Mbowe na TANROADS, mita 30 kutoka barabara ya Machame mna maana gani?

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,680
22,685
Habari wakuu,.

Kumekuwa na sintofahamu kubwa sana kwa wakazi wa wilaya ya HAI ambayo mbunge mwenye dhamana ni Mhe Freeman mbowe.

Hususan kwa wananchi ambao wapo karibu na barabara hii ya machame.

Kabla barabara hii haijakabidhiwa Tanroads ilikuwa chini ya serikali za vijiji na halmashauri ya wilaya ya HAI, sasa baada ya Tanroads kuichukua wakaanza kuweka "X " katika majengo yaliyopo mita 22.5 kutoka katikati ya barabara hii ya machame miaka mitano iliyopita bila kuahidi fidia yoyote na wala hakuna maelezo yoyote kutoka ofisi yoyote akiwemo mbunge wa Jimbo hili la wilaya ya HAI Mhe Freeman.

Sasa leo wamekuja kuweka "X " mpya lakini wamezidisha vipimo, kutoka mita 22.5 za awali kufikia mita 30 kwa sasa bila kulipa fidia yoyote zaidi ya kuandika BOMOA.

Kinachosikitisha wananchi wengi ni kwamba barabara hii haina matumizi makubwa kiasi cha kusababishia watu wakae mita 30.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hii barabara haipanuliwi bali wanataka wananchi wakae mbali na barabara.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hata barabara za miji mikubwa wananchi hawakai mbali na barabara kwa umbali huo.

Kinachosikitisha zaidi hata mbunge mwenye dhamana Mhe Mbowe amekaa kimya juu ya sintofahamu hii waliyonayo wananchi wake.

Kinachosikitisha zaidi inasemekana watalii hawapendi kuona nyumba zikiwa karibu na barabara, wanapenda kuona miti, vichaka, n.k Je tumefikia hatua hii ya kukosa uhuru tukiwa kwetu?

Kinachoaikitisha zaidi ardhi maeneo haya ni adimu sana na nyingi ni za urithi hivyo watu wanafukuzwa kwao.

Kinachosikitisha zaidi mwezi ujao wamesema wanaanza kubomoa nyumba za watu na notisi tiyari wameshatoa.

Wakuu niishie hapa maana inaumiza sana.
 
Kinachosikitisha zaidi sidhani kama mmekaa kama serikali ya kijiji/ mtaa mkalijadili hili na kulitafutia ufumbuzi?

Kinachosikitisha zaidi kila tatizo tunakimbilia kwa viongozi wakubwa walioko karibu na ninyi wakati mnao viongozi wa mitaa na kijiji

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba nimesikitika sana na hiyo taarifa yako kwasababu machame ni nyumbani pia
 
Serikali ya kijiji haina info zozote mkuu, siyo mara ya kwanza kuulizia huko.

Machame sehemu gani mkuu, nazungumzia wahanga ambao ni wale waliojenga karibu na barabara mkuu
 
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba sheria lazima ifuate mkondo wake na mbunge hawezi kufanya lolote hapo labda asaidie wananchi wake kudai fidia tu
Sheria bila maelezo wala fidia mkuu?
 
Mimi niko Dar, lakini tuna eneo letu hapo, mwaka jana nilikuta x kweli, lakini wakasema itachukua muda sana kuvunja na watu watalipwa fidia

Sasa hii habari ya kuvunja nyumba mwezi huu tena bila fidia yoyote, wakati barabara hiyo imekuta watu hapo na sio watu wamefuata barabara hiyo maana maeneo mengi hapo ni ya urithi sio ya kununua,

Huyo Mbowe naona kajisahau kama ni mbunge wa HAI mpaka wananchi waandamanaji ndio atakumbuka,

Cha msingi kifanyike kikao cha wananchi wa hapo na kutoka na uamuzi mmoja katika kudai haki yao, tuache kuwategemea Hawa wanasiasa uchwara ambao wako kimaslahi zaidi,

Inauma sana aisee!
 
Pole sana mkuu, hizi X zimepigwa tena leo na zile za zamani ni kama upya huku wakiongezea na neno BOMOA pamoja na kuandika notisi ya kuvunja jengo.

X zinaanzia toka kona ya Lambo kuja mfoni, nshara mpaka Park.

Ni kweli barabara imekuta watu ila ndiyo hivyo Mbowe na wenzake wamepiga buyu mapaka waone tunalala nje labda watasema kitu.

Nasema ninachoshuhudia sijaadithiwa mkuu
 
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba sheria lazima ifuate mkondo wake na mbunge hawezi kufanya lolote hapo labda asaidie wananchi wake kudai fidia tu
Hata kama akiwaambia anaenda kuwasaidia kudai fidia atakuwa anawadanganya kwa sababu barabara haikuwafuata bali wao ndio wameifuata.

Kwa serikali hii ya Rais Magufuli, wasahau kupata fidia kama wameifuata hiyo barabara.

Msikilize aliyekuwa Waziri wa ujenzi ambaye kwa sasa ni Rais wa Tanzania anavyosema kuhusu watu waliofuata barabara.

Fuatilieni vizuri. Kuanzia mita 22.5 unatakiwa kulipwa fidia kwani ni barabara imekufuata wewe.
Ila kama uko ndani ya mita 22.5 imekula kwako.
Tafuteni wanasheria wawasaidie kutafsiri sheria za barabara. Mkimuingiza mbowe mtasumbuliwa zaidi kwani itaonekana anatafuta umaarufu
 
Back
Top Bottom