Mbowe vs Lissu ni mtihani kwa viongozi na wana CHADEMA

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,159
27,194
Katika mapambano ambayo sio rasmi jakuwa hapo ni hili la mbowe na lissu. Viongozi na Wanachama wa Chadema hadi mashabiki hawajui waende na nani.

Wapo wanaosema pembeni, wapo walioamuaa kukaa kimya kwa hofu ya kuwekwa kwenye kundi mojawapo.

Ukweli kwa niliobahatika kukutana nao, wapo upande wa Lissu. Wanasubiri lolote litokee waingilie humo. Kwa sasa hakuna tena kuaminiana ndani ya chadema, mgawanyiko ni mkubwa.

Mbowe soma alama za nyakati, wanachadema na viongozi wao wengi wapo upande wa Lissu japo hadharani wanaonekana bado wapo na wewe.

Lakini Mimi niwaonye kuwa mara 100 ya mbowe kuliko Lissu. Kuna siku mtamkumbuka mbowe.
 
Ushauri huo mzuri ungepeleka CCM ungesaidia kuondoa makundi ndani ya chama chako.

Ile kauli ya WAZURI hawafi, ilituudhi sana sisi makada.
 
Chadema wanagombea vinyesi sasa huyo lissu na mbowe kuwagombea si upumbavu uliotukuka .....sasa chadema inakwenda kufa kifo cha pili ambacho kitskuwa kifo cha ndani dalili ya kifo ilionekana wazi kwa mbowe mwanza
 
Huo mpambano wa Mbowe vs Lissu utapiganwa kwenye ukumbi gani, na lini, ili niwahi kukata tiketi?

Lissu kesho anakuja, hamna jinsi tena, ni kukubali tu ili mjiandae kisaikolojia kwa muda huu mfupi uliobakia.
 
Huo mpambano wa Mbowe vs Lissu utapiganwa kwenye ukumbi gani, na lini, ili niwahi kukata tiketi?

Lissu kesho anakuja, hamna jinsi tena, ni kukubali tu ili mjiandae kisaikolojia kwa muda huu mfupi uliobakia.
Ujio wa Lissu ni pigo kubwa kwao. Hawajui kulia wala kushoto kwao ni wapi.

Walipo wanarukia kila jambo.

Ushauri wa bure kwao, wakipenda tukutane kesho JKNIA.

Kwa hakika wajiandae kisaikolojia kwani si muda mrefu umebaki, watajua kuwa hawajui.
 
Back
Top Bottom