Mbowe: Nitajiuzulu siasa tusipochukua jimbo la Masasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe: Nitajiuzulu siasa tusipochukua jimbo la Masasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 5, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema moto uliowashwa na chama hicho katika Operesheni Sangara utaendelea nchi nzima, lengo likiwa ni kuiondoa CCM madarakani na iwapo itasalimika mwaka 2015, atajiuzulu siasa.

  Mbowe alitoa kauli hiyo juzi alipohutubia mamia ya wakazi wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakati chama hicho kilipofanya mkutano mkubwa kwenye uwanja wa mpira wilayani humo.

  Alisema CCM kimepoteza mwelekeo wa kuongoza taifa na ndiyo sababu maisha ya Watanzania yamezidi kuwa mgumu kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.

  "Wajibu wa Serikali kokote duniani ni moja tu, kuwezesha watu wake kutoka katika hali ngumu za maisha na kuwapeleka kwenye heri, leo CCM wameligawa Taifa katika vipande, wanauza rasilimali za nchi na kuwadidimiza watu wa kipato cha chini wengi wao wakiwa ni wakulima," alisema Mbowe na kuongeza:

  "Ndugu zangu ngojeni niwaulize swali, wakati wa utawala wa Mwinyi na Mkapa (marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa), ni kipindi gani maisha yalikuwa mazuri?" Wananchi wakajibu (kipindi cha Mwinyi). Miaka 10 ya uongozi wa Mkapa na miaka saba ya Kikwete, ni kipindi gani maisha yamekuwa magumu zaidi?" Wakajibu (Kikwete); Je, 2015 wanakuja tena kutuomba kura huyo atakayekuja si ndiyo itakuwa mbaya zaidi, Chadema hatuwezi kukubali na moto huu tuliowasha utaendelea nchi nzima hadi Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kama CCM itasalimika nitajiuzulu siasa."

  Mbowe alikishambulia CCM akidai kimepoteza mwelekeo uliowekwa na waasisi wake, chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuzingatia usawa, udugu huku kikijikita katika msingi wa kutetea wakulima wanyonge na wafanyakazi lakini sasa kimewagawa wananchi katika matabaka ya walio nacho na wasio nacho.

  "CCM ya Mwalimu Nyerere ilijali wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini, ilijenga mshikamano baina ya Watanzania wote bila kujali ukabila. Tanzania ina makabila zaidi ya 120, lakini tunaishi kama mtu na ndugu yake, leo taifa limegawanyika vipande huku maadili ya uongozi yakiporomoka," alisema Mbowe.

  Katika mkutano huo uliokutanisha viongozi wote wa kitaifa wa chama hicho, Mbowe alisema kwa sasa CCM kimevuruga hata mitalaa ya elimu huku akituhumu watunga sera kuwa wanafanya hivyo makusudi kwa kuwa watoto wao hawasomi katika shule hizo.

  "Mwalimu alijenga CCM iliyozingatia usawa, watoto wote walisoma shule moja, mimi nilisoma na watoto wa Mwalimu Nyerere, mawaziri na wakulima katika shule hiyo, leo watoto wa mkulima wanasoma shule za kata ambazo hazina walimu, vitabu, maabara wala library (maktaba), wakati watoto wa vigogo wakisoma nchi nje na wale wa wakuu wa wilaya wakisoma shule za (academy)," alisema Mbowe.

  Aliwataka wakazi wa mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara kuunganisha nguvu kwa lengo la kukiondoa CCM madarakani katika chaguzi zote ukiwamo mkuu wa 2015.

  "Ndugu zangu wa Masasi, mimi Mbowe ninatimiza miaka 21 nikiongoza siasa za upinzani zenye lengo la kuleta ukombozi wa kweli kwa Taifa hili, nimefunguliwa kesi za uchochezi tisa hadi leo, lakini sitaacha harakati hata wakinifunga, bado nitaendelea na harakati za ukombozi hadi Watanzania watakapofikia kwenye uhuru wa kweli," alisema Mbowe.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alieleza kusikitishwa kwake na umaskini unaoukabili Mkoa wa Mtwara licha ya kuwapo rasilimali nyingi zinazouzunguka ikiwamo gesi na korosho.

  Alisema kumekuwa na ufisadi mkubwa unaofanywa katika ununuzi wa korosho na licha ya wananchi kukatwa Sh30 katika kila kilo wanayouza, bado mikoa hiyo ya kusini inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji, huduma muhimu za kijamii kama zahanati na shule.

  "Taifa linaweza kuendelea ikiwa rasilimali za nchi ambazo zinatoka kwa wananchi zitawarudia na kutumika katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Leo mnakatwa Sh30 katika kila kilo moja ya korosho mnayouza, tumetafuta ni kiasi gani cha korosho kimepatikana kwa mwaka hapa nchini lakini taarifa hizo hatuzipati."

  "Lakini taarifa tulizopata Ulaya zinasema Tanzania imeuza tani 157,000 kwenye soko la dunia, haya mabilioni ya fedha mnazokatwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika wapi?" alihoji na kuongeza kuwa fedha hizo zinastahili kudaiwa.

  Source:
  Mwananchi

  My concern

  Huu msimamo naungojea kwa hamu kuuona kama utafanikiwa na kutimia
   
 2. Tangopori

  Tangopori JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 1,614
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  Ni maneno ya kamanda mbowe baada ya kuona hamasa ya watu wanaotaka mabadiliko huko masasi.
   
 3. h

  hans79 JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Usisubiri njaa itoke bali zuia njaa isitoke, kauli ya mkiti ni namna ya kujenga maendeleo sehemu ambazo hazina mbunge anayewajibika kwa wapiga kura wake. Juhudi ziwe namna ya kumpata kijana alosoma wa maeneo hayo agome ubunge 2015.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sio masasi tuu tunataka mtwara nzima
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Siasa ni zaidi ya uijuavyo
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Viapo vingine ni vya kisiasa zaidi kuliko viapo vya kweli.
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kusini yote ni ya CHADEMA hilo halina ubishi hata Yule mlemavu wa ngozi jimbo lake tunachukua namuomba sana asitumie ulemavu Kama Kinga (naomba mnisamehe sina nia ya kumkosoa Mungu ila tunataka jimbo tu basi)
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Hapa kamanda nadhani ali nukuliwa vibaya, sasa kama chadema wameshinda uraisi? Mtwara wamekosa kiti kimoja tu masasi?
  Any way makamanda wetu naamini wanajua nini wanakifanya!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Pamoja sana kamanda wa anga. Vipi kuhusu majimbo ya mkoa wa Singida?
   
 10. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Cha muhimu ni ukombozi kwa wananchi kutokana na kukata tamaa na kushinda kutwa kwenye vijiwe wakivuta bangi wakidhani itawasaidia kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
   
 11. s

  slufay JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mchemkaji huyo ashakuwa kama Tom Ngawaiya 2010 wakati wa kampeni akidai kuwa CDM ikipata urais atahama Nchi ,,, Siasa gani isiyokuwa na mwelekeo wa ridhaa ya wananchi (ataiba kura au?)
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Usihofu, ni hatua kwa hatua hadi nchi nzima. Hakuna atakayeachwa na m4c. Bado nasubiri kwa hamu sana m4c ndani ya Msoga, Bagamoyo!
   
 13. S

  SEBM JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Binafsi napata shida sana kuwaelewa waandishi wa wetu na uelewa, uadilifu na weledi wao katika fani yao ya uandishi. Binafsi sijasoma hilo gazeti lakini ninapata mashaka sana katika maeneo niliyoyaainisha;

  1.Hivi ni Operesheni Sangara au M4C ambayo inaenezwa huko mikoa ya kusini?
  2.Hapa anasema mamia ya wananchi...lakini pale anasema mkutano mkubwa wa hadhara!Watu mia tano; wanaweza waka-qualify mkutano ukaitwa 'mkubwa?'.

  Naona hii inafanana na ule mkutano wa Wassira wa watu 7,000 ambao ulizidiwa kete na walevi 4 ambao walipayuka na kuzomea na kuuteka mkutano mzima kwa sauti zao.

  NGUVU YA UMMA
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mbowe punguza viapo hii thread itakuwa itakuwa kama ushahidi baada ya uchaguzi.
   
 15. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naamini Mbowe hatagombea ubunge Masasi hii ni changamoto kwa vijana wapenda mabadiliko kutoka Masasi waitumie kupata ubunge na wawaletee mabadiliko wana Masasi kama M/kiti lazima aweke hamasa ya kauli kama hizi ili makamanda waone hili linawezekana.

  Tusiishie kwenye kauli tunahitaji kwenda zaidi ya hapo.
   
 16. h

  hans79 JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Angelikuwa kama usemavyo chama kisingekuwa kama kilivyo, ushibapo ujue pana walalalo njaa kutokana mfumo mbovu wa serikali. Je wawasaidiaje hao? Tembea uone, pia jiulize kipi kilojiri hadi mkiti kusema hivyo.
   
 17. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa kufanya mkutano pale Home Masasi ni kweli jimbo letu lina mwamko mkubwa sana wa kifikra hivyo ni sahihi kusema jimbo linaweza kwenda upinzani 2015 kwa kuwa tuna historia ya kutoremba remba tumebadilisha wabunge mara kwa mara na hii inaonesha mbunge asipowajibika tunammwaga so CDM iongeze juhudi kuhamasisha ili watu wawajue na kuwakubali kisha kuwapa kura.
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  ritz Anza na Zitto Kabwe kwanza ndio alitangaza hatogombea Ubunge mwaka 2010 ili arudi kufanya kazi zake za Taaluma aliyosomea.

  Hata wachezaji mpira wapo wanaoahidi asipofunga goli mechi fulani basi atajiuzulu, hizi ni dhamira anazopaswa kuwa nazo mtu Jasiri na dume la mbegu, na hata JK alipaswa kuahidi hivi kwamba asipotimiza ahadi ya kununuwa meli mpya kama ya Mv Bukoma basi tusichaguwe tena CCM.

  All in all haya ni mambo ya kawaida na ni muhimu katika kuwapa watu hamasa kwani siasa nayo kuna wakati inahitaji burudani zake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. k

  kaeso JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeikopi na kuihifadhi kabisa....
   
 20. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Sasa litaendaje tena upinzani mkuu??mbona unakosea?upinzani ya 2015 si sisiem au?
   
Loading...