Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Anaandika Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe.
Uamuzi wa kwanza wa msingi ni Kama Mkuu wa Mkoa anayo mamla kisheria kuagiza watu wakamatwe na kuhusika moja kwa moja katika kufanya uchunguzi katika masuala yanayohusiana na dawa za kulevya? na jambo hilo limepangiwa tarehe ya kusikilizwa wiki ya kwanza yw mwezi Machi.
Jambo la pili lilikuwa ni kutaka basi hadi hapo suala la msingi litakaposikilizwa wazuie wasiweze kunikamata au kunisumbua kwa njia yeyote kunipa haki zangu za Kikatiba haki zangu za kisheria kwa sababu wanaohusika kutenda tendo hilo hawana mamlaka hayo kwa maana ya Mkuu wa Mkoa na wasaidizi wake, kwa hilo mahakama imekubaliana na mimi na imetoa zuio kwa Polisi kunisumbua kwa njia yeyote ile hadi hapo Mahakama itakapokuwa imeamua kama wana haki ama hawana haki.
Tulifungua shauri hili tokea tarehe 10/2/2017 mpaka leo ni tarehe 21/02/2017 ni siku 11 zimepita katika kipindi chote hiki Polisi wamekuwa wanazunguka sana tunamtaka Mbowe tunamtaka Mbowe, Mahakama ina uwezo wa kujipangia kalenda yake yenyewe ambayo ilipanga kusikiliza jambo hili mbali kidogo ikatoa siku 11 sasa, siku 11 pamoja kwamba tuli-file katika mazingira ya haraka (certificate of urgency) lakini kwa bahati mbaya haikufanikiwa kusikilizwa mapema kwa hiyo ikatoa nafasi ndefu sana Polisi kuendelea kunisumbua kuni-harass mimi,wafanyakazi, wanachama na viongozi wengine wa CHADEMA tunamtaka Mwenyekiti, sasa sikutaka kuonekana Kama Mwenyekiti Mbowe nakimbia shtaka, siliogopi shtaka kwa sababu ni la kutengenezeka tu, lakini nilichokuwa nakikataa ni ile kupewa amri na mtu ambae hana mamlaka kisheria kutoa amri hiyo.
Nataka nchi irejee katika misingi ya utawala wa Katiba, Sheria na taratibu, Viongozi wa Kiserikali au viongozi wenye mamlaka juu ya watu wengine wasijione wao wana haki ya kutenda mambo kinyume cha Katiba, kinyume cha taratibu hata kama jambo wanalotaka kufanya lina njia njema, lazima yapitie katika mfumo unaokubalika wa kisheria.
Hilo ni jambo la kwanza la msingi sana , hapa ni Mbowe napambana na dola na pambana na Serikali na pambana na Polisi napamba na Mkuu wa Mkoa lakini wapo Watanzania wengi tu ambao wanaonewa katika misingi kama hii na hawana ujasiri wa kupambana na Serikali kuidai haki, kwa hiyo napoidai haki hii sio naidai haki hii, sio kwamba naipigania haki mimi kama Mbowe hapana, napigania haki katika taifa, taifa liendeshwe kwa mujibu wa Katiba,Sheria na taratibu za nchi.
Hilo la kwanza lakini la pili Mimi ni Kiongozi wa watu, ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani,Kiongozi wa Upinzani Bungeni, ni Baba mwenye familia na watoto ni Mbunge wa jimbo la Hai naaminika na wananchi na mahusiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, napokuwa nasikia nimetuhumiwa kwa tuhuma za dawa ya kulevya ambazo hazina ushahidi, haina msingi ni jambo baya sana jambo baya sana ni character assassination.
Nina mipango wa kudai fidia kwa kuchafuliwa jina, hilo liko wazi nilisema toka siku ya kwanza kwa hiyo mpango huo lazima tutautekeleza.