, CHAUMA, n.k. Matamko yote, maelekezo yote yatolewe na hii alliance. Punguzeni nguvu za vyama vyenu ili mpeleke nguvu kwenye alliance.

Na alliance itoke na tamko moja
"Sisi ni wamoja. Akishambuliwa mmoja, tumeshambuliwa wote. Akifungwa mmoja kwa kuonewa tumeonewa wote. Akidhulumiwa mmoja tumedhulumiwa sote"
Watanzania wamewadharau ndio chanzo cha kufeli kwao
 
Dhana ya mfumo wa vyama vingi ina lengo la kuruhusu na kuwezesha kushamiri kwa mawazo na mikakati tofauti (mbadala) ya kujiletea maendeleo na kusimamia maslahi ya jamii husika. Kwa msingi huo, kutaka muungano wa vyama ili kukishinda chama kimoja (tawala) ni kuminya upeo wa kisiasa na kukaribisha udikteta wa fikra (totalitarianism).

Hatuhitaji miungano ya vyama. Tunahitaji kushindanisha sera na mikakati ya vyama ili kuchagua kilicho bora kabisa kushika uongozi wa nchi. Tena lengo kuu liwe kutuwezesha wananchi kubadili uongozi na vyama kwa kadiri tutakavyoona inastahili. Sio huu ukiritimba uliosimikwa na mfumo wa CCM tangu uhuru.

Lakini kufikiria kuiondoa CCM madarakani kama lengo kuu pekee ni mtazamo finyu sana na wa hatari. Kwanza tayari tunafahamu baadhi ya viongozi na wanasiasa wa upinzani, kama walioko CCM, hawaaminiki - wana malengo ya kibinafsi sana; huwezi kutarajia ushirikiano wenye tija baina ya watu wa aina hii na wanasiasa makini wa upinzani. CCM ikiondoka kwa ushirikiano wa aina hii, tutajikuta tunahangaika na “vikao vya maridhiano na kugawana madaraka” kama vinavyoendelea Sudani ya Kusini.
 
Kama hawatakubali kufanya kazi pamoja dawa ni kuwachomoa wao ili muweke wanaoshirikiana

Huwezi kuwachomoa kwa sababu ya kugoma kushirikiana kwani hakuna mahali kwenye katiba zao kuna lazimisha kushirikiana, hilo ni jambo la hiari na linahitaji kuaminiana na kuridhiana zaidi kuliko kulazimishana.
 
sasa mkuu kama wananchi wanataka waungane itakuwaje? au wananchi wawape adhabu kwa kuendelea kuiamini CCM?
 
Huwezi kuwachomoa kwa sababu ya kugoma kushirikiana kwani hakuna mahali kwenye katiba zao kuna lazimisha kushirikiana, hilo ni jambo la hiari na linahitaji kuaminiana na kuridhiana zaidi kuliko kulazimishana.

Kubuniwa kwa Ukawa ilikuwa hatua kubwa kuelekea ushirikiano. Lakini ndani ya ushirikiano huo walitokea baadhi ya waasisi wake ambao ghafla waligeuka na kuamini kuwa ni bora kushirikiana na ccm kuliko UKAWA yenye Lowassa ndani yake! From nowhere to these opposition politics gurus Lowassa as an individual became far more dangerous than ccm! Nani alitarajia kuwa hiyo miamba ya upinzani inaweza kurubuniwa kirahisi hivyo? Ghafla kazi ya hao watu ikawa ni kubomoa kazi ya mikono yao wenyewe! Nadhani mambo kama haya huchangia kufanya vyama kuwa na hofu. Wanasiasa wengi wa nchi hii wanayo bei.
 
Back
Top Bottom