Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Wakuu, M/kiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe amesema, Chama chake hakitamuogopa kiongozi ye yote atakayekiuka taratibu za Chama, na amepongeza mahakama ya Arusha kwa uamuzi wake dhidi ya madiwani waliofukuzwa, Tz daima limeripoti Leo. Mbowe alisema Chadema haimwonei mtu lakini haiko tayari kuwa na viongozi wasiofuata taratibu, sheria na kanuni za Chama. Alisema hafurahii kutimuliwa kwa viongozi, lakini Chadema haina nafasi kwa viongozi wasiowatumikia watu. Wakati huo huo waziri wa Tamisemi Gorge Mkuchika alipoulizwa kuhusu maoni yake amesema, hana maoni kuhusu hukumu hiyo. My take.Kwa Mwendo na msimamo huu wa Mbowe na Dr Slaa Chadema inaweza kuingia ikulu ktk wakati usiotarajiwa.