WanaJF,
Ni nani kati yetu ambae hajasoma waraka wa mabadiliko ulioandaliwa na Dr Kitila?
Kama wote tumesoma na tumeelewa yaliyomo, ni kwanini wahusika wa zile tuhuma wajikaushe na kufanya mambo yaonekane kawaida?!
Kwa tafsiri ya kawaida, mtu anapo tuhumiwa kwa tuhuma fulani, na mtu huyo akikaa kimya, tafsiri yake ni kwamba amekubaliana na tuhuma.
Hivyo basi, vinara hao wawili wa CHADEMA (Mbowe na Dr Slaa) ambao wanakabiliwa na tuhuma nzito, kwa sasa wana options mbili, moja wawaombe wanachama na Watanzania kwa ujumla radhi ama wajiuzuru nafasi zao ili hatua za uchunguzi zichukuliwe.
Aidha, CHADEMA kwa sasa ni chama kilichojipambanua kuwa ni adui wa ufisadi na unyonyaji wa namna yoyote.
Hivyo basi, ni wakati na fursa kuthibitishia Watanzania hilo. Vinginevyo, Watanzania kwenye hili hatuwezi kuwaelewa mpaka kieleweke.