G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini ndugu Freeman Mbowe amemshambulia naibu Spika wa Bunge la Tanzania ndugu Tulia Ackson Mwansau kwa kumuita kuwa ni mtu mwenye kiburi, kujifanya mjuaji na mwenye kiherehere cha ziada.
Mbowe ameyasema hayo huku akitahadharisha kuwa upinzani watapambana naye kikamilifu.
"Huyu ni mtu anayeingilia majukumu yasiyomhusu, mwenye kiburi na kiherehere cha ziada" amesema Mbowe.
Aidha bado upinzani wameendelea kususia vikao anavyoviongoza na kumpuuzilia mbali pale anapoingia bungeni.
Naibu Spika huyo aliyeteuliwa kuwa mbunge na baadaye kupitishwa kuwa Naibu Spika, amekuwa mtu wa kuyumba kusiko kawaida na kudandia hoja bila uelewa pale anapoongoza shughuli za bunge.
Aidha anadaiwa kujitwalia majukumu ya kuiongoza ofisi ya Spika na kuamua mambo pasipo kufuata kanuni za bunge.