Mbowe na dhana ya vyama mamruki, Kweli Tanzania vipo?

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
Kimantiki maelezo ya mh, Mbowe wakati akitoa msimamo wa chama cha CHADEMA kuhusiana na kusimamishwa kwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho mh, Tundu Lisu na kamati ya maadiri ya tume ya taifa ya uchaguzi, Mbowe amevirushia dongo vyama ambavyo viliunga mkono kusimamishwa kwa mgombea wa chama hicho kuwa ni vyama mamuruki vya CCM. Zipo sababu kadhaa zinazonifanya nipingane kidogo na kauri hiyo:
  1. Mh, Mbowe hana sababu za msingi kudhani kuwa wote waliopiga kura dhidi ya chama chake ni mamuruki,walichoangalia ni kutendeka kwa kosa au la.
  2. Kutochukuliwa hatua kwa makosa yanayotendwa na mgombea kupitia CCM, yanayofanana na hayo au mengine yanayo katazwa na sheria ya vyama au na Maadiri.
  3. Tangazo la chama chake kuunga mkono chama cha ACT kwenye kinyang'anyilo cha Zanzibar hilo limedhihirisha kuwa kuungana mkono sio umamuruki.
Ni kweli kuwa adui wa vyama vya upinzani ni mmoja tu CCM,yanakuwa ni maajabu kidogo kwa wapinzani kuiunga mkono CCM kukandamiza upinzani lakini kumbukeni sababu zilizowafanya wabunge wa upinnzani kuunga mkono juhudi ndio hizo hizo zimewafanya wakina MREMA,CHEYO na wengineo kama mnavyo wafahamu kuwa wapambe wa CCM sitaki kuwaita mamruki au vibaraka.

Naamini kwa kiwango furani kuwa ACT,CHAUMA NA CHADEMA yenyewe ndio vyama vilivyo pinga uamuzi huo mnataka kuniambia kuwa hawa wengine wote ni mamruki? ruksa povu
Mrema na Cheyo waomba CHADEMA ifutwe
 
Mkuu Kama hoja yako ilivyo na kwa maongenzi ya mbowe, vipo vyama ambavyo Kila uchaguzi ukianza ndo utavisikia na bahada ya hapo ni kimia ,Kuna vyama vya kimkakati na vyama vya upinzani ,wasomi wa sayansi ya siasa wanaelewa vizuri Sana hili na si tz tu ,mchezo wa siasa ni mgum mno kwa iyo mbowe iliongea akimanisha maana amekua kwenye siasa kwa mda mrefu hivyo anajua,ila Kama ni mshabiki wa siasa kwa juu juu unaweza usimuelewe mbowe
 
Back
Top Bottom