Mbowe, Zitto kutikisa Kahama na Tarime leo

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Viongozi wakuu wa siasa za Tanzania Freeman Mbowe na Zitto Kabwe leo wataunguruma katika miji miwili tofauti nchini.

Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Freeman Mbowe atakuwa Kahama kumnadi mgombea wa Udiwani wa kata ya Bugalama kwa tiketi ya Chadema huku Kiongozi wa chama cha ACT Zitto Kabwe akiwa Tarime kumnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Turwa kwa tiketi ya Chadema.

Mikutano ya wanasiasa hawa popote inapofanyika mara nyingi imekuwa ikichukua sura ya kitaifa kutokana na nyadhifa zao na pia uwezo wao wa kuelezea maswala kadhaa ya kitaifa.

Tangu jana kumekuwa na hekaheka nyingi katika miji ya Tarime na Kahama huku wananchi wakiwa na hamu kubwa ya kuwasikiliza viongozi hawa wanaoonekana mihimili ya upinzani nchini.

Zitto anatarajiwa kusindikizwa na viongozi kadhaa wakiwemo viongozi wa Chadema na ACT mkoa wa Mara akiwemo Mbunge wa viti maalum Geita Chadema Upendo Peneza.

Mwenyekiti Mbowe atasindikizwa na maafisa kadhaa wa makao makuu na Kanda wa Chadema wakiwemo wabunge kadhaa wakiongozwa na Mwenyekiti Kanda ya Serengeti John Heche

Ulinzi wa vijana wa Chadema maarufu kama Red Brigade umeimarishwa kote kuzunguka miji ya Tarime na Kahama kama ishara ya kuwalaki viongozi hao.
 
Mbowe ni shoka jamani. Ana influence, sema hawa fisiem na serekali yao ndo wanajaribu kumziba mdomo kwa kukataza wana siasa kufanya siasa.

Peopleeeeeeez, poooweerr!
 
CCM kwa CHADEMA imekuwa rojo kabisa wamebaki kuwatumia vyombo vya dola..
Iko wazi hiyo CCM kwa sasa haina uwezo wowote wa kupambana na Chadema.Kama sio vyombo vya dola hawana uwezo wa kushinda hata kata moja
 
Back
Top Bottom