Mbowe ni mtu hatari sana, nimeanza kumuogopa

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,015
1. Ameongoza CHADEMA kwa miaka 10 kwa mafanikio makubwa, hadi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

2. Ameweza kuwaondoa wasaliti na waswahili ndani ya CHADEMA bila kuogopa chama kufa.

3. Amekuwa akisakamwa sana na pro CCM a.k.a nyumbu wa kijani kuwa anafisadi chama, mara anajikopesha pesa, mara anauza chama, hii yote ni woga tu ili wanaCHADEMA wamtoe Mbowe, CCM ipate ahueni.

4. Ni mwanasiasa hatari mwenye vision, alipobadili gia angani watu walidhani kakosea, ila japo kuna watu wanalalamika, ukweli ni kuwa, ujio wa Lowassa umeleta neema CHADEMA,

Kupata kura milioni 6 si jambo la mzaha, ukweli babu wa mihogo asingefikisha, na ukweli ni kuwa hamasa za mabadiliko wakati wa kampeni zilikuwa za moto zaidi kulipo Slaa angekuwepo.

5. Namna upinzani unavyominywa ni dhahiri inahitaji kiongozi makini kumudu hali hiyo. Lakini Mbowe ameweza.

Kwa hayo machache naamini Mbowe ni mtu hatari sana anayepaswa kuogopwa na CCM kwani wanakosa raha kwa ajili yake.
 
Watu wengi tuna kawaida ya kujisifu kwa kuangalia matokeo na kusema nimejitahidi sana, nimeweza kufika mahali ambapo sikufika mwaka jana etc.

Ifike mahali tuyaweke malengo yetu wazi, mfano tunataka kuwa na bunge 50% 50% uchaguzi wa 2020, au tunataka kushinda uchaguzi wa rais, na ikifikia tusifanikiwe iangaliwe tatizo ni nini ili kama kuna kuwajibishana ifanyike hivyo.

Ila kwa jinsi tunavyoenda utashangaa kila mwaka sisi ni chama kikuu cha upinzani na bado tutakuwa tunapongezana. Tuweke malengo, watu wawe responsible kwa malengo yaliyowekwa kabla na si kuanza kusifiana baada ya matokeo ambayo hatuna uhakika kama ndo lilikuwa lengo letu au zuga.
 
Akina Mugabe na Museveni huwa wanasifiwa hivyohivyo na wapambe wao ili kutetea muendelezo wao wa kukaa madarakani. Ili tuweze kuuona vizuri uzuri wake aachie wengine waongoze tuweze kufanya comparison, viongozi wazuri hawang'ang'anii madaraka, Mandela ni mfano.
 
Subiri baada ya 2020 ndio use me haya.

Wallah Uongozi mbovu Wa Kikwete ndio ulioibeba CDM. Watu walikata tamaa na CCM na serikali yake.
 
Mbowe Kama Nyerere ......ule uwezo wa kuondoa kiongozi na bado Hali ikabaki tulivu....mnakumbuka Aboud Jumbe

Haikuwa rahisi kuweza kumuondoa Zitto ...na Chama chao kikabaki imara ...vile vile kubwa kuliko kuandoka Slaa siku chache Kabila ya uchaguzi na bado upepo ukapita .....Ana kipaji
 
Back
Top Bottom