Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Habari wana jamiiforums,
Ni muda umepita, nilikuwa member humu ikiwa JamboForums na baadae Jamiiforums nakumbuka mwanzoni mwaka 2006 tulimpokea Ndg.Freeman A.Mbowe tulileta mijadala kuntu kuleta fikra mpya japo watu walijadili bila kuweka itikadi za vyama,ilikuwa ni mawazo ya kizalendo tu.
Niliondoka JF baada ya mlipuko wa vijana wa kundi liitwalo mtandao wa CCM ambao ni kama walimwagwa vijana humu JF kuhakikisha wanamtukana yeyote anayetowa hoja zenye mashiko kwa maendeleo ya nchi na mwenye kukemea nyendo za vigogo/mafisadi hao kutwaa ikulu kwa gharama yoyote.
Leo nimelazimika kuandika kuonyesha ni jinsi gani CHADEMA, CUF na UKAWA wamenasa kwenye nyavu za CCM na kufifisha harakati zao kisiasa, japo kuna ongezeko la uwakilishi bungeni na udiwani lazima nikiri tu katika sayansi ya siasa ni sawa na kupanda mbegu kwenye miiba, mmea utaota japo hautakuwa.
Lazima tukiri kwamba CCM inaimarika kuliko tulivyofikiria; kuanzia oganaizesheni, uongozi, wanachama,uibuaji wa kizazi kipya cha uongozi, nk. waliweza kwa mafanikio kuusambaratisha mtandao uliyoitafuna kwa miaka zaidi ya 20 kutaka madaraka. Inawezekana kwa kujuwa, kutokujua au tamaa ya pesa CHADEMA bila ya ajizi wakauchukuwa kama ulivyo na kuukabidhi chama kwa nia ya kushinda uraisi, 2015 kutokana na uzoefu na pesa za hili kundi. Madhara ya ujio huu ni makubwa kwa chadema na yanajitokeza;
Mosi; Ajizi nyumba ya njaa; kuondoka kwa Dr.Slaa na Prof Lipumba CHADEMA na CUF kwa kutokubali maamuzi ya kubadili gia angani imeleta madhara makubwa kwa vyama hivyo ki-oganaizesheni ni kama kumkata mbuzi miguu ya mbele. Mbowe anaendeleza makosa kwa kutumia gazeti lake kumchafua Dr.Slaa na familia yake ambaye kimsingi hafanyi siasa kwa sasa hivyo tabia hii haiongezi umaarufu wa CHADEMA bali inamnyima Mbowe na Chadema fursa ya mahusiano ya kibinadamu na Dr.Slaa (Akiba ya maneno), akumbuke madhila anayopitia Kubenea ambaye kwa mwaka mzima amemtukana Zitto ila uwezo wake finyu bungeni umemfundissha kwamba siasa sio ukanjanja, wiki 2 bungeni zimemtosha kuwa na akili kidogo na kuacha hekaya zake za uongo na chuki.Ni ngumu kupata mbadala anayeaminika.
Pili; EL ni kinyago kilichochongwa na CCM kwa hivyo hawezi kuwatisha wanajuwa kila mbinu zake, CCM wamefanikiwa kumkamua sumu yote na atawatumikia hana jinsi. Ameshaota mizizi ndani ya CHADEMA kiasi cha yeye kuhusishwa na ushindi wa madiwani na wabunge wote Ukawa, na hii mbinu aliitumia ndani ya CCM kuaminisha kwamba mkutano mzima ni ‘’watu wake’’.Vijana wake wametamalaki itakuwa shida kwa CHADEMA kupata wagombea ubunge na udIwani 2020 pale ambapo vijana wake watakapotaka kugombea huku CHADEMA wakiwaona sio wenzao, ikumbukwe tu kwamba ni vijana aliowatengenezea ukwasi na ushawishi hivyo kutachimbika na hii inaiweka CHADEMA katika hatari ya usaliti mkubwa ndani ya chama kwa miaka mingi ijayo kuliko kipindi kingine (Team Lowassa v CHADEMA).Tukumbuke EL na timu yake ni wakubwa kuliko CHADEMA na wamepewa utukufu kwamba bila yeye CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wasingeshinda ubunge na udiwani, ikiwamo Tanzania bara na Zanzibar (rejea Magazeti ya desemba 2015; Lowassa awapa UKAWA wabunge 116, halmashauri nk), hataguswa na ataachiwa aamuwe nani anamtaka agombee wapi, kwani katika nafasi alizopewa kuteuwa viti maalum aliteuwa marafiki zake waliokuwa CCM, ofisi yake mikocheni ndio yenye maamuzi sio ufipa pale hapana hadhi yake.
Tatu; CCM wamefanikiwa kugeuza taswira na ni kama inawaeleza wananchi ambao ni wapiga kura kwamba kwa kuondoka kwa EL na gene lake kimepumua na sasa mzigo umehamia CHADEMA na kwa kweli hili wamefanikiwa ndio maana wakikosoa yeyote hujibiwa ‘’mbona CHADEMA mlimchukuwa EL kaeni kimya mafisadi nyinyi’’ nk. CCM imejivua gamba (mtandao) uliyowatesa na wanaonekana kuitumia hii fursa vyema ili kujenga taswira mpya huku CHADEMA wakitowa maelezo na utetezi (dodoki) ambao haueleweki vema, CCM kutumia fimbo hiyo kuwachapa, Kwa hali yoyote ile kataa kubali EL, Sumaye na wengine ni mradi mpya wa CCM upinzani kwa akili za kawaida itachukuchuwa miaka 20 kutambua kosa hili kama ilivyokuwa Mrema baada ya kushindwa uraisi mwaka 1995.Kibaya zaidi Maalim Seif kukubali EL awe bosi wake nayyeye maamuzi anafanyia Mikocheni bila kufahamu anatekeleza mipango isiyo ya CUF.
Nne; CHADEMA inafanya makosa makubwa kujaribu kupinga mabadiliko yanayofanywa na Raisi Dr.Magufuli, ambayo kwa pamoja na Kina Freeman Mbowe tuliyaongelea, kama kubana matumizi, safari za nje, utegemezi wa nje mbaya zaidi nimemsikia Mbowe akilalamikia viongozi na wafanayakazi wa Umma wanaowajibishwa kwa kuleta hasara bandarini, Nida, TRA, mahakama ya mafisadi, nk akisema ‘’wanaonewa’’ eti Raisi ‘’hafuati sheria ’’, EL analalamika ‘’marafiki zake’’ kutozwa kodi (japo yeye siwezi kumshangaa) kundi kutamani serikali ifanye makosa ili wapate cha kukosoa (siasa za fisi) kama ambavyo viongozi wa juu wanavyofanya. Badala ya kuboresha hoja chadema kimekuwa ni chama kinachopiga makelele.
Mwisho; Propaganda zisizo na mantiki kama ‘’kushitaki ICC & ICJ’’, ‘’TB Joshua kaja na ujumbe mzito’’!, ‘’Mkapa kafariki’’!,’’tumeibiwa kura’’ ambazo ni sawa na kujidanganya kwamba ‘’usiku hautakwisha”. Kinachoudhi zaidi ni Chadema kuacha kwenda kuishitaki serikali kwa wananchi na sasa wanakimbilia kwenye western media na mabalozi hizi ni dalili kwamba hoja zao haziaminiwi na wananchi. Kwangu mimi Dr.Slaa ni rasilimali muhimu tuliyotupa kwani hata angeshindwa uraisi bado angekuwa na uhalali wa hoja dhidi ya serikali. Mbowe kala matapishi yake na EL kamuumbua kwa kumbandika bei yake (price tag) mwaka 2013 alijitapa kwenye hana bei kipindi wanagombana na Zitto ni Kama namwona JK anamkejeli Mbowe ‘’Dogo mbowe bei yako ni chee mno!’ unakumbuka ulichosema mwaka, 2013? kwamba hauna bei, sasa vipi? Ni muda muafaka kwa Mbowe na Maalim kutafakari upya mustakabali wao kisiasa!
Nakaribisha hoja na si viroja