Mbowe, Zitto, Mnyika, Tundu tusaidieni vijana kulizungumzia hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe, Zitto, Mnyika, Tundu tusaidieni vijana kulizungumzia hili

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by itagata, Jun 28, 2012.

 1. i

  itagata JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  SEKRETARIATI ya ajira ilipoanzishwa moja ya lengo lake ilikuwa ni kuajiri watu wenye sifa ikiwa ni pamoja na kupunguza urasmu uliokuwa ukitokea wakati taasisi zinazojitegemea na mamlaka za serikali za mitaa zilipokuwa na jukumu la kuajiri watumishi wake.
  Pamoja na malengo hayo mazuri, hali imekuwa tofauti sana na ni afadhar mamlaka za serikali za mitaa pamoja na taasisi zinazojitegemea zilipokuwa na mamlaka ya kuajiri wafanyakazi wake, hali ilivyo sasa katika sekretariati ya ajira ni mbaya, bila kujuana au kutoa kitu kidogo usitegemee kupata kazi, imekuwa ni dili kubwa kwa ma-HR waliopo hapo na wenye jukumu la kuajiri.
  Ninachojiuliza jamani wana JF kweli hadi Afisa Mtendaji wa Kijiji anasafiri kutoka Kigoma kuja Dar kwa ajili ya kufanya interview? Mi napingana sana na utaratibu huu kwani tunaoumia wengi ni watoto wa masikini tunaoka mikoa ya mbali na Dar.
  Kwanini serikali isizipe na kuimarisha mikoa ili iweze kuajiri wafanyakazi wake badala ya kutegemea makao makuu ya secretariat pekee? Kama ni lazima utumishi waendelee kuajiri basi wachague baadhi ya kada angalau zenye vyeo vya juu ili wafanyakazi wenye vyeo vidogo waajiriwe na mamlaka za mikoa badala ya wote kutegemea kufanyiwa usaili na makao makuu ya utumishi.
  Nina amini kuwa sisi watoto wa masikini tuliomaliza vyuo vikuu ambao hatuna uwezo wa “kuhonga” milioni moja ili tupewe kazi na tunaochangiwa na kijiji ili tupate nauli ya kuja Dar kufanya usaili ndio tunaoumia.
  Nawaomba wapiganaji wetu, Zitto, Mbowe, Tundu, Mnyika na wapiganaji wengine wenye mapenzi mema na maisha ya vijana walipigie kelele hili ili angalau interview ziwe zinafanyika kwa ngazi ya kanda au mikoa ili kuwapa fursa watoto wa masikini kupata ajira.
  Nimeamua kuandika mawazo yangu haya kwenu wana JF kwani nimefanya interview 3 ambazo nina uhakika nilifanya vizur lakini mpaka leo sijapata hiyo ajira, na ninatoka mikoa ya mbali nalazimika kusafiri siku mbili ili kufika Dar.
   
 2. p

  panadol JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mleta hoja acha uzushi kuzushia watu kama wanakula rushwa inamaana wote waliopata ajira kupitia utumishi wamehonga?huo ni uzushi sana ukweli ni kwamba pale watu wanapata ajira kwa uwezo wao mimi nina jamaa zangu wameajiriwa serikalini kupitia utumishi bila hongo yoyote ukikosa ujue umekosa hukufanya vizuri aliyekwambia wewe lifanya vizuri kwa interview zako zote tatu ni nani,wewe umejuaje? Wangapi wanamaliza shule wakijiamini watafaulu na matokeo yakitoka huwa wanakuwa wamefeli,mbona hawalaumu iweje wewe ulaumu au unapewa maswali na mitihani ya interview? Acha uongo na unafiki jijue unakosa hujakidhi viwango,kama uko vizuri kwa nini private sekta zisikuajili unakomalia serikalini tu?acha uzushi jipange vizuri siku moja utafanikiwa lakini si kulalama na kusingizia watu wanaingia kwa rushwa na kubebwa kumbe wewe mwenyewe unafeli interview kwa kutokujiandaa vizuri,suala la interview ziwe zinafanyikia kwa kanda hilo naliafiki ili kuokoa gharama za watu wote kuja dar,mengine ya rushwa na undugu siyaafiki ni uzushi mtupu na kuchafua watu!
   
 3. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Je unaconclude kuwa kuna rushwa 7bu umefanya interview 3 bila mafanikio au 7bu kuna mtu alikuambia ametoa rushwa na kufanikiwa?
  Angalia vizuri hizo red hapo juu kwani zina mambo sana
  Kama wakiruhusu kanda kuajiri haina maana kuwa gharama zitapungua bali zitaongezeka zaidi, mfano Mtwara wakitangaza nafasi yoyote na mtu wa Bukoba akaomba na kuitwa kwenye interview unadhani itakuwaje? ukisema kila watu waajiriwe kwenye Mkoa wao utapalilia Ukabila na kuvunja umoja wetu watanzania. Ajira za serikalini ni haki ya kila raia bila kujali mkoa au ukanda atokako mwombaji.

  Majina ya Wabunge uliyoyataja hujayatendea haki, ilikuwa vizuri uombe wabunge kwa ujumla wao waliisemee hii unayodhani ni kero kwako.Yeyote mbunge atakayeliona ombi lako na kuliafiki atalisemea.

  Kumbuka kuwa nafasi za ajira ni chache kuliko Wahitaji,hivyo unapokosa usichukulie umeonewa wakati wote maana hata wenzako huwa wanajibu vizuri interview kama au zaidi ya wewe.

  Kama ni issue ya rushwa basi hiyo inabidi ichunguzwe au wewe mwenyewe wakikuomba hao ma HR nenda kawachukulie pesa TAKUKURU wapelekee wakamatwe ili kukomesha tabia na kuondoa mbegu hii mbovu.

  Au tuwaombe tume ya ajira wajaribu kuweka uwazi katika interview process, au wachunguzwe kwa tuhuma wanazotuhumiwa nazo
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  Pengine kazi yako uliyopata haikuwa chagua la wenye network.Shukuru kwa hilo?
   
 5. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  huyu bwana itagata ,anonesha anatabia za kulalamika sana na unafiki ndani yake .anataka psrs waonekana wa image mbaya kwa wata nzania kwa sabaubu hajapata ajira ,yeye kama ameona kuna dalili za rushwa kwa nini asipeleke taarifa takukuru
  alafu ana usiasa ndani yake kwanini ?zitto,mbowe,mnyika kwani hao ndo wawakilishi pekee? alafu si kila interview lazima utakayo fanya upate!
  but usikate tamaa ipo siku tutapata kijana mwenzangu
   
 6. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mbowe, zito, mnyika, tundulisu..HAO NDO WABUNGE PEKEE UNAOTAKA WAKUSAIDIE? KWANINI USISEME WABUNGE WOTE KWA UJUMLA..

  Pia kazi zinazotangazwa ni chache na watu ni weng ukikosa haimanish umeonewa bali kuna wakali zaid yako kumbuka ukizidiwa hata point moja anachukuliwa aliekuzid,na ikitokea mko draw, anangaliwa mwenye extra atributes hata moja 2..so jipange zaid
   
 7. u

  uwiii Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sitaki kuamini hilo kabisaaaa!Kuna watu wanapata kazi bila kufahamiana na mtu wala kuwa na cha njano kupitia taasisi hiyo.Nafikiri mimi(Bado ni nasaka job) na wewe tujipange tu upya,tutapata tu siku moja hizo nafasi na sisi.
   
 8. i

  itagata JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  nashukuru kwa maoni yako kwa mtizamo wako, ni kweli sio wote wanaopata kazi kupitia utumishi wanahonga, lakini si jambo la kupinga kuwa hakuna rushwa katika mchakato wa kupata ajira kupitia utumishi. najua umetumia maneno makali katika kuchangia uzi huu kwani yawezekana wewe mwenyewe ni sehemu ya hao wa utumishi, ila kwa taarifa yako kama hujui, nina rafiki yangu ambae alifanya usaili mara mbili akakosa, mara ya tatu akatafuta mtu akamuunganisha na wahusika akatoa "mpunga" huyo mhusika akalisimamia jina lake kuanzia kwenye '' k-ushort list'' mpaka interview zote na sasa yupo kazini. una haki yako kupinga lakini ukweli ndo ulivyo.
   
 9. i

  itagata JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Samahani kama ntakuwa nimeeleweka tofauti kwa kuwataja hao Majemedali wetu wachache, lakini katika kazi yoyote ili ifanyike lazime kuwe na viongozi, hawa nimewataja kama makamanda wa mstari wa mbele katika mapambano ya kuleta haki! kama uliusoma vizuri uzi wangu, nilimalizia na kusema ''na wapiganaji wengine'' hii inaamanisha sio wao peke yao.
   
 10. josam

  josam JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Tanzania hii, organisation zote za serikali BILA RUSHWA HAKUNA HUDUMA!!!

  Bodi husika inatakiwa kulipa gharama zote za usafiri, malazi na chakula kwa muda wote wa interview.
   
Loading...