Mbowe: Nimetoka Gerezani kwa moyo mweupe. Katiba ni ajenda yetu, Sisi sio magaidi

Ni ngumu sana,,labda vyama vyote viungane kwa pamoja, na wagombea wake watokee pwani, kanda ya magharibi na kanda ya ziwa hapo atleast. Lakinii kwa chadema tu co rahisi, kwani ninavyoona wafuasi wake wengi hutokea kaskazini tu,, Tanga sidhani kama kuna wafuasi wengi, labda wa kuokota okota.

Binafsi, mara elfu kumi ccm iendelee kutawala kuliko chadema, na mama yetu aliongoze taifa letu hata kwa miaka 30 mbele sawa tuu,, tunampenda sana, ni mtu wa watu.
halafu unaiogopa katiba mpya. Uzuzu Ni ugonjwa aisee
 
Tayari ashatengeneza mazingira ya kuwahadaa watu.

Jamaa kaishavimbishwa mfuko na bimkubwa ili aje atulie na kuwahadaa hadaa ndondocha wake hadi 2025.

Sasa hivi tutasikia jamaa karuka mala moja Dubai kutumia alichokusanya kwa bimkubwa ili kupunguza mawazo.
halafu kumbuka huyo Mbowe sio maskini kama alivyo baba yako
 
Upumbavu at it's best, na fedha hii kutoka kwa bimkubwa ni kodi yako wewe ambaye huioni inatumika vibaya,

Mr.Mbowe ametoka kwenye upper class family, fedha sio issue kabisa, ni uzalendo wake ndio maana yupo frontline, mimi na wewe ni keyboards kings!tunalalama na hizi fake id
Ana hela gani mbona anauuza magari mabovu Chadema
 

MBOWE ANAZUNGUMZA MAAZIMIO YA CHADEMA, ASEMA ALICHOZUNGUMZA NA RAIS SAMIA​



Sehemu ya nukuu za Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 18, 2022:

"Leo nazungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza baada ya miezi saba na nusu ya kuwa kifungoni. Waandishi mbalimbali walinitafuta kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi wakitaka mwenyekiti nitoe kauli ya mambo kadha wa kadha yanayojiri katika nchi yetu lakini nilichelea kufanya hivyo

"Nilitambua kiu na shauku ta Watanzania wengi wakitaka kusikia kauli ya Mbowe, kimsingi kauli ya Mbowe ni kauli ya chama, hivyo isingekuwa sahihi kama kauli ya Mbowe ingetoka bila ya Mbowe kukaa na chama chake…

"Chini ya mbingu kila jambo lina wakati wake, kuna wakati wa kukusanya na kuna wakati wa kutawanya, na mengine mnaweza kusoma katika biblia kwenye kitabu cha Muhubiri mlango wa 3.

"Hakika nimeushuhudia upendo na sijui kwamba nitaulipa kwa njia gani, na nimekuwa nikilizungumza hili kila nikipata nafasi, siku zangu na walinzi wangu tukiwa gerezani, dunia ulisimama upande wetu kwa mithili na mifano ambayo siwezi kuielezea.

"Nimekuwa gerezani kwa muda mrefu na nimejifunza mengi sana, nataka kuwahakikishia Watanzania na dunia kuwa sikupoteza zile siku.”

"Nimesema na ninasema kuwa, natangaza msamaha kwa yeyote yule nafikiri aliyenitendea baya, sina chuki wala kisasi na nawaomba Wanachadema wenzangu tusiwe na chuki na yeyote katika mapambano ya kutafuta uhuru na Ustawi wa watu.

"Baada ya kutoka gerezani nililetewa salamu za mheshimiwa Rais kwamba angependa kukutana na mimi mapema iwezekanavyo. Mtakumbuka kwa muda mrefu sisi kama chama tulitaka kuzungumza na Rais tukiamini kwamba ana majibu ama ana ufunguzi wa mambo mengi yanayolisibu taifa letu.

"Mbowe aliyeingia gerezani ndiyo Mbowe aliyetoka gerezani, tena pengine akiwa imara zaidi. Kwa hiyo nimezungumza na Rais mambo kadhaa. Lakini sikuyafikisha kwa umma kwa sababu nilihitaji kwanza kuzungumza na Kamati Kuu ya Chama changu na viongozi wenzangu.

"Nilipokwenda gerezani, chama hiki hakikuenda gerezani. Viongozi wenzangu walikuwepo, vikao vya chama vilifanyika, mashauriano mbalimbali yalitokea. Ninaporejea kutoka gerezani ninapaswa kwanza kukabidhiwa kiti changu ndo nizungumze kama msemaji mkuu wa chama.

"Kwa hiyo nawashukuru viongozi wenzangu walikilinda chama chetu katika mazingira magumu sana. Kwa hiyo ilinipasa mimi kwanza nizungumze na kamati kuu ya chama changu ili nitakapotoa kauli kwa umma nitoe kauli ya chama na sio kauli ya Mbowe.

"Waheshimiwa viongozi, nilipokwenda kukutana na mheshimiwa Rais Ikulu, tulichokizungumza ni kitu kimoja tu cha msingi. Kwamba tulikubaliana kutafuta njia za haki, za mazungumzo, za mashauriano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa letu."

"Na tulikubaliana kwamba tuna tatizo moja kubwa la kutokuaminiana kwa sababu tumekuwa na urafiki wa mashaka. Tumekua na urafiki wa mashaka na hakika tuna urafiki wa mashaka, hatuaminiani.

"Tukakubaliana, ili kuvuka kikwazo hicho, lazima kila upande ujaribu kujenga kwa mwenzake, na majibu yatapatikana kwa wakati, sio jambo au tukio la siku moja. Hilo lilikua la kwanza la msingi.

"Tulikubaliana na Rais Samia Suluhu tuache kuzungumza neno amani amani kila wakati, na badala yake tuzungumze haki, tutaunganishwa kama taifa kama pale viongozi na watawala wataitanguliza haki katika kila hatua ya maisha yetu.

"Haki haitawali, zinatawala sheria na katiba, haki ni makusanyiko wa vitu vingi ambavyo vinawekewa utaratibu katika nchi ikiwemo katiba. Kama wote mtazamo wetu ni kuitanguliza haki ya makundi yote, CHADEMA tuko tayari kuzungumza na yeyote. Hilo tulizungumza na Rais."

"Nilimfahamisha Rais Samia kuwa apende yeye au apende yeyote mwingine, CHADEMA ndiyo chama kikuu cha upinzani, hauwezi kufanikisha mchakato wowote wa kisiasa kwa kukiacha nje chama kikuu cha upinzani.”

"Nafasi ya CHADEMA katika siasa na kuwa chama kikuu cha upinzani hatukujitakia bali imejengwa kwa imani na wananchi, tupo kila kanda, mkoa, jimbo, wilaya, kata, mtaa, kijiji na kitongoji na hilo limetokea kwa kuwa watu wamefanya kazi.

"Nilimwambia Mhe. Rais Samia kuwa juhudi zozote za vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi nyingine za serikali kufikiria kwamba vinaweza kuitenga CHADEMA, havitaituliza nchi hii kwa kuwa sisi ni wadau kamili kwa kuwa tuna uhalali wa kuwawakilisha watu."

“Tarehe 21 Machi 2022 kutakuwa na kikao cha TCD (Umoja wa Vyama Vyenye Wabunge), CHADEMA tulisema hatuna Wabunge hadi hali hiyo itakapobadilika, lakini tupo kama wajumbe kwa nafasi yetu kama waanzilishi.

“Tuna taarifa kuwa kuna Kongamano limendaliwa na TCD la Machi 31 jijini Dodoma, kuna mambo kadhaa yanajadiliwa kule, sina sababu ya kuyajadili kwa kuwa kuna mambo mengi yanazungumzwa kuhusu hilo.

"Mazungumzo katika taifa letu ndiyo yawe msingi wa kutatua matatizo yetu, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na yaliyotokea tuligundua kuwa kiini cha tatizo ni Katiba na Tume ya Uchaguzi. Kama chama tukachakua ajenda hizi tukiamini pia ndizo ajenda za wananchi.

"CHADEMA na katiba hakuna namna tutatenganishwa nayo kuna maneno eti ooh Mbowe amekwenda Ikulu hivyo ajenda ya katiba haitakuwepo, nani kasema maneno hayo? Katiba ndiyo ajenda yetu kuu na tutaipigania kokote kule, ni ajenda ya CHADEMA na itabaki kuwa hivyo.

"Tulichokubali pekee ni kutumia mazungumzo kama njia ya kupata katiba mpya, Katiba ni maridhiano katika nchi, CHADEMA pekee hatuwezi kuunda katiba, kwa kutokuwepo maridhiano mwaka 2014 upinzani tuliikosa katiba na CCM iliikosa katiba.

“Mapambano ya Katiba yatupeleke kwenye mazungumzo, ambayo nayo yakishindikana tutatafuta mbinu nyingine lakini harakati za Katiba hazitakoma. Masuala ya Tume Huru ni vingine vingi ni mazao ya katiba.

“Kongamano la TCD tumeshauriana kama chama, haya maridhiano yanayozungumzwa kupitia TCD, sisi hatukushiriki kuyaandaa na sisi hatutashiriki kongamano la TCD na hatuoni nia njema ya kupata katiba mpya kupitia TCD, siyo Mbowe wala chama kitakachoshiriki kongamano hilo.

“Tafuteni kokote ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA ameridhia, siwezi kuuza chama changu kirahisi hivyo, mimi siyo rahisi kihivyo, mimi ndiyo Mbowe. Japo nimesema tutakubali mazungumzo lakini siyo CHADEMA wala Mbowe atashiriki kongamano hilo.

“Nimekubaliana na Mhe Rais kuwa tutashiriki katika mazungumzo, na tumepanga tarehe nyingine ya kuendeleza mazungumzo, tutashauriana na vyama vingine vya siasa lakini kuhusu Katiba mtazamo na msimamo wetu uko palepale.

“Kuna vyama takribani 20 na vinatofautiana mitazamo, vyama hivyo vimepitia mapitio tofauti, siamini kama kuna chama kimepitia mateso tuliyoyapitia CHADEMA kwa miaka sita iliyopita, kuna wapiganaji wamepotea, wengine wapo magerezani, wengine wamefukuzwa kazi, sisi siyo magaidi, tumeumizwa sana.

“Maridhiano maridhiano tulikoseana wapi? Kuna wengine hata kwenye uchaguzi hawakuwepo, wala hawajashiriki, hawajajua maana ya kusingiziwa makosa, hawajui uchungu wa risasi, hawajafungwa gerezani, wanasema turidhiane.

“Vipo baadhi ya vyama vya siasa vinasema hawahitaji mikutano ya hadhara, wanasema hivyo kwa kuwa hawana wa kumhutubia, wanakaa kwenye Baraza la Vyama vya Siasa vinasema ‘Uchaguzi ulikuwa huru na haki’.

“Kwa sababu sisi tumetengwa nimemwambia Mh Rais kuwa mchakato wowote wa upatanisho lazima itanguliwe na ukweli. Hatujakaa tukaelezana uchaguzi ule ulikuwaje, tuambiene ilikuwaje kisha ndiyo tuangalie tunafanyaje.

“Tume ya Chaguzi imepeleka majina ya uwongo bungeni kisha mnataka tukae mezani turidhiane, turidhiane nini?

“Tukiona tunachokijadili sicho tulichodhamilia tutatoka na tutawaambia Watanzania tumetoka.

“Yawezekana hampo katika viatu vya viongozi wenzangu wa CHADEMA mkajua maisha tunayopitia, ubaguzi wa kihitikadi, uonevu. Nina uhakika wenzetu upande wa pili hawajui na hawajapitia tunachopitia sisi CHADEMA, wala hawana idea hali hii ipoje.

“Yaliyofanyika katika uchaguzi wa 2020 niite tu ulikuwa Uhuni uliofanywa na Tume ya Uchaguzi na vyombo vya usalama, hatua ya kusamehe inatakiwa kuambatana na hatua ya kutambua tatizo, hatuwezi kwenda mbele wakati tuna chuki.

“Hatua ya kwenda mbele inatakiwa iendane na hatua ya kutambua tatizo kisha aliyekosa aseme sorry.

“Mnatuita chama kikuu cha upinzani bungeni wakati hatua mbunge bungeni, Kanda ya Ziwa tulikuwa tunaongoza asilimia 48 vijijini leo hatuongozi hata sehemu moja…Tuayajadili haya, nali aliwajibika ndipo tuweke utaratibu, wanataka twende mbele bila kutambua walifanya makosa.

“Leo kiongozi wa upinzani anaenda kuonana na Rais inakuwa ishu kubwa, wakati hili linaoaswa kuwa jambo la kawaida.

“Kwanza tukubaliane kuwa tunahitaji Katiba Mpya. Hivi vikao na mazungumzo tulivyokubali kushiriki ndiyo vijadili tunaipataje Katiba Mpya. Wenzetu katika makongamano wanaonekana hawaipi kipaumbele Katiba Mpya wanasema ni suala la baadaye sana.

“Kuomba na Rais hatukuanza leo, nilipotoka gerezani sikuwa na kinyongo, nikutaka kuweka kiburi, naitwa na Rais wa nchi eti nikatae, hiyo ni fursa mimi kuitumia.

“Ninapoona fursa yoyote kuisaidia Chadema, kuisaidia nchi yangu nitaitumia. Rais ameonesha nia njema akaniita Ikulu, siwezi kukataa, tukakubaliana kutangaza haki na hilo tulilifanya. Wapo watakaopinga upande wa Rais na wapo watakaopinga upande wa CHADEMA.

“Siwezi kukataa kuitwa na Rais wa Nchi, naogopa nini kwenda Ikulu kwa Rais! Nimechoka kuona Wanachadema wanaonewa, wanafungwa, hiyo inatakiwa ifike mwisho.

“Mimi ni mpiganaji wa siasa, nilifanya hivyo nikiwa gerezani nilikuwa naendeleza siasa nikiwa huko, nina uhakika wafungwa wote ni Wanachadema nap engine maafande nusu.

“Tatizo la msingi la nchi yetu ni Katiba, nakiona kinachoenda kutokea Dodoma sijui ni marekebisho ya kisiasa, hatutaki Katiba ya Viraka, tunataka kubadilisha Katiba Mpya.

“Kauli za Spika Tulia Ackson kuhusu wabunge 19 ni kauli za kilaghai, wanatufanya sisi ni mazuzu, tumeshawaandikia barua na wakapokea, ndiyo hayo mambo tunasema yanaleta ufa na Baraza Kuu litakuwa 25 Aprili kama kuna rufaa zao zitasikilizwa, mengine muda utaongea.

“Msimamo wa chama umeshazungumzwa. Kuna baadhi ya magazeti yameandika kuwa Mbowe ameenda kuridhia wabunge 19, mara ishu siyo kukubali Wabunge 19, ishu ni kukataa ubatili uliofanyika.

“Nilichojifunza gerezani ni kula ugali na maharage, familia yangu ilikuwa inaletea chakula Jumamosi na Jumapili, kisha Jumatatu hadi Ijumaa napiga don ana wenzangu.

“Nimejifunza kuwa kuna uonevu mkubwa sana nchi hii, Polisi licha ya kuwa wanafanya kazi nzuri baadhi lakini wanaonea sana watu baadhi ya maeneo, watu wengi wapo magereza na hawakustahili kuwa gerezani.

“Nilikuwa nakaa na wafungwa wa kunyongwa, katika 100 basi 70 wanashinda rufaa zao, hiyo ni kwa kuwa polisi hawafuati utaratibu. Siyo kila mtu anaweza kupata upendeleo kama nilioupata mimi katika kesi yangu ya michongo, lakini kuna watu wanaonewa kwa kukosa msaada wa kisheria na kifedha.

“Nimekaa gerezani nilichoathirika zaidi ni kupotezewa muda, lakini nilikuwa naomba kesi isimalizike haraka ili tuone ushahidi wao na mliona kwa ushahidi ule eti Mbowe ana kesi ya kujibu na kama tungeanza kujitetea...nisiseme sana.

“Kauli ya CCM kuwa Jeshi la Polisi lijitathimini sisi CHADEMA tumelisema sana, tumeisema miaka na miaka, nashangaa mpaka leo IGP (Simon Sirro) bado yupo ofisini? Chama tawala kusema vile hapaswi kuwa ofisini mpaka sasa.

“Kwa kauli ile ya Kamati Kuu ya CCM, Sirro alitakiwa akiuzulu ndani ya dakika moja inayofuata.


“Kabla ya kwenda gerezani nilikuwa pale Oysterbay, mule ndani wakati nalala chini nilikuta kuna vijana zaidi ya 40, wamewekwa ndani kwa wiki tatu, hawana mwanasheria, hakuna mtetezi, wanasema ni msako wa uzururaji.

“Wakaniandikia niwasaidie, nikampa karatasi yule alileta chakula, karatasi ikakamatwa, nikahamishwa, aliyenipa hizo taarifa akahamisha na sijui alipelekwa wapi.

“Kama Duni yeye kwake anaona haiwezekani Serikali kujitokeza na kuomba radhi, basi mimi naamini inawezekana, tunachotaka ni Serikali itoke ijitokeze iseme ukweli.

“Kuhusu kauli ya Rais Samia kuhusu kanuni za mikutano ya siasa, mimi siyo Msemaji wa Rais, sijui kanuni inatoka wapi, sisi tunachotaka ni uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa tu. Hatudai kanuni, tunataka haki ya kufanya mikutano ya siasa.

“Kuhusu walinzi wangu, sisi tumewaamini, wakikengeuka hiyo itakuwa ni juu yao, hata CHADEMA kuna watu tuliowaamini wakatugeuka.

“Tulikuwa na Red Brigade wakapigwa marufuku na Mwendazake. Nilipotafuta walinzi hawa nilijuwa nitakachokutana nacho mbele, hata viongozi wangu nao wanahitaji Makomandoo, tutaacha pale tutakapokuwa na uhakika wa kutodhuliwa na watu wasiojulikana.

“Mwaka mmoja wa Mama Samia, nafikiri jambo hilo alizungumzie Shaka, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi.”

“Jumamosi nitakwenda nyumbani kwetu, Machame Hai, nikiwa kule Jumapili nitafanya ibada na wananchi wangu, walioungana na wengine kuniombea mara kwa mara, nikirudi Dar nitashiriki katika Kampeni ya Join The Chain na nitatembea mkuu kwa mguu.”

Msamaha ni Uponyaji.

Mwamba sio Gaidi
 
Ana hela gani mbona anauuza magari mabovu Chadema

Dharau zenu hizi kisa CCM zinawafanya mjione mko juu kuliko kila mtu. Wewe unamjua Mbowe leo?. Mwaka 1999 Mbowe alikuwa mmoja wa wadhamini wa shindano la miss Tanzania.
 
Yani ccm hapo wanatamani kufa , maana walisema hatazungumzia katiba mpya na amepishana na makamu wake mambo yamekuja tofauti,
walisema amepingana na makamu wake kuhusu join the chain naona napo wamefeli wanateleza tu wakitafuta pa kushika.
Ndio maana huwa hawamtaki mbowe awe mwenyekiti wa chadema kumbe wanaelewa moto wake.
na bado maji mtaita mma ngoja katiba ije mtajua hamjui nyoo
 
nawaahidi chadema hamtaishinda ccm milele ila mtaishinda kwenye tweeter na mitandaoni hapo nawasifu mnajua matusi na hasa mkiisha kunywa mbege mnafungua mitandao na kuanza kutukana tu hongreni sana nyumbu mmeshinda
 
nawaahidi chadema hamtaishinda ccm milele ila mtaishinda kwenye tweeter na mitandaoni hapo nawasifu mnajua matusi na hasa mkiisha kunywa mbege mnafungua mitandai kutukana tu hongreni
Kweli kabisa kwa matusi hawawezekani,
Kuna mmoja humu kanitukania mama yangu aliyeko kaburini kisa tu mbowe gaidi
Ajaaaabu kweli kweli,
Namuheshimu mama aliyemzaa siwezi kumtukana na pia nimemsamehe
 
Wewe unaamini uchaguzi ulikuwa huru na Haki?. Yani siku ya uchaguzi mpaka siku ya kutangaza matokeo mtandao wa internet ulifungwa kwaajili gani Kama sio wizi?.
Ni mpumbavu tu na mtu asiye na akili aneyeweza kuamini kuwa ule ulikuwa uchaguzi
 
Back
Top Bottom