Kama unafuatilia vizuri vyama vya upinzani vimepig hatua zaidi kuliko mfumo wa vyama vingi ulioanza. Sasa hivi watanzania wengi, siyo wote lakini idadi inayoongezeka wanajua kuwa upo uwezekana wa kuishinda CCM. Kama unafuatilia idadi ya kura, na wabunge wa vyama vya upinzani imekuwa ikiongezeka uchaguzi hadi uchaguzi kuanzia 1995 uchaguzi w vyama vingi ulipofanyika kwa mara ya kwanza. Kura kwa vyama vya upinzani zimepatikana pia vijijini kuliko hapo mwanzo zilikuwa zikipatikana mijini tu. Makosa ya viongonzi wa vyama vya upinzani pia yanachangia kushindwa kukabiliana na mbinu za chama kizoefu cha migogoro kwa miaka mingi. Dhana ya viongozi kumiliki chama na kujipa mamlaka ya kuwaengua wasiowataka inawafanya wanachama waone chama si chao bali nicha baadhi ya viongozi. Kuweka imani katika nguvu ya mtu mmoja badala ya chama, mfano kumuengua Dr. Slaa kwa gharama ya kumpata Lowasa kunathibitisha hoja hii. Kuamini kuwa pesa inaweza kuwezesha kupata uongozi.
Unafikiri Lipumba na Slaa wangekuwepo ingebadilisha kitu? Kuishinda CCM ni zaidi ya kinachotokea kwenye masanduku ya kura (CCM is an experienced electoral machine. Huwashindi tu eti kwa kuwa kura zao hazijatosha. Tizama kinachotokea Zanzibar, kama unataka ushahidi).
Watanzania wengi bado ni waoga wa kuiadhibu CCM. Hawajiamini. They are ignorant of their own power - power of their votes. Wanafikiri uchaguzi ni kwa ajili ya viongozi na si kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao. Wanapiga kura kama kutoa zawadi kwa wagombea wanaowataka badala ya kupiga kura kwa mustakabali wa maisha yao. Kwamba nimeamua kumchagua flani na yeye akafaidi.
Wanadanganyika kirahisi. Hawahoji mambo. Maneno matupu wanaridhika. Ukabila. Kwamba mchague flani bana "ni wa nyumbani".
By design, uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki. Tume ya Uchaguzi na vyombo vyote vya dola + wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, DEDs, wakuu wa taasisi za umma - wote hawa hufanya kazi kuhakikisha kuwa maslahi ya CCM yanalindwa na upinzani unadidimizwa. CCM ikiwa na shaka na taasisi yoyote ile, basi hufanya mabadiliko ya uongozi katika taasisi hiyo hata siku chache kabla ya kura kupigwa. Usiposhiriki kikamilifu kufanikisha kampeni/mikakati ya CCM unatolewa kwenye nafasi uliyopo.
In short, "the spirit of let's have a fair war is not deep enough" - bila kujali ni Slaa, au Lipumba, au Lowassa, au Hashimu Rungwe anayegombea urais kwa tiketi ya kambi ya upinzani.