Mkuu Mbowe huna sababu ya kususia matokeo ya uchaguzi, kulikuwa na kila sababu kwa nyinyi kushindwa na miongoni mwa sababu kuu ni hizi hapa:-
1.Taswira ya team ya kampeni (team ya kanda vs taifa stars)
hakuna anayeweza kubisha kuwa sura ya team ya kampeni ya ukawa ilikuwa haina taswira ya kitaifa.
watu wa kaskazini waliongoza team kwa kiasi kikubwa na kufanya watu wa maeneo mengine wasijione kufit ndani ya ukawa. team iliongozwa na Mbatia, Mbowe, Sumaye, Lowasa na Mrema. Team hii haikutoa support kabisa kwa Mgombea mwenza na kumfanya Mnyaa wa cuf kumpa support jambo ambalo nalo linaweza kuwa swali kwa wadadisi wa mambo. Lakini tujiulize ukawa haikuwa na hazina nyingine kabisa katika uundaji wake wa team ya kampeni.
Kwa upande wa ccm ilikuwa wazi unaiona Tanzania kwa kiwango cha kujihisi kufit zaidi huko kuliko kwa vyama vingine. Unamuona Mwigulu, Kinana, Makamba, Kikwete, Magufuli, Msukuma, Mkapa, Mwinyi, Warioba etc, hii ilikuwa team ya taifa kwelikweli.
2. Afya ya Mgombea wa ukawa
Wakati wa kampeni hali ya kiafya ya Mh. Lowasa ilikuwa tete kiasi cha kufanya iwe ni news sehemu nyingi za kampeni. Slogan ya hapa kazi tu na push up zilitawala na kuzijengea umaarufu kampeni za ccm. lakini hali ya afya ya mgombea wa ukawa ilimfanya Lowasa ashindwe kupambana mwenyewe jukwaani na kushindwa kujitetea kabisa. Kimsingi Lowasa alikuwa mgombea mwenye sifa nyingi nzuri za kiuongozi. Mfano, Taaluma yake ya digrii ya uzamili ni juu ya maendeleo na sera zake pia zilikuwa zinaeleweka lakini hakuwa na nafasi kutawala jukwaa kutokana na afya yake kuwa na mgogoro.
3. kujiengua kwa Lipumba na Slaa
Hawa walikuwa ni mwiba sana kwa ccm, nadhani itabidi baada ya matokeo ya mwisho tujumlishe alama alizopata Slaa na Lipumba na tuone kwa umoja wao walifanikiwa kwa kiasi gani? Lakini kukosekana kwa Lipumba kumevuruga sana kura za cuf ndio maana maeneo ambayo cuf imeshinda Lowasa hakupata kura nyingi sana kama maeneo ambayo CDM walikuwa wakishinda.
4. UKAWA kushindwa kufikia muafaka
kwa kiasi kikubwa ukawa walikuwa wanapambana wenyewe kwa wenyewe ktk baadhi ya sehemu. kwa hili mbowe ana lawama kwa kiasi fulani maana yeye ndiye engineer mkuu wa umoja huu hasa hatua hii ya pili ya kuungana kwa ajili ya uchaguzi. Kuna baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa na utata na yeye alishindwa kutoa uamuzi na kuacha mgogoro ukue. kigoma, dar na kusini zilitokea kesi na chadema walipuuzia kwa kiwango kikubwa. hii ilileta ugomvi kwa kiasi kikubwa na kusababisha mfarakano ambao haukuwa wa lazima. Mbowe alikuwa na nafasi ya kuwakemea wanachadema waliokuwa hawaheshimu makubaliano na pia Maalim na Mtatiro na mbatia walishindwa kuwajibika kwa nafasi zao na hivyo kuwa-cost kwa kushindwa kutumia vema fursa hii ya muungano wao.
5. uwekezaji mbovu kwa vijana
Lowasa na ukawa waliinvest mno kwa vijana hasa wale wafanya biashara wachuuzi na vijana wa boda boda. kuna kila dalili uwekezaji huu umemgharimu sana maana kama utakumbuka siku ya uchaguzi kulikuwa hakuna usafiri kwa masaa mengi hasa ya asubuhi na kwa jinsi hiyo vijana walikuwa wanakimbiza nyomi la abiria na kusahau kuwa walikuwa na ahadi na mgombea. lakini wakati wa uandikishwaji vijana walikuwa wanajiandikisha sana makazini kwao ila kwa bahati mbaya watu wengi hawakupata fursa ya kwenda mbali na kwao na kwa hali ya usalama ilivyokuwa vijana hawakuthubutu kwenda mbali na kurisk usalama wao.
ilipaswa lowasa awasome aina ya vijana waliokuwa wanadeal nao, kinyume chake ccm iliinvest kwa vijana wenye nafuu na fursa hasa za elimu na nafasi kama wasanii na baadhi ya vikundi vya vijana. hawa huwa wanajua thamani za kura zao na walijitahidi kuhakikisha kuwa wanapiga kura.
Yapaswa wakajipange upya kuliko kuendelea kukataa kwa tatizo waliloliunda wenyewe.