Mbowe na CHADEMA warudishwa kwenye mstari baada ya kifinyo kikali

kababu

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,699
804
Licha ya awali kuwa na msimamo tofauti, vyama vya Chadema na NCCR-Mageuzi vilivyoweka msimamo wa kutokushiriki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) vimetengua msimamo huo sasa vitashiriki.

Mkutano huo wa maridhiano ya umoja wa kitaifa, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 unatarajiwa kufanyika Machi 30 na 31 jijini Dodoma, ukiwashirikisha Rais Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Awali, vyama hivyo vya upinzani vilisusia kushiriki shughuli yoyote ya kisiasa, ukiwamo mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa madai kwamba hoja tano walizokuwa wanazilalamikia hazikufanyiwa kazi kama wanavyotaka.

Kwa nyakati tofauti, viongozi wa vyama hivyo jana walisema sasa wapo tayari kushiriki mkutano huo baada ya hoja walizokuwa wakizilalamikia kuanza kufanyiwa kazi, ikiwamo kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Uhusiano wa Umma wa NCCR- Mageuzi, Edward Simbeye alisema kuachiwa Mbowe kulikuwa miongoni mwa hoja walizozisimamia.

“Kamati kuu ya chama chetu kupitia kikao cha kamati kuu walichofanya jana (juzi) Machi 10, tumejiridhisha baada ya kuanza kufanyiwa kazi hoja tulizozitoa. Kwa msingi huo hatutakuwa na sababu ya kutoshiriki mkutano wa majadiliano ya amani kule Dodoma,” alisema.

Simbeye alisema hoja yao nyingine walivyokuwa wanataka utekelezaji ni kabla ya mkutano huo wa Machi 30 na 31, ufanyike mkutano mdogo wa awali utakaovikutanisha vyama vya siasa kuweka hoja zao kwa pamoja.

“Wamekubali hilo na utafanyika Machi 18, Rais atakuwepo na kila chama kitatuma mwakilishi na NCCR ni mwenyekiti wetu, James Mbatia,” alisema Simbeye.

Naye Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipozungumza na gazeti hili aliunga mkono hoja ya kuachiwa huru mwenyekiti wao Mbowe na kueleza watashiriki mkutano huo huku wakiendelea kusisitiza utekelezaji wa hoja zao nyingine.

“Hoja yetu ilikuwa Mbowe aachiwe kwanza, hilo limefanyika, hivyo tutashiriki kwa kuwa ni wajumbe, lakini madai yetu mengine, ikiwemo Katiba Mpya tutaendelea nayo,” alisema.

Katika maelezo yake, Mrema alisema wanaendelea kutafuta njia sahihi ya kuurudisha mchakato wa Katiba Mpya mapema ili kuleta suluhisho la kudumu la changamoto zinajitokeza mara kwa mara ndani na nje ya siasa.

Madai mengine kwa vyama hivyo ilikuwa kuruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa, ikiwamo mikutano ya hadhara ili kuzungumza na wanachama wao pamoja na kujijenga katika maeneo ambako hawana nguvu kubwa.

Vyama vitakavyoshiriki mkutano huo ni Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha ACT-Wazalendo na Chama cha Mapinduzi (CCM) na vin gine vyenye usajili wa kudumu.
 
Back
Top Bottom