Jiji la Arusha linatarajiwa kuzizima siku ya Jumamosi wakati Mkiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Wilfred Lwakatare watakapohutubia wakazi wa jiji hilo.
Viongozi hao wanatarajiwa kuhitimisha kampeni za udiwani ambapo uchaguzi wake utafanyika Jumapili.
Taarifa zilizopatikana kutoka Arusha ni kwamba maelfu ya wafuasi wa Chadema wanatakiwa kwenda kuwalaki viongozi hao uwanja wa ndege siku ya Ijumaa.
Mapokezi hayo yanatarajiwa kushirikisha magari,pikipiki,baiskeli na watembea kwa miguu.
Mikutano ya Mbowe jijini Arusha imekuwa ikisababisha jiji kusimama kutokana na idadi kubwa ya wananchi kufunga shughuli zao kwenda mkutanoni.
Mpaka sasa tathmini inaonyesha Chadema itashinda kata zote kwa ushindi usiopungua asilimia 80%