Mbowe, Zitto, Lissu na Peter Msigwa wanakubaliana Magufuli alijenga Nidhamu Serikalini. Wakumbuke nidhamu haiji kwa kuchekeana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,898
141,836
Kitu kimoja ambacho Viongozi wakuu wote wa Upinzani wanakubaliana ni kwamba hayati Magufuli aliimarisha nidhamu ya Watumishi wa Umma na nidhamu ya serikali kwa Wananchi Wote.

Wanapopongeza hili wajue pia Nidhamu haiji kwa kuchekeana bali hutengenezwa kwa mfumo wa kimkakati.

Ni katika kutengeneza Nidhamu ndipo Yesu alipindua meza za Wauza njiwa na Wabadili Fedha pale Hekaluni.

RIP JPM
 
Hiyo nidhamu kwani haipo Kwa Sasa? Kuna mtu anaweza thibitisha?

Mwisho tupime matokeo ya uchumi awamu ya 6 na awamu ya 5 hicho ndio Kilimo Cha nidhamu ya Watumishi mengine ni upuuzi usio na maana
 
Kujenga nidhamu sio lazima kuua watu, sio lazima kudhulumu watu, sio lazima kuvuruga uchumi na sio lazima kutesa watu.

Kuna namna nyingi ya kujenga nidhamu
 
Nidhamu haiji kwa kuua wanaokukosoa wala nidhamu haiji kwa kukwapua mapesa ya Plea Bargain na kuyaficha China.
 
Back
Top Bottom