Mbowe: Wabunge wote wa CHADEMA kutokushiriki vikao vya bunge kuanzia kesho, wataelekea Arusha!

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Hii ni kauli ya mwenyekiti wa taifa wa chadema mheshimiwa Freeman Mbowe akihojiwa na mwandishi wa channel ten.
Hivyo wabunge wa chadema hawatahudhuria kikao cha bajeti hapo kesho na badala yake wataungana na wana wa arusha kuomboleza na kufariji wafiwa.
 
Ndugu wana jamii forum habari nilizozipata hivi punde ni kuwa kuanzia kesho wabunge wote wa CDM hawatahudhuria vikao vya bunge na badala yake wataelekea Arusha kwa ajili ya maombolezo na kushiriki msiba wa watu 2 waliopoteza maisha ktk mlipuko wa jana Soweto
 
Mh.mbowe amesema wabunge wote wa CHADEMA hawatashiriki bunge kesho watakuwa Arusha kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi pamoja na kushiriki mazishi ya waliouawa na bomu.source:chanel ten.
 
Mh Mbowe amesema wabunge wote wa chadema kutokuingia katika vikao vya bunge kuanzia kesho na watakuja Arusha kushiriki katika maziko na kuwafariji majeruhi.

source: CHALLEN TEN habari ya saa moja usiku huu
 
mkuu hiyo ni kauli ya kambi rasmi? tupe updates zaidi ili wa mbali tuhabarike naona habari iko nusu nusu mkuu!
 
Wabunge wote wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA HAWATAUTHURIA VIKAO VYA BUNGE MJINI DODOMA MPAKA WAMALIZE SHUGHULI ZA MSIBAMKOANI ARUSHA. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Taifa chadema Freeman Aikael Mbowe..
 
safi kamanda anawajali wananchi wake hawa magaidi ya ccm waende wakapange ugaidi wao
 
Mmefanikiwa kama rank za fifa mmepanda kwa nafasi 50 juu. Lkn kwa staili hii mtamwaga damu nyingi sana kwa kukipatia umaarufu chama chenu
 
Si wabunge Wa Chadema tu bali inatakiwa Wabunge wote. Hili ni tukio la Taifa. Watu wamepigwa bomu katika mkutano wa siasa. Nasubili kwa hamu kusikia wabunge wa CCM wakipiga meza au kuzomea hatua hii ya Chadema kutoingia bungeni kesho
 
Mbowe kama kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni (KUB) ametoa maamuzi ya kustaajabisha kuhusu shughuli za mazishi zinazo pangwa kufanywa kesho kwa wale walio poteza maisha katika tukio la mlipuko Arusha.

Mbowe ameagiza kuwa, kesho wabunge wote wa CHADEMA hawata hudhulia kwenye kikao cha bunge na badala yake wote wataenda kuhudhulia mazishi ya wahanga waliopoteza maisha kwenye tukio hilo la kinyama.

Je, kukosa kuhudhulia kwa wabunge wa CHADEMA kwenye kikao cha kesho kwa ajili ya shughuli hiyo ya mazishi, ni sahihi?
 
mkuu hiyo ni kauli ya kambi rasmi? tupe updates zaidi ili wa mbali tuhabarike naona habari iko nusu nusu mkuu!

Hiyo ni kauli ya kamanda wa anga Mh. sana ninaemheshimu Freeman Aikaeli Mbowe. Source Chanel ten news
 
Si wabunge Wa Chadema tu bali inatakiwa Wabunge wote. Hili ni tukio la Taifa. Watu wamepigwa bomu katika mkutano wa siasa. Nasubili kwa hamu kusikia wabunge wa CCM wakipiga meza au kuzomea hatua hii ya Chadema kutoingia bungeni kesho

makinda aliunda timu yake feki ili kutoa pole kwa wahanga wa bomu la olasiti.......ni timu iliyoenda kufaidi perdiems tu...wiki chache baadae tunashuhudia haya
 
Back
Top Bottom