Mbowe: Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja

Mhe Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja cha utawala wake kutokana na kuendesha nchi kibabe bila kufuata sheria, uonevu, upendeleo na hali ngumu ya maisha inayawakabili wananchi tofauti na kipindi kilichopita.

Mbowe ametoa kauli hiyo wakati akizindua tawi jipya la Chadema katika kijiji cha Mpakani Kata ya Kwakifua Wilaya ya Muheza mkoani Tanga leo Jumamosi.

Freeman Mbowe
M/kiti Chadema-Taifa.
Muheza leo
25.03.2017
View attachment 486862

FREEMAN Aikaeli Mbowe, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema atajiuzulu kufanya siasa iwapo Rais John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, anaandika Charles William.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa Chadema wilayani Muheza Tanga ambapo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa chama.

“Huyu atakuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu. Na kama Magufuli akishinda tena uchaguzi mwaka 2020 mimi nitajiuzulu siasa,” amesema Mbowe.

Kiongozi huyo aliorodhesha madudu kadhaa ya utawala wa awamu ya tano ikiwemo upendeleo wa kugawa madaraka na kulinda waovu wasio na sifa ya kuwa viongozi akitolea mfano wa Paul Makonda mwenye tuhuma mbaya ya kufoji vyeti vya elimu na mtu aliyeongoza uhalifu wa kuvamia kituo cha Habari cha Clouds.

Pia Mbowe aliutuhumu utawala wa sasa wa kunyanyasa wananchi na kuonyesha ubabe huku ukiminya uhuru wa vyombo vya habari na ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya nchi.

Amesisitiza kuwa chama chake tayari kimeanza kujiandaa na uchaguzi wa 2020 kwani kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Mbowe yupo ziarani mkoani Tanga, akifungua matawi ya chama hicho na kukagua uhai wa chama.

Ameambatana pia na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).
Mbowe ndiye mwanasiasa pekee ambaye bado anafanya siasa miongoni mwa waasisi wa mwanzo kabisa wa Chadema.
Wengi wamekufa na wengine ni wazee kiasi cha kutoweza kumudu mikimiki ya siasa za majukwaani.

Hii ni ahadi ya pili ya Mbowe kujiuzulu siasa.
Mara ya kwanza, mwaka 2014 aliahidi kujiuzulu siasa mwaka 2015 iwapo chama chake kingepata idadi ndogo ya kura za Urais na wabunge kuliko kilichopata mwaka 2010.

Hata hivyo Chadema kiliongeza Wabunge kutoka 49 mpaka 71 huku kura za urais zikipanda kutoka asilimia 26 kwa mwaka 2010 mpaka asilimia 40 kwa mwaka 2015.

Angejiihuzuru sasa angeisaidia Chadema, Mbowe hana sifa ya uongozi jengo la wananchi kulitumia bila kodi hafai kabisa, wapinzani wamehalibiwa Jin a na watu kama Mbowe. Watanzania hatuna choice wrala pa kukimbilia, kila kona kuna mtoto
 
Mbowe kweli Kanjanja.....afu wafuasi wake ndo wale wanyama wetu pendwa wa Serengeti.

Sio mjanja ni mudanganyifu na ni mtu mwenye tamaa, anaweza kuiuza nchi kwa bei rahisi na watu wake. Hafai hafai. Is better the devil you know,
 
Akishindwa Magufuli raisi mwingine awe nani?

Hivi Jecha kastaafu?

Thinking like the fish out of water!!
 
Mbowe uchaguzi wa 2015 alisema chadema isingeshinda angejiuzuru siasa saiv karudia tena maneno hayo hayo.
 
Sio mjanja ni mudanganyifu na ni mtu mwenye tamaa, anaweza kuiuza nchi kwa bei rahisi na watu wake. Hafai hafai. Is better the devil you know,
Nimesema Mbowe ni Kanjanja sio mjanja,above all nakuunga mkono maoni yako.
The guy is devil himself
 
....hata Kama JPM anamapungufu bado ni rais bora

Nakubaliana na wewe. Rais Magufuli ametupa hope kubwa sana baada ya utawala mbovu wa miaka mingi. Kitu kimenisikitisha, sio Mimi tu ninwatu wengi waliokuwa wakimutegemea kuleta mabadiliko, ni kumulinda mutu kama Makonda. Yeye anaamini Makonda anachukiwa kwaajili ya kupigana na madawa, hiyo sio kweli, kwani Rais Magufuli kaisha teuwa mtu wa shuguli hiyo, na wala humsikii mtu akimshambulia. Kila muzazi anaunga mkono hili swala la madawa, na tunashukuru sana Rais kuteuwa mtu wa wakulishughulikia. Tatizo ni vile HUYU Mkuu wa Mkowa anavyoyatumia madaraka yake, anamchonganisha Rais Magufuli na watu aliyowapa hope na waliompa kula. Inaonekana anabaguwa ikifika kwenye utendaji wa sheria. Upungufu mwingine sio kitu, lakini huu wa Makonda ni upungufu sio tu unamvunjia heshima na kumuchonganisha hapa nyumbani, hata nchi za nje. Hakuna muwekezaji ambaye anaamini the rule of law atawekeza kwenye nchi AMBAYO Mkuu wa Mkowa anatumia polisi kuvunja sheria. UCHUNGU ni kwamba Watanzania hatuna pa kukimbilia, hope yetu ni HUYU Rais, Sasa akianza kuwachukulia watu hatuwa ya kuwafukuza kazi kwa kusema ukweli, haswa wa HUYU Makonda tunaanza kuwa na Shaka. Namuunga mkono kwa kesi ya mchanga wetu unaopakiwa kwenye macontainer. Kwani huu sio muchanga wa kawaida, na mambo mengi anayoyafanya mazuri.
 
Mhe Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja cha utawala wake kutokana na kuendesha nchi kibabe bila kufuata sheria, uonevu, upendeleo na hali ngumu ya maisha inayawakabili wananchi tofauti na kipindi kilichopita.

Mbowe ametoa kauli hiyo wakati akizindua tawi jipya la Chadema katika kijiji cha Mpakani Kata ya Kwakifua Wilaya ya Muheza mkoani Tanga leo Jumamosi.

Freeman Mbowe
M/kiti Chadema-Taifa.
Muheza leo
25.03.2017
View attachment 486862

FREEMAN Aikaeli Mbowe, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema atajiuzulu kufanya siasa iwapo Rais John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, anaandika Charles William.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa Chadema wilayani Muheza Tanga ambapo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa chama.

“Huyu atakuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu. Na kama Magufuli akishinda tena uchaguzi mwaka 2020 mimi nitajiuzulu siasa,” amesema Mbowe.

Kiongozi huyo aliorodhesha madudu kadhaa ya utawala wa awamu ya tano ikiwemo upendeleo wa kugawa madaraka na kulinda waovu wasio na sifa ya kuwa viongozi akitolea mfano wa Paul Makonda mwenye tuhuma mbaya ya kufoji vyeti vya elimu na mtu aliyeongoza uhalifu wa kuvamia kituo cha Habari cha Clouds.

Pia Mbowe aliutuhumu utawala wa sasa wa kunyanyasa wananchi na kuonyesha ubabe huku ukiminya uhuru wa vyombo vya habari na ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya nchi.

Amesisitiza kuwa chama chake tayari kimeanza kujiandaa na uchaguzi wa 2020 kwani kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Mbowe yupo ziarani mkoani Tanga, akifungua matawi ya chama hicho na kukagua uhai wa chama.

Ameambatana pia na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).
Mbowe ndiye mwanasiasa pekee ambaye bado anafanya siasa miongoni mwa waasisi wa mwanzo kabisa wa Chadema.
Wengi wamekufa na wengine ni wazee kiasi cha kutoweza kumudu mikimiki ya siasa za majukwaani.

Hii ni ahadi ya pili ya Mbowe kujiuzulu siasa.
Mara ya kwanza, mwaka 2014 aliahidi kujiuzulu siasa mwaka 2015 iwapo chama chake kingepata idadi ndogo ya kura za Urais na wabunge kuliko kilichopata mwaka 2010.

Hata hivyo Chadema kiliongeza Wabunge kutoka 49 mpaka 71 huku kura za urais zikipanda kutoka asilimia 26 kwa mwaka 2010 mpaka asilimia 40 kwa mwaka 2015.
ok tuone kama kweli atakaa kipindi kimoja. walipokua wanagawana hela kwa viroba waliona ndio hela ziko mtaani kumbe wananchi walio wengi wana hali ngumu. sasa wamebanwa kwa kua vyombo vyote vya habari wanamilikii wao mapepari uchwara ndio wanasema jpm kipindi kimoja. ngoja tutaona.
 
Kwa nijuavyo mimi, basi atakua ndio rahisi pekee tangu Nyerere kuweza kufanikisha makubwa ndani ya kipindi kimoja. Na pia kwani ni lazima rais akae vipindi 2? Swala ni ndani ya kipindi hicho kimoja kafanya nini!!!
 
Kuna watu kwenye hili jukwaa mpo kimya sana...Kama mnafikiri mna freedom ya kukaa kimya, Be careful, nasema watch it, not to that extent.
 
Back
Top Bottom