#COVID19 Mbowe ni nani hadi atangaze vifo vya wagonjwa wa Corona?

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Nimekutana na video ya Freeman Mbowe mitandaoni akitangaza msiba wa kaka yake Charles Mbowe kuwa amefariki kwa ugonjwa wa Corona!

Swali Mbowe amekuwa nani wa kutangaza magonjwa ya Corona?

Agizo lilipo mpaka sasa ni kwamba ugonjwa wa Corona utaongelewa na kutangazwa na

1. Waziri mkuu
2. Rais
3. Waziri wa afya
4. Madaktari

Je, Mbowe ni nani kati ya hao?

Licha ya hivyo Mbowe haaminiki mbele ya uma wa Tanzania tokea siku ile alipoangushwa na konyagi alafu akaitangazia dunia kuwa amepigwa na wasiojulikana ili tu apate kiki kisiasa.

20210708_205429.jpg
 
Kwani ugonjwa wa corona ni siri hadi watu waogope kutangaza? Ni ugonjwa kama magonjwa mengine tu!

Ni sawa tu na mtu kaugua kichwa, pressure, kisukari, malaria, AIDS, etc, hamna cha ajabu hapo! Acheni kukuza vitu vya ajabu!!

Kwanza kuutangaza ni kuongeza awareness, watu wachukue tahadhari!

Hamna jipya! Kojoa kalale.
 
Yupo sahihi, ametoa taarifa kama mwanafamilia. Pia amepewa cheti cha kifo na Dr haina mbaya.

Hajatoa takwimu kitaifa.

Shida unachanganya ukereketwa wa siasa.

Amiri Jeshi mkuu amempa pole, wewe nani uhoji
 
Haijakatazwa popote, yeye kawasiliana na watu wake, Kama haikuhusu iache

Ila pia nimesikitika kumuona kinara wa kudai serikali itambue covid akiattend mkutano wa akina mama na hajavaa mask Wala wale wamama hawajavaa

Ni unafiq mkuu, in less than 6 months Kawa careless
 
Kama alipimwa, ikathibitika hivyo, hata wewe utasema, na ninataka tuwe wawazi na wakweli zaidi juu ya hili.

Jambo lingine la kujiuliza kwa mh Mbowe, kwamba, yeye alitangaza kuwa amechanjwa chanjo ya Corona. Je, kaka yake, kuchanjwa?

Nachotamani pia, atokee shujaa atakaye sema kuwa, hata wenye chanjo wanaambukizwa tena na wanakufa, ili baada ya hapo, Sua wafanye kazi ya ziada ili tusiwategemee wazungu peke yao
 
Back
Top Bottom