Mbowe unapata wapi hoja ya kuwaita Mkapa na JK majipu na kuwaacha Sumaye na Lowassa?

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,188
1,576
Leo nimesoma gazeti la Tanzania Daima Likinukuu kauli ya Mhe. Mbowe jana Bukoba akiwaita Mkapa, Kikwete na Sefue kuwa ni majipu watumbuliwe.

Mimi nikajiuliza, kwa mtanzania mwenye akili timamu unawezaje kuwaita majipu hao bila kuwataja

1. Sumaye,
2. Lowassa.

Na kukumbusha kauli yako ya "Over dead body kipindi cha Mr Richmond. Leo umeanza kugeuza kauli jitathimini siasa za namna hii hazina tija.

Ungekuwa unakerwa na majipu hawa wote ungewataja kwenye list moja!
 
Mkuu tatizo la mwenyekiti wa cdm ana kisukari cha kupoteza kumbukumbu kwani husahau anayoyaongea. Pia hajijui kuwa yeye mwenyewe ni jipu? Kuuza chama sio jipu? Ajitathmini kwanza yeye.
 
Mbona Magufuli alisema wazi kuwa waliosababisha nchi kuwa katika hali mbaya ni mkapa na kikwete hivi unaelewa kauli yake anaposema kwamba kwa utajiri wa nchi hii haiwezekani wanafunzi kukaa chini wala wagonjwa kulala kitanda kimoja watu watano.

ILA Ni kutokana na watu wachache na hao Mkapa na Kikwete ndio waliokuwa wanaongoza hiyo serikali ya hao watu wachache anaowasema Magufuli kwahiyo hao ndio majipu yaliyoiva.

Hivi ni Lowassa na Sumaye waliokuwa wamezima mita pale bandarini au Kikwete? Maana ndiye aliyekuwa rais kwa miaka yote hiyo mita ikiwa imezimwa.
 
hayo majipu aliyotaja mbowe yalikuwa yanatoa amri kwa hao lowasa na sumaye sema kingine
 
Lumumba acheni kulalama! Jibuni hoja. Hivi kama ni kweli JK na Mr. Clean ni majipu hawatakiwi kutajwa? Hayo ya EL na Sumaye yatajeni nyie.
 
Mbowe ni jipu namba moja Chadema, kule hakuna wa kulitumbua, isipokua kumpa nyimbo za kumsifu tu, ni aibu sana kua mwenyekiti wa chama kwa zaidi ya miaka kumi halafu unaona ni sawa tu, na kuwaona wenzako hawafai wakati wewe unakalia katiba na kuikandamiza. Atoe kwanza boriti ndani ya jicho lake kabla ya kibanzi kwenye jicho la jirani yake.
 
Sio wajibu wa Mbowe kuwataja wote, hizi kauli zenu kukubaliana na Mbowe kuwa hao no majipu ila mbataka kusema mbona "sio peke yao?"
Atumbue basi ndio tujue seriousness yake katika jambo hili. Sio mwindaji anayejisifu kuwa hodari kumbe anawinda digidigi ila akimuona nyati anakula kona
 
Mkuu tatizo la mwenyekiti wa cdm ana kisukari cha kupoteza kumbukumbu kwani husahau anayoyaongea. Pia hajijui kuwa yeye mwenyewe ni jipu? Kuuza chama sio jipu? Ajitathmini kwanza yeye.
Afadhali kuu za chama kuliko viongozi wenu walio amua kuuza rasilimali za watanzania,kuiba fedha za escrow, epa,meremeta,kagoda,mgodi wa kiwira
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom