Mbowe: Rais Magufuli ndiye rais wa pekee Tanzania atakaekaa madarakani kwa kipindi kimoja

FREEMAN Aikaeli Mbowe, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema atajiuzulu kufanya siasa iwapo Rais John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, anaandika Charles William.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa Chadema wilayani Muheza Tanga ambapo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa chama.

“Huyu atakuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu. Na kama Magufuli akishinda tena uchaguzi mwaka 2020 mimi nitajiuzulu siasa,” amesema Mbowe.

Kiongozi huyo aliorodhesha madudu kadhaa ya utawala wa awamu ya tano ikiwemo upendeleo wa kugawa madaraka na kulinda waovu wasio na sifa ya kuwa viongozi akitolea mfano wa Paul Makonda mwenye tuhuma mbaya ya kufoji vyeti vya elimu na mtu aliyeongoza uhalifu wa kuvamia kituo cha Habari cha Clouds.

Pia Mbowe aliutuhumu utawala wa sasa wa kunyanyasa wananchi na kuonyesha ubabe huku ukiminya uhuru wa vyombo vya habari na ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya nchi.

Amesisitiza kuwa chama chake tayari kimeanza kujiandaa na uchaguzi wa 2020 kwani kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Mbowe yupo ziarani mkoani Tanga, akifungua matawi ya chama hicho na kukagua uhai wa chama.

Ameambatana pia na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).
Mbowe ndiye mwanasiasa pekee ambaye bado anafanya siasa miongoni mwa waasisi wa mwanzo kabisa wa Chadema.
Wengi wamekufa na wengine ni wazee kiasi cha kutoweza kumudu mikimiki ya siasa za majukwaani.

Hii ni ahadi ya pili ya Mbowe kujiuzulu siasa.
Mara ya kwanza, mwaka 2014 aliahidi kujiuzulu siasa mwaka 2015 iwapo chama chake kingepata idadi ndogo ya kura za Urais na wabunge kuliko kilichopata mwaka 2010.
Hata hivyo Chadema kiliongeza Wabunge kutoka 49 mpaka 71 huku kura za urais zikipanda kutoka asilimia 26 kwa mwaka 2010 mpaka asilimia 40 kwa mwaka 2015.
Kwani uchaguzi kwenye chama chake lini??
 
Huyo Mbowe alitakiwa awe ameshajiuzulu siasa angalau miaka mitatu iliyopita.

Watu wanakomaa na Makonda kwa sababu media ya bongo karibu yote ni mali ya wauza dona.

Lakini Mbowe kwa kashfa zote zilizokwisha mkumba alitakiwa sasa hivi awe ameshaanza kusahaulika kwenye siasa za bongo.

Anaishi kisiasa katika muda wa kukopa (borrowed time) na Mzee Mtei alishamwambia ajipime kwa kujitazama mwenyewe baada ya ile kashfa ya kuitwa pale central police.
 
Kashfa zakupangia hapo store za Lumumba
 
Ajiuzuru tu maana hata yeye nae amekaa mda mrefu mno na kabinya democracy kwenye chama chake. Hana tena jipya..kawatimua vijana wote walio kuwa wanataka kujikakamua.
 
Huyo Mbowe alitakiwa awe ameshajiuzulu siasa angalau miaka mitatu iliyopita.

Watu wanakomaa na Makonda kwa sababu media ya bongo karibu yote ni mali ya wauza dona.

Lakini Mbowe kwa kashfa zote zilizokwisha mkumba alitakiwa sasa hivi awe ameshaanza kusahaulika kwenye siasa za bongo.

Anaishi kisiasa katika muda wa kukopa (borrowed time) na Mzee Mtei alishamwambia ajipime kwa kujitazama mwenyewe baada ya ile kashfa ya kuitwa pale central police.
kuna Kauli ukizisikia zinakera hasa zinapotoka kwa mtu anayedhaniwa kuwa sane mind.

unasema media karibu zote n za wauza dona.....na hapohapo mnajidai mna serikali makini

mliruhusu vipi media zinazomilikiwa na wauza dona?
kwanini had Sasa ilihali mkijua hamjawahifadhi jela???
 
Mkuu ndio maana ya mapambano mazito yanayoendelea duniani kote. Na wala usidanganyike ukadhani kwamba wauza dona wanatesa hapa bongo tu. Hii ni biashara isiyolipiwa kodi, biashara yenye super profit.

Serikali ipo makini ndio maana hata wale jamaa kutoka Ulaya na Asia waliweza kudakwa kipindi kile kuelekea uchaguzi mkuu. Wakihesabu kura kana kwamba wao ni waajiriwa wa tume ya uchaguzi.

Mkuu wewe ni mtu mzima kiumri sio mtoto mdogo wa sekondari au yule wa mwaka wa kwanza chuo kikuu. Zama kwenye tafakuri nzito utaelewa mantiki ya mapambano kuelekezwa kwa Makonda mara tu baada ya wauza dona kuanza kushughulikiwa kikamilifu.
 
blabla tu...hujibu maswali unaleta porojo
 
blabla tu...hujibu maswali unaleta porojo
Mkuu utamjuaje muuza dona kwa kumuangalia usoni au kwa kukaa nae kwenye vikao ofisini?.

Kumbuka kuwa mhubiri injili wa leo ndio muuza dona wa kesho. Hii ni vita nzito zaidi ya ambavyo media zetu zinajaribu sana kupotosha lengo kuu la mapambano.
 
Huyu sizonje kwa mambo anayotufanyia watanzania hapaswi hata kufika 2020, ifanywe namna huyu Mzee atuachie Nchi yetu haraka iwezekanavyo. Na achunguzwe asili yake, wasukuma hawana tabia kama zake. Hata huku koromije tumemkana huyu Sizonje!!! Wazee wenzake hawaamini kama huyu nae ni Ngosha mwenzetu, wanasema atakuwa na asili ya Rwanda au Burundi.
 
Ukweli mtupu , kwanza hata hiyo mitano ashukuru Mungu sana , uhakika ni kwamba atang'olewa bungeni .
 
Je amejiuliza hicho kipindi kimoja kitaisha baada ya miaka mingapi? "Wazalendo" wanaweza kumuongezea muda usio na kikomo ili aendelee kuinyoosha nchi
 
"Tanga mmeendelea kuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu mmeendelea kukikumbatia Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwapigia kura na kuwafanya wawatawale kwa muda mrefu bila kuwaletea maendeleo, nimesikiliza risala hapa mnahitaji Shule, umeme, maji salama, zahanati n.k vitu ambavyo mikoa inayoongozwa na Upinzani wamesahau, kama ni shule labda wanataka kujenga shule ya nne au zaidi" hayo yamesemwa leo Jumamosi 25/03/2017 na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Freeman Mbowe akiwa katika ziara mkoani Tanga ambapo amezindua ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Muheza na kuzindua msingi wa Chama katika kijiji Mpakani Kata ya Kwa Kifua Muheza Tanga.

Hii ni muendelezo wa ziara katika Kanda zote 8 nchini, Ziara hii imeshapita katika Kanda ya Nyasa, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Pwani na sasa ni Kanda ya Kaskazini ambayo inajumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Dhumuni la ziara hii ni kuwashukuru wananchi/ wapenzi/ wakereketwa wa CHADEMA, kuangalia uhai wa Chama mara baada ya uchaguzi Mkuu Oktoba 2015, kuongea na viongozi katika ngazi kupitia mikutano ya ndani, kuvuna wanachama wapya, kuzungumzia na kuleta Ujumbe wa Chama kuhusu hali ya siasa, uchumi nchini pamoja na kukijenga Chama n.k .

CHADEMA ina utaratibu wakuwashukuru wananchi kila baada ya Uchaguzi unapomalizika, kwa niaba ya mgombea Urais Mhe. Lowassa, Mhe. Mbowe amewashukuru sana wananchi wa Muheza.

Jitahdi sana kuwa unaumiza kichwa chako kwa kujisomea....kuna kitu kinaitwa cost sharing kati ya wananchi na serikali....ifike muda tujitambue hayo yasingewezekana ikiwa watu kama akina Lowassa na sumaye wameshindwa yafanya miaka yote wakiwa serikali ya ccm na wanataka kuyafanya wakiwa chadema tena kwa Mwaka mmoja tu.
 
Nina maana mumeo Mbowe.

Mbona naona CCM ndio amewanyoosha vizuri. Tena kashajihakikishia hakuna wa kumzuia 2020 na kakata vichwa NEC. Kama uamini anagalia video ya uapishwaji wa mwakyembe na waziri mpya wa sheria. Watu wote wamekuwa wapolee, hawana raha na waonga. bashite pekeyake ndio alikuwa anatikisa kichwa mtakatifu akiongea
 
Back
Top Bottom