chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 19,685
- 22,694
Habari wakuu,.
Kumekuwa na sintofahamu kubwa sana kwa wakazi wa wilaya ya HAI ambayo mbunge mwenye dhamana ni Mhe Freeman mbowe.
Hususan kwa wananchi ambao wapo karibu na barabara hii ya machame.
Kabla barabara hii haijakabidhiwa Tanroads ilikuwa chini ya serikali za vijiji na halmashauri ya wilaya ya HAI, sasa baada ya Tanroads kuichukua wakaanza kuweka "X " katika majengo yaliyopo mita 22.5 kutoka katikati ya barabara hii ya machame miaka mitano iliyopita bila kuahidi fidia yoyote na wala hakuna maelezo yoyote kutoka ofisi yoyote akiwemo mbunge wa Jimbo hili la wilaya ya HAI Mhe Freeman.
Sasa leo wamekuja kuweka "X " mpya lakini wamezidisha vipimo, kutoka mita 22.5 za awali kufikia mita 30 kwa sasa bila kulipa fidia yoyote zaidi ya kuandika BOMOA.
Kinachosikitisha wananchi wengi ni kwamba barabara hii haina matumizi makubwa kiasi cha kusababishia watu wakae mita 30.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hii barabara haipanuliwi bali wanataka wananchi wakae mbali na barabara.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hata barabara za miji mikubwa wananchi hawakai mbali na barabara kwa umbali huo.
Kinachosikitisha zaidi hata mbunge mwenye dhamana Mhe Mbowe amekaa kimya juu ya sintofahamu hii waliyonayo wananchi wake.
Kinachosikitisha zaidi inasemekana watalii hawapendi kuona nyumba zikiwa karibu na barabara, wanapenda kuona miti, vichaka, n.k Je tumefikia hatua hii ya kukosa uhuru tukiwa kwetu?
Kinachoaikitisha zaidi ardhi maeneo haya ni adimu sana na nyingi ni za urithi hivyo watu wanafukuzwa kwao.
Kinachosikitisha zaidi mwezi ujao wamesema wanaanza kubomoa nyumba za watu na notisi tiyari wameshatoa.
Wakuu niishie hapa maana inaumiza sana.