Mbowe na Lwakatare kulitikisa jiji la Arusha Jumamosi

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Jiji la Arusha linatarajiwa kuzizima siku ya Jumamosi wakati Mkiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Wilfred Lwakatare watakapohutubia wakazi wa jiji hilo.

Viongozi hao wanatarajiwa kuhitimisha kampeni za udiwani ambapo uchaguzi wake utafanyika Jumapili.

Taarifa zilizopatikana kutoka Arusha ni kwamba maelfu ya wafuasi wa Chadema wanatakiwa kwenda kuwalaki viongozi hao uwanja wa ndege siku ya Ijumaa.

Mapokezi hayo yanatarajiwa kushirikisha magari,pikipiki,baiskeli na watembea kwa miguu.

Mikutano ya Mbowe jijini Arusha imekuwa ikisababisha jiji kusimama kutokana na idadi kubwa ya wananchi kufunga shughuli zao kwenda mkutanoni.

Mpaka sasa tathmini inaonyesha Chadema itashinda kata zote kwa ushindi usiopungua asilimia 80%
 
Safi sana MAKAMANDA tuko pamoja, Hakika taifa linakombolewa sasa. Baadaye mkapige kambi Bukoba wale MAKAMANDA nao wamwone kijana wao aliyefanyiwa FITNA na MAGAMBA
 
June 16...

....chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema chadema.....usishangae nahesabu kura....
 
CHADEMA ndio mpango mzima. Twanga kote kote mpaka CCM na mataahira wake wote wasambaratike.
CHADEMA yatosha!!!
 
Jiji la Arusha linatarajiwa kuzizima siku ya Jumamosi wakati Mkiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Wilfred Lwakatare watakapohutubia wakazi wa jiji hilo.

Viongozi hao wanatarajiwa kuhitimisha kampeni za udiwani ambapo uchaguzi wake utafanyika Jumapili.

Taarifa zilizopatikana kutoka Arusha ni kwamba maelfu ya wafuasi wa Chadema wanatakiwa kwenda kuwalaki viongozi hao uwanja wa ndege siku ya Ijumaa.

Mapokezi hayo yanatarajiwa kushirikisha magari,pikipiki,baiskeli na watembea kwa miguu.

Mikutano ya Mbowe jijini Arusha imekuwa ikisababisha jiji kusimama kutokana na idadi kubwa ya wananchi kufunga shughuli zao kwenda mkutanoni.

Mpaka sasa tathmini inaonyesha Chadema itashinda kata zote kwa ushindi usiopungua asilimia 80%

Asilimia 80% mijitu mingine bana
 
Usishangae Mahakama ikaamuru Lwakatare akamatwe kwa kuvunja masharti ya dhamana yanayomtaka asitoke nje ya Dar bila kibali cha mahakama.
 
Duh sasa hapo wamecheza na mazingira mana lwakatare famous sahiz naona wametumia nafas effectvly... Bgup 2 CHADEMA.
 
wanakuja kumaliza machali tunawasubiri.....inabidi na akina nchemba nao wafunge kampeni siku hiyohiyo au...
 
Lwakatare amepewa kibali cha kutoka nje ya Dar na mahakama?

Endapo ataomba kibali na mahakama ikaridhika kuwa halina madhara basi nafikiri watamruhusu labda jamaa watumie karata ya turufu. Ila ni lazima apate ruhusa toka mahakamani vinginevyo akienda kichwa kichwa kwa ukaidi iatakula kwake. Na huo utakuwa ni mtego sasa wanasubiri tu.
 
Nakumbuka 2010 dk slaa alifungia kampeni mbeya mjini pale ndipo sugu alipowapga bao la kisigino kwa kuwaacha kwa kura nyingi sana.... Japokuwa alikuwa na uhakika wakushinda ila ile ilisaidia kushinda kwa kishindo.. Naifananisha hiyo na wanachotaka kufanya arusha..... Hakuna mahali kama A-TOWN A-TOWN...
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom