Mbowe sio yule tuliyemzoea

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,071
15,895
Najaribu kumwangalia mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Aikael Mbowe si yule mMowe tuliomzoea, Mbowe amepoteza kujiamini, inaonyesha kuna kitu kikubwa kinasumbua na kitu hicho si kingine ni ile ahadi ya Mbowe CHADEMA kushika dola,

Mbowe amekua muoga kiasi ana wasiwasi kwa wafuasi wake wanataka kujua ni faida gani waliopata mpaka sasa kwa ujio wa Lowassa kiasi kwamba hata kama Lowassa asingejiunga mafanikio hayo wangeyapata tu.

Ujio wa Nyalandu bado nafsi inamsuta, Mbowe hailezi kwanini chini ya uongozi wake chama kimedumaa japo kimepata pesa nyingi lakini hazisaidii chama,
chama kimepata majina ya mafisadi maarufu lakini bado umaarufu wao hausaidii chama.

Mbowe leo hii amebaki na sababu isiyo na mashiko ya Rais Magufuli ni dikteta, mpaka leo hii Mbowe ameshatoa matamko kama mia ya kuishutumu serikali lakini Mbowe huyu hajaguswa wala kukamatwa.

Dikteta gani anaweza kukuacha tu, kuitwa polisi ukaenda kuhojiwa na kutoka huko si kukamatwa, anawadanganya wafuasi watiifu wadai haki, haki gani asiyo kuwa nayo Mbowe gari ya serikali alikwenda nayo mpaka nairobi kwa shughuli za chama na binafsi lakini serikali kimya.

Nafikiri imetosha serikali imuonyeshe mpera mpera wa siku moja tu ili ajue kama yupo huru, kuku wa kizungu hata ukimuacha huru atajihisi ayupo huru, punda haendi bila viboko.

Kampeni za nini ilihali madiwani washanunuliwa na CCM
 
11f00db41ee32026b9b3265e7a1201db.jpg
 
Najaribu kumwangalia mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema freeman aikael mbowe si yule mbowe tuliomzoea,
mbowe amepoteza kujiamini,inaonyesha kuna kitu kikubwa kinasumbua na kitu hicho si kingine ni ile ahadi ya mbowe chadema kushika dola,

mbowe amekua muoga kiasi ana wasiwasi kwa wafuasi wake wanataka kujua ni faida gani waliopata mpaka sasa kwa ujio wa lowassa kiasi kwamba hata kama lowassa asingejiunga mafanikio hayo wangeyapata tu.

ujio wa nyalandu bado nafsi inamsuta,mbowe hailezi kwanini chini ya uongozi wake chama kimedumaa japo kimepata pesa nyingi lakini hazisaidii chama,
chama kimepata majina ya mafisadi maarufu lakini bado umaarufu wao hausaidii chama,

Mbowe leo hii amebaki na sababu isiyo na mashiko ya magufuli ni dikteta,mpaka leo hii mbowe ameshatoa matamko kama mia ya kuishutumu serikali lakini mbowe huyu hajaguswa wala kukamatwa.

Dikteta gani anaweza kukuacha tu,kuitwa polisi ukaenda kuhojiwa na kutoka huko si kukamatwa,anawadanganya wafuasi watiifu wadai haki,
haki gani asiyo kuwa nayo mbowe gari ya serikali alikwenda nayo mpaka nairobi kwa shughuli za chama na binafsi lakini serikali kimya,

Nafkiri imetosha serikali imuonyeshe mpera mpera wa siku moja tu ili ajue kama yupo huru,
Kuku wa kizungu hata ukimuacha huru atajihisi ayupo huru,punda haendi bila viboko!

Kampeni za nini ili hali madiwani washanunuliwa na ccm,
Mku Mimi ni mwanaccm nisiyepepesa macho juu ya ukweli tusilishane Nyama ya Kasa mwenye sumu. Mbowe ndio mwenyekiti bora Tanzania na hilo halipingiki ndo maana yaliandaliwa majaribio mengi juu yake mwisho tuliuona pale Msajili aliyekuwa anasimamia hilo jaribio alikosa mvuto baada ya kususwa na Chadema ikabidi JK amwondoe ktk nafasi ile.
Mbowe ni mwanasiasa mahiri asiyeyumbishwa na siasa ambazo aliyevaa hawezi kuzishiriki kwani ni faida ya muda mfupi kwa wachache walioko nyuma ya hili zoezi la kutugawa
 
Sema nashangaa kwanini kamanda siro anawaruhusu hawa wahuni kufanya kampeni za kihuni kutukana serikali badala ya kujenga hoja za maendeleo, kwa nini wasichambue sera zao? Mbona CCM tunajinadi kwa sera wao kwa nini utasikia eti serikali inatuminya uhuru?? Mbona ndani ya hilo li chama mfu lake mbowe mtu akisema Mbowe dikiteta anafukuzwa uanachama
 
Kila mmoja anajinasibu kuwa ccm sasa umemsaidia nini mwenyekiti bora kuchukua nchi!
 
Hivi kumbe hata Sunday transaction za CCM-Lumumba zinafanyika? Hongera sana Polepole, ama kwa hakika upele umepata mkunaji.
 
Mbowe anayesemwa kapooza na ni muoga na hawa mavuvuzela jana aliuwasha moto akifungua kampeni Saranga.
 
Sema nashangaa kwanini kamanda siro anawaruhusu hawa wahuni kufanya kampeni za kihuni kutukana serikali badala ya kujenga hoja za maendeleo, kwa nini wasichambue sera zao? Mbona CCM tunajinadi kwa sera wao kwa nini utasikia eti serikali inatuminya uhuru?? Mbona ndani ya hilo li chama mfu lake mbowe mtu akisema Mbowe dikiteta anafukuzwa uanachama
Anajaribu kukipiga chama vanish kiukweli kilishajifia kitambo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom