Mbowe shikilia hapo hapo, CHADEMA can't be for dogs!

Hakuna kama Chadema, niwashangaa sama kama Chadema wangempa mtu kama Sumaye, Hana tofauti na Lowasa.
Chadema hata akija Magufuli kugombea uenyekiti hapati hadi tumpime jee anatosha?
Ila kwa tabia aliyo nayo yakutokusema ukweli mambo mengi basi haina haja hata kumpima. Uamuzi ni HAFAI
 
Certainly. You know damn well that “Smart opposition players” have already started shifting to the winning side.
Mkuu Driter, kiukweli nimekupenda haswa katika kuambiana kitu kinachwoitwa the bitter reality, it's very bitter to swallow but is is the reality you will have to swallow regardless unapenda au hupendi, unakubaliana na hali hiyo au hukubaliani, kama hicho ndicho kilichopangwa kitokee, ndicho kitakachotokea hiyo 2020.

Hao smart opposition players unaowazungumzia na mimi ndio nimewazungumzia katika bandiko hili

P
 
Wanaotaka Mbowe atoke Ni Wafadhili wa Chadema wa ndani na nje.Mbowe akirudi madarakani chadema itakuwa moja ya vyama maskini kuliko Chama chochote.

Matajiri na Wenye fedha wa ndani na nje wanaiaga rasmi chadema.Wana chadema mchague mawili Mbowe abaki au Wafadhili wenu waondoke
Kwahiyo wapigaji kelele na shinikizo lá ccm ni upinzani? Angalia mada zote zinazoanzishwa humu ili mbowe atoke ni nani?

Mbowe shikilia hapohapo mpk hawa wajinga wanyamaze. Rais wako alishasema atahakikisha anauwa upinzani. Kwanini pilipili usioila inakuwasha?
 
Mkuu Ruhi, kama unaamisha upinzani wa ndani ya mioyo ya watu, then its true, upinzani hauishi, ila upinzani ninaouzungumza mimi ni upinzani rasmi wa kisiasa, tayari serikali za mitaa ni CCM, mwakani madiwani wote ni CCM, wabunge wote ni CCM, then Chadema will be reduced to nothing.

P
Kwakuchaguliwa ni wananchi au kwamatakwa yenu ya kisiasa?
 
Jukumu LA kwanza la kiongozi was chama cha siasa ni kufikisha chama toka A mpaka B kwenye nchi ya asali na maziwa haraka iwezekanavyo ili sababu za kuanzishwa kwake zitimie. Hapa kwetu kila miaka 5 vyama vyote vya siasa vinapata fursa ya kuingia kwenye nchi ya ahadi na ni jukumu la kiongozi kuwafikisha wanachama wote huko. Akishindwa wenzake wanaweza wakampa nafasi nyingine kama alikaribia lakini kama alikuwa mbali sana kiongozi mstaarabu huachia ngazi mwanachama mwingine ajaribu maana lengo lao ni moja. Baada ya kupewa nafasi nyingine na akafanya vibaya zaidi kuliko fursa iliyopita, atolewe kwa kurihusu wanachama wengine wachukue nafasi yake ya uongozi kwa njia ya kidemokrasia. Kuna njia na namna nyingi za kufika B.
Eeenh, umejipinda kweli kweli, na ukadhani umetoa bonge la hoja.

Hizo 'fursa' zinazopatikana kila miaka mitano unazoziandika hapa, wewe unazijua?

Huoni wala husikii kutokuwepo kwa 'fursa' kwa vyama vingine vyote mbali ya CCM?

Wewe unaishi pango gani la giza kusikokuwa na mwanga!
 
Baada ya kupitia misukosuko yoote ambayo alishatupiwa akiwa kiongozi wa chama, na kwa uvumilivu mkubwa kaihimili; na huku akijua wazi kwamba huko mbele tuendako hali haitabadilika kuwa nzuri kwa chama chake, na badala yake itakuwa ngumu zaidi; na bado akaamua hawezi kutelekeza chama ajinusuru hali yake binafsi.

Huyo ni kiongozi shujaa. Viongozi wa aina hiyo hawapatikani kirahisi rahisi.

Wakati huu ndio ulikuwa wakati mwafaka kabisa wa Mbowe kujinasua; huku akisingizia awaachie nafasi wengine, na huku akijua hao wengine ni madalali ambao wapo tayari kukiuza chama..

Mh. Mbowe, umejitambulisha kuwa kiongozi mwenyekusimamia unachokiamini bila ya kujali maslahi yako binafsi. Heko kwako. Historia itaandikwa.
 
Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alipoona nguvu ya Mrema ilivokuwa na ombwe lililokuwepo ktk uongozi wa nchi!Aliamua kusimama kidete kunusuru nchi.(sio CCM) na kumpigis Kampeni ya nguvu BWM na hatmaye akawa Rais.

Mwalimu alitumia msemo wa Kingereza tafsiri siwezi kukaa Butiama na kuiacha nchi MIKONONI mwa mbwa(going to dogs)Kila mtu alitafsiri kivyake,wengine walisema alitukana!

Leo hii tunasikia kelele nyingi,kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa amekaa Sana ,awaachie na wengine!
Aidha anavunja katiba.

Kinadharia inaweza kuwa kweli!
Lakini katika mazingira ya Siasa za kihunii zilizoendeshwa kwa Miaka 4 sasa Ni ngumu sana Kuwaamini Hawa wema walijiotokeza kuitakia mema CHADEMA kwa kimtaka Mbowe apumzike!

Haya NI machozi ya mamba! Mbowe Shikilia hapohapo huwezi kuwaachia Chama Mbwa!
Yeah, nakumbuka siku ya Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi 2015 Rais Mstaafu Mkapa alisema, "...wanaosema nchi hii hakuna kitu chochote cha maendeleo kimefanyika tangu uhuru ni WAJINGA na WAPUMBAVU..."! Kauli hii ilinifariji sana.
 
Wanaotaka Mbowe atoke Ni Wafadhili wa Chadema wa ndani na nje.Mbowe akirudi madarakani chadema itakuwa moja ya vyama maskini kuliko Chama chochote.

Matajiri na Wenye fedha wa ndani na nje wanaiaga rasmi chadema.Wana chadema mchague mawili Mbowe abaki au Wafadhili wenu waondoke
Chama kina wanachama wenye pesa, hata wakijitoa hao unaowafikilia haitakuwa na madhara kitajiendesha kwa michango yetu sisi wanachama.
 
Mkuu Driter, kiukweli nimekupenda haswa katika kuambiana kitu kinachwoitwa the bitter reality, it's very bitter to swallow but is is the reality you will have to swallow regardless unapenda au hupendi, unakubaliana na hali hiyo au hukubaliani, kama hicho ndicho kilichopangwa kitokee, ndicho kitakachotokea hiyo 2020.

Hao smart opposition players unaowazungumzia na mimi ndio nimewazungumzia katika bandiko hili

P
Sio smart ni opportunist na selfish ni watu bao wako tayari kuuza nchi Kwa sababu ya ubinafsi wao

Ndo maana Kwa afrika almost kila MTU ana dau lake ndo maana biashara ya utumwa ilifanikiwa sana afrika Kwa sababu ya ubinafsi wa waafrika walikua tayari kuuza wenzao

Na ujiulize nyerere au Mandela wangeamua kuunga juhudi mkono Kwa wakoloni je tungepata Uhuru kweli, Mandela alipoteza kila kitu Kwa kuamini kile anachokiamini
 
I'm afraid to say, the time to save Chadema is too little too short!, baada ya matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2020, Chadema will be reduced to almost nothing!.
P

Not only Chadema but all opposition paries in the country will be liquidated in the same way that ccm has. And we will get paradise right here on earth! But one thing I can bet my last coin on is that some people will one day regret all this.
 
Mkuu Ruhi, kama unaamisha upinzani wa ndani ya mioyo ya watu, then its true, upinzani hauishi, ila upinzani ninaouzungumza mimi ni upinzani rasmi wa kisiasa, tayari serikali za mitaa ni CCM, mwakani madiwani wote ni CCM, wabunge wote ni CCM, then Chadema will be reduced to nothing.

P

Hata hiyo ccm nayo hakitakuwepo kama chama cha siasa. Kuna mtu aliwahi kusema kuwa utawala wetu wa sasa hautaki chama chochote cha siasa; including ccm itself! Je, ccm wako tayari kupoteza chama chao chenye historia iliyotukuka kwa gharama ya hushika dola pasipo kushindana? Tusubiri tuone. Lakini kwa wenye macho ya kutazama sawa sawa there is a lot to be said on the timing and contents za kile kitabu tulichokizindua hivi majuzi.
 
I'm afraid to say, the time to save Chadema is too little too short!, baada ya matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2020, Chadema will be reduced to almost nothing!.
P
Ndoto za alnacha hizo,labda Kama CCM ingekuwa ile ya Nyerere ,kidogo ya Mkapa ambapo kulikuwa na bongo ...lakini kwa Sasa ,Hawa watu wanaofikiria kutumia MOYO,...NEVER!
Matumizi ya nguvu Yana muda tu...na hupelekea kutotenda na hakika ...Haki Huinua Taifa,na kinyume chake....!
DAIMA MBELE.
 
Mkuu Ruhi, kama unaamisha upinzani wa ndani ya mioyo ya watu, then its true, upinzani hauishi, ila upinzani ninaouzungumza mimi ni upinzani rasmi wa kisiasa, tayari serikali za mitaa ni CCM, mwakani madiwani wote ni CCM, wabunge wote ni CCM, then Chadema will be reduced to nothing.

P
Matokeo ya ukandakizaji huu utaiua CCM....Mungu akupe maisha marefu ushuhudie unabii huu!
 
Cecil Mwambe, kwli utoke CCM leo uje CDM kesho, upewe Chama? hapana! NEVER! Sahau kabisa. Ulitoka CCM kwa vile ulinyimwa kugombea ubunge baada ya kupita kura za maoni. Hukuja CDM kwa vile unaipenda CDM! Hicho klichokuudhi CCM wakikiondoa utauza chama na kurudi ulikotoka! Nakushauri, rudi CCM
 
Back
Top Bottom