Mbowe na Slaa sasa yatosha,watanzania hatutaki tena maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe na Slaa sasa yatosha,watanzania hatutaki tena maandamano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by itahwa, Mar 24, 2011.

 1. i

  itahwa Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kwa heshima na taadhima nawaomba waheshimiwa Mbowe na Slaa kusitisha mipango yao ya maandamano,Tanzania bado inataka hali yake ya amani na utulivu,maandamano mengi yanavunja utulivu na ni kero kwasisi watanzani,nilikuwepo kagera wakati slaa na jopo lake likipita,kwakweli walitujaza maneno machungu sana na kutufanya tuichukie serikali yetu tuliyoiweka madarakani kihalali,hii itatufanya tushindwe kuendelea na uzalishaji wetu kwa kuichukia serikali. maoni yangu ni kuwa maandamo yaliyofanyika yanatosha kwani ujumbe ulishafika lakini kuendelea na maandamano itakuwa ni kuchuana na serikali kitu ambacho si kizuri,siasa ni zaidi ya maandamano kuna mengi sana ya kufanywa na wanasiasa zaidi ya maandamano lakini kuendelea na maandamano itaonekana kuna chokochoko mnazitafuta!
   
 2. N

  NNYAMBALA Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe ndiye Msemaji wa Watanzania? kama hutaki ni wewe na siyo Watanzania.
  CDM- Aluta Contimuer!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wewe umelazimishwa kuandamana??
  Ulijifunza somo gani hapo kwenye BLUE?
  Na kwanini uache uzalishaji, wakati huo ndo mkate wako.

  usitumie sana hisia zako kuliko facts.

  Inawezekana wengine hawajaelewa kama ulivyoelewa wewe..
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,822
  Likes Received: 576
  Trophy Points: 280
  jua litawachwea. maandamano lazima. kama mnapinga tumieni nguvu ya dola yawakute ya Qaddafi. wapuuzi nyie

  CCM haitakiwi. i wonder why some people don;t want to appreciate this truth.
   
 5. Dr. Willibrod Slaa

  Dr. Willibrod Slaa Verified User

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 35
  Itahwa,
  Thanks for the post.
  i) Itahwa, ni simple logic tu, unaposema "Watanzania" uliwakusanya wapi kuwazungumzia katika ujumla wao. Hata mtoto wa darasa la kwanza anajua kuwa hhuu ni upotoshwaji.
  2) Itahwa, mimi na Mbowe ndio tunaozunguka nchi nzima. Ndio tunaokutana na Wananchi katika mikutano midogo na mikubwa hivyo tuna nafasi kubwa kujua Watanzania wanahitaji nini kuliko wewe.
  3) Itahwa, Mbowe na Slaa ni viongozi, angalau wana kura ya Watanzania iwe ndani ya Chama au nje ya Chama jambo lenye kutupa uhalali wa kuwazungumzia "watanzania" Wewe Itahwa, kakupa nani hasa mamlaka hayo. vzinginevyo usijifiche tukufahamu kwa jina lako halisi ili tukujue na kukupima vizuri na kauli zako zisizo na mshiko. Tunahitaji kujua kama kweli unajua maana ya "amani" au unaimba tu kama wimbo, au tukujue kama wewe ni mojawapo wa wanufaika wa ufisadi ambao dhahiri Watanzania walio wengi wameukataa na kuupinga kwa nguvu zao zote. Kama uko Serikalini ni vema ukasoma vizuri ishara za nyakati na kuzitumia ipasavyo na au kushauri mabosi wako inavyohitajika.
  4) Vinginevyo kauli zako ni maneno ya upotoshwaji, uchonganishi usio na maana na ni debe tupu.

   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 21,587
  Likes Received: 15,969
  Trophy Points: 280
  Kama serikali ya Tanzania ilivyo na wasemaji wengi unataka Watanzania nao wawe na wasemaji wengi mmoja wao akiwa wewe itahwa? Pse jisemee peke yako usiwasemee watanzania ambao hawajakutuma. Unakumbuka neno aliloropoka mzee Mapesa Bungeni wakati Tindu akitoa hoja ndani ya Bunge? basi nami naropoka kama Cheyo dhidi ya hoja yako!
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,001
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  unatulisha upepo tu, Watanzania gani unaowasemea wewe? Waambie NCCR na CUF wasitishe mikutano yao kama ujumbe umefika. Sijui kwanini mnahofu na maandamano ya Chadema. Ukitaka kujua watanzania wanaikubali chadema na maandamano yake jitahidi uhudhurie na yale ya Nyanda za Juu hasa mbeya na Iringa
   
 8. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,233
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa mimi Slaa na Mbowe ningekamatia hapo hapo.Sikujua kama mmekamatwa pabaya...Wanasema ukitupa jiwe gizani ukasikia "Uuwii" ujue kuna mtu limempata.
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  itahwa .... yaani usipojibu haya maswali uliyoulizwa nitaridhika kabisa wewe ni makamba .... kwani makamba hajawahi kuwa hata diwani kwa kuchaguliwa na wananchi
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  The known propensity of a democracy is to licentiousness which the ambitious call and the ignorant believe to be liberty
   
 11. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 14,514
  Likes Received: 2,606
  Trophy Points: 280
  wewe ni mpumbavu..nadhani pia wewe ni CCM B..nahisi pia huna ufahamu wa kutosha na siasa za leo,..nafikiri pia hauelewi misingi ya maendeleo,nakushauri ukamsome Carl Marx,Lenin,Pr.Shivji na J.K Nyerere juu ya mitizamo ya maendeleo

  usihishi kwa illusions..watanzania tupende kusoma tusije kuhaibika..hauna tofauti na Kikwete asiyejua ni nini kinapelekea taifa hili mbali ya kuwa na utajiri mwingi bado ni maskini

  raisi wako miaka 50 sasa ya uhuru bado anadai "ukoloni ndo kii cha umasiki Tanzania"...mbona Rwanda wametoka vitani juzi tu hawashikiki,kwa nini hela ya Kenya inapanda thamani ya Tanzania inazidi kushuka?ama Kenya haikuwahi kutawaliwa..?ama tuseme kenya iliitawala Tanzania?..si nakuuliza?
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  LAT huyo itahwa hana hoja ya msingi ya kujibu hayo maswali sababu inaonekana amekurupuka tu au amelishwa maneno ambayo hata hayajui
   
 13. M

  Munghiki Senior Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh wwe mzima kweli?wakati w2 wanataka mabadiliko wwe unapinga na kuyakalia au umetumwa!
  CDM kama kawa washa moto Dr Slaa mwendo huohuo.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  CHADEMA SISI VIJANA TUTAWAALIKENI MAANDAMANO ZAIDI KOTE NCHINI MPAKA KATIBA MPYA IPATIKANE BILA JANJA JANJA ZAIDI ZA MAFISADI: VIJANA TUMETAMBUA KWAMBA KUMBE MAANDAMANO NDIO LUGHA PEKEE WANAYOIELEWA KIURAHISI ZAIDI MAFISADI SERIKALINI

  Mhe Mbowe, Dr Slaa na Timu zima ya CHADEMA hakika MNATUCHELEWESHA MNO NA MAANDAMANO ZAIDI YA AMANI kote nchini mpaka Katiba Mpya ipatikane (1) kwa njia shirikishi zaidi kwa hatua zote, (2) Kuitisha Mkutano Mkuu wa Taifa kwa ajili ya Upangaji wa Ratiba ya Mchakato mziwa wa kuundwa upya kwa Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi; Bara na Visiwani!!!

  Kwa kuwa hali halisi tayari imetudhihirishia bila ya ta kubaki tashwishwi yoyote kwamba lugha pekee wanayoielewa vema serikali hii ya kifisadi iliojaa kiburi na dhuluma a kila aina ni LUGHA YA MAANDAMANO TU ndipo waweze kufikisha huduma muhimu kwa walalahoi tulio wengi nchini, basi sisi vijana kote nchini tunasema tunahitaji maandamano zaidi na zaidi ili MAFISADI wasiendelee kulala sikio na kugawana wao kwa wao Maslahi ya nchi.

  Maslahi ya taifa mbeeele kama tai!!! Maandamano zaidi ya kutuelimisha sisi wananchi juu ya haki zetu (ambalo ni jukumu la kikatiba kwa chama chochote cha kisiasa nchini) huku tukiwabana zaidi MAFISADI, yasicheleweshwe hata kwa sekunde.

  Maadam kumedhihirika wazi kwamba kumbe serikali HAINA MPANGO NA KUUNDWA KWA KATIBA NCHINI MOJA KWA MOJA NA SISI WANANCHI, kwa haraka zaidi huku wakijiamulia tu peke yao jinsi wapendavyo juu ya mambo yanayotuhusu bila kutushirikisha, sasa ndio haswaaa muda wa Maandamano ya kufa mtu wameukaribisha na sisi tunayaitikia si kipindi kirefu kwa staili ya aina yake zaidi safari hii!!

  CHADEMA; maandamano siku zote huwa tunaandaa sisi wenyewe wananchi na nyinyi kama chama huwa tunafanya kuwaalikeni tuu hivyo kama kuna mtu, chama na au taasisi yoyote nchini ambayo lugha yetu ya maandamano ya amani kwa mafisadi kidogo inampa shida basi waelekeze kwetu sisi wenyewe vijana tuno hapa kitaa na wala msibughudhiwa lolote kwa kupata tu mialiko ya ushiriki.

   
 15. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 491
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  asante Dk kwa kumjibu vizuri huyu jamaa, kwaatarifa tu. siku hizi mitandao hasa JF imevamiwa na vijakazi wa mafisadi mfano wa huyu sijui ITWAHA na jopo lake la maralia sugu type ambao lengo lao ni kuzima moto wa mageuzi unaoikumba TZ.

  sisi wananchi aliotusemea kwamba hatutaki maandamano, tunayataka na tunawatuma muendelee mpaka pale haki na mambo muhimu kwa watanzania yatakapotimizwa na serikali hii ya kifisadi.

  aluta continua CDM, msiwasikilize hawa viwavi jeshi wa ufisadi, GO CDM GOOOOOOOOOOOOO
   
 16. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,676
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :embarassed2:

  Hongera kwa kujivika zigo la kuwa msemaji wa Watanzania........Nadhani ungesema CCM hamtaki sio Watanzania

  Na mwaka huu mpaka za ndani zitapanda juu kama enzi za VIP
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 6,370
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  Mkuu comenti yako Itahwa hawezi kuielewa kwa jinsi nionavo uwezo wake wa kufikiri ulivo hakuna
   
 18. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 827
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani na wewe ni mtanzania???/ Afretall kwani umetumwa na nani kutusemea sisi watanzania??? Shut UP!!!!
   
 19. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,074
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sio Gaddafi na Wafuasi wake wanaoteseka tu bali hata na hao Wapinzani Walioanzisha Maandamano nao kiyama chao wamekiona na wanaendelea kukiona bali maji waliyavulia nguo hawana budi kuyaoga!

  Sasa Libya hakukaliki sio Serikali wala Wapinzani yaani ni vita na mauaji tu! ndio haya mnayoyataka hapa Tanzania?

  Unaweza kuwa Umesoma lakini ukawa Mpumbavu!!!
  Nyambafu kabisa!!!!
   
 20. L

  LAT JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  zubeda .... mbona una jazba kama vile G-String imekubana
   
Loading...