Uchaguzi 2020 Mbowe umetia aibu. Jiuzulu, umeporwa jimbo kizembe

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Amani iwe kwenu wajumbe!

Tunaposema upinzani katika nchi hii bado sana ieleweke kwamba bado mbichi kweli kweli hata uwezo wa kuendesha nchi bado.

Mbowe kama kiongozi Mkuu wa kambi Rasmi ya upinzani na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha upinzani ulitakiwa kukataa hila za wazi wazi za Bwana mdogo Sabaya kukupora ushindi kwa namna yeyote ile. Hukuwapanga wananchi wako vizuri kukataa upuuzi wa aina yeyote ile, ni bora mngegawana kesi kuliko kuporwa uchaguzi.

Ulitakiwa uwe mkali na jeuri pamoja na mbabe. Naamini njia zote za wizi ulikua unazijua ulitakiwa kuzizuia kila mahali. Kama kweli DC na timu yake ndio walikua wanahujumu uchaguzi basi ungeionyesha dunia kua hutaki Upumbavu hata kama ni kwenda jela. Wewe mtu anakuja kwako usiku usiku na watu wasiojielewa anabeba walinzi wako unalia lia,kwanini usingemalizana naye usiku huo huo?

Kule south Afrika na power yako ashinde Malema kwenye jimbo lake halafu upore ushindi wake uone, nenda pale Mombasa ashinde Hassan Joho halafu upore ushindi wake uone kitakachotokea.

Mbowe wewe ni business man huna uchungu wowote na maisha ya wananchi acha kupigia watu kelele. Ninyi watu wa fursa siyo wanasiasa.Kwa hali iliyotokea kabla ya matokeo kutoka mlitakiwa kuwa jela wote kwa kuukataa Upumbavu.

Eti mpo mtaani mnalia lia mnataka kuitisha maandamano? Muitishe maandamano wakati tayari mmeshashindwa na washindi wametangazwa ni ujinga. Mlitakiwa mzuie ushindi huo wa Magumashi kwa namna yoyote ile.

Endeleeni kulia lia CCM iwe inawapangia majimbo ya kushinda. Isipoamua kuwapa jimbo hata moja hapati kweli. Huu ni udhaifu mkubwa sana kwetu, hamna uchungu wowote na raia wote watu fursa tu.
 
. wakamatwe na polisi,NEC iwaonee,kura feki ziingizwe kwenye uchaguzi bado mnamlaumu na kutaka ajiuzulu.
Hapana sio fair kabisa.
MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.
Hawa wazee hawahitaji lawama za aina zozote .WAMEPAMBANA Ila mtesi wao ana nguvu
Screenshot_20201105-192407.jpg
 
Kushinda na kutangazwa ni vitu viwili tofauti. Huyu DC wala msimpe ujiko, hakuna alichofanya kumkwamisha Mbowe. Ilishapangwa nani atangazwe.
Sio ilishapangwa MBOWE ilikua lazima asitoboe! Wananchi wa HAI walishamchoka ,hamna chochote alochofanya! Ye mwenyewe analijua hilo!.Angalia hata gape la kura alizoachwa 87k kwa 22k wapi na wapi! Huyo kashindwa kihalali kabisa!
 
Huu ujinga unaleta hasira watu bado tuna mazito mnaleta mzaha.
 
Kama ww mleta mada upo Lindi, SAWA, una haki ya kulaumu..
Ila Kama upo Dar au kwingine ambako ushindi wa wananchi uliporwa wazi wazi na hukufanya chochote, usilaumu.

Kazi ya kuhakikisha hujuma, wizi na dhulma havifanyiki haiwezi kuwa ya viongozi pekee, bali ya wananchi wote
 
Mtu kaja na bunduki anawatoa kibabe mawakala kwa kuwanyooshea bunduki kwa msaada wa polisi, then wanaingiza masanduku ya kura toka gari zenye plate namba za un ili kuwaadaa watu wajue ni waangalizi wa kimataifa kumbe ni majambazi yamekuja iba kura. Rejea kauli ya ocd wa Hai ni mpango uliandaliwa mapema.
 
Huwezi pambana na mtu mwenye bunduki wakati huna bunduki, labda tu Kama wananchi wangepewa bunduki ili kupambana na wezi wa kura.
 
Mbowe ameanza kuzomewa jimboni Hai tangu mwaka 2018 baada ya kushindwa kupeleka maendeleo na badala yake akajikita kula raha na Joyce Mkuya.
 
You have written so accurately that I am very surprised that Mbowe was robbed of his constituency and a child very much in politics, that is, he has absolutely no influence on opposition politics.
 
Back
Top Bottom