Mbowe na CHADEMA mnataka kumkwamisha Rais Samia kwakuwa amewalegezea kidogo?

CCM hawako tayari kutoka madarakani ndio maana akingia raisi yoyote kupitia ccm lazima wakupe plan yao yakutawala kwa muda wanaoutaka wao

Ndio maana alivyoingia mwendazake ikulu ccm wakampa plan yao ambayo ni kuhakikisha ccm inatawala bila ukomo au kutolewa madarakani na vyama vingine

Mwendazake akaipokea na akafanyia kazi plan aliyopewa na ccm kuongoza na kukilinda chama kwa nguvu zozote

Nanukuu "Nimekuajiri mimi nakulipa mshahara mimi, nimekupa gari mimi alafu unaenda kutangaza mgombea wa mpinzani kashinda"?

katiba ni muhimu sana
 
Friends and Enemies,

Mbowe na CHADEMA wanataka kutupeleka wapi Tena? Je, ni kweli kwamba walishazoea ile hali ya kupelekwa kibabe na mwendazake na wameikumbuka kisha wameanza kutingisha kibiriti?

Katiba mpya ni suala la mchakato, ni suala mtambuka na jumuishi kwa makundi mbali mbali ndani ya nchi hii.

Wao kama wanasiasa ni kundi moja tuh wenye maslahi yao na katiba hii, na maslahi yao kama chama cha siasa ni kushika Dola, lakini Kuna makundi mengine meengi ambayo nayo yana maslahi yao vile vile kama wao, sasa iweje wao walishikie bango kwa kiasi hiko hadi kutishia kuingia barabarani kufanya fujo?

Rais Samia kaahidi na kaomba apewe muda, hawataki na wanataka kulazimisha.

Magufuli hakuahidi, na alisema siyo kipaumbele chake, waliufyata na kukaa kimya, sasa tunawauliza wanataka KUMKWAMISHA huyu mama kwasababu gani?

Kwa kuwa ni Muislam au kwa kuwa ni mwanamke?

Wana ajenda gani kwani.
mbafu ww
 
Friends and Enemies,

As they sow,so shall they reap...

Chadema wahusike na kichwa Cha habar hapo juu,sisi wananchi tusiokuwa na affiliation zozote na hawa wanasiasa siku zote mindset zetu huwa free kuzungumza chochote kwa maslahi ya Taifa. Letu,

Kwa watu kama chadema,ukiongea chochote kinachohusu kuwakosoa wao MOJA kwa MOJA wanajudge kuwa mkosoaji ni mtu wa mrengo mwingine,lakin potelea mbali tutazid kuongea,

Chadema they need to stop crying like babies na wajikite kutengeneza chama kwa kufanya overhaul na kuingiza fikra mpya na NGUVU mpya kwenye chama,for over 17 years now mbowe na wenzake lazima watambue kwamba kama vile ambavyo watanzania wameichoka ccm ndivyo hivyo hivyo ambavyo wameichoka chadema,na hiyo ni kwa kuwa fikra za viongoz ni zile zile,sura ni zile zile,approach zao ni zile zile,watanzania wakiwaangalia chadema hawaon jipya zaid zaid ya kuwaona wao kama ni wachumia tumbo tuh refers kesi hii ya wabunge wao hawa covid 19 na hii hama hama ya viongoz wao waandamiz kwenda kuunga mkono juhud especially enz zile za mwendazake,

Muda unaenda,wanashinda kujenga chama na kusoma fikra za watanzania,wamekomaa kumchafua RAIS SAMIA na kumforce aendeshe nchi kulingana na MATAMANIO yao,

Rais SAMIA ANAONGOZA NCHI kutekeleza ilani ya chama chake na kutimiza ahad alizowaahid watanzania kipind Cha kampen akiwa na mwendazake,na hayupo hapo kutekeleza maagizo ya chadema na kuendesha nchi kama wao wanavyotaka,

Hata kama ni kweli mamlaka Ina Nia ya kubadili upepo wake wa kuruhusu mikusanyiko ya kisiasa,je ni kwa kipind hiki Cha maradhi ya Covid 19?,pia kama wanasema katiba hiyo wanayoipigania ni kwa maslahi ya wananchi ambao wanataka kuwakusanya,kipi muhim kwa hao wananchi kwa sasa zaid ya afya zao?

Mbowe anataka watanzania waendelee kuathirika na huu ugonjwa na wazikwe kama alivyozika marehem kaka yake??

Chadema watavuna hiki wanachokipanda,muda ni mwalim mzuri Sana,tuzid kuomba uhai na afya tutaona matunda ya hiz harakati zao uchwara...
Najua kimoyomoyo unasema Magufuli was right ila kwa kinywa hutaki kutamka. Naona njia hiyohiyo mama anaichukua
 
Wananchi waliichagua CCM kutokana na Ilani yake sio ahadi ya katiba mpya
Kama hujui ngoja nikuambie. CCm haikushinda uchaguzi 2020 ushahidi
1. Kinondoni vijana walikusanywa siku mbili kabla ya uchaguzi waliahidiwa kulipwa 5000 wakapewa karatasi za kura na kuweka alama za kumchafua ccm, raisi, mbunge na madiwani. Ushahidi huu upo banana mana mdogowangu alishiriki na hahwajalipwa mpaka leo
2. Vituo vya kupigia Kura zote nchini vilifunguliwa saa 9 usiku kazi ilikuwa moja tu kupiga kura kwa ccm. Wasimamizi wa uchaguzi waliambiwa wafanye hivyo na TISS na wasiogope chochote. Waliopewa jukumu la kusimama uchaguzi ni watumishi wa umma wenye mlengo wa ccm. Hili naweza kulithibitisha popote pale.
Unadai ccm ulishinda ilishanda wapi???
 
THE BIG SHOW ,

Natofautiana na wewe unapohusisha harakati za Chadema kudai Katiba mpa na suala la IMANI ya Rais Samia Suluhu pamoja na JINSIA yake.

Kilichotokea kati ya Rais Samia Suluhu na uongozi wa Chadema ni kupishana kwa mitizamo yao kuhusu muda gani ni sahihi kwa suala la Katiba mpya kushughulikiwa.

Sisi tunaowafuatilia viongozi hawa, tunapaswa kupima kauli na misimamo iliyotolewa na kila upande, na kuangali upande upi umejenga hoja iliyo sahihi.

Binafsi sijakubaliana na hoja ya Rais Samia Suluhu ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Zuio hilo linakwenda kinyume cha katiba na sheria zetu.

Pia sijashawishika na hoja ya Rais Samia Suluhu kwamba wabunge peke yao ndio wanaoruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Uamuzi huo ukitekelezwa utakipendelea chama cha Raisi, CCM, na kuvikandamiza vyama vingine vya siasa.

Vyama vya upinzani huku Tanganyika vina mbunge ktk jimbo moja tu, hivyo CCM watafanya mikutano ktk majimbo zaidi ya 200++ nchi nzima, huku Chadema wakifanya mikutano katika jimbo moja tu.

Kwa upande mwingine nadhani Mh.Mbowe anakosea anapolalamika, au kulazimisha, Rais akutane na Chadema. Kama Rais anaamini muda haujafika wa kuonana na Chadema basi wamuache aendelee na ratiba na majukumu yake aliyojipangia.

Kila upande hapa uendelee na shughuli, ratiba, na mipango yake. Raisi Samia Suluhu aendelee kurekebisha uchumi kama alivyoahidi. Chadema nao waendelee na operation yao ya kuelimisha kuhusu Katiba mpya, na wasibugudhiwe na mtu au chombo chochote.

Rais Samia Suluhu akirekebisha uchumi Watz wote tutafaidika. Chadema nao wakihamasisha kuhusu Katiba bora umma mzima utafaidika.
Umemaliza uchambuz mzuri mnoo,wenye kusikia wasikie
 
Kama kiongozi anaweza kukujibu asiyetaka kulipa tozo ahamie burundi, basi nadhani hii reli ni level za train ya maglev.
Kumbe watumiaji wa mitandao ya simu tunaibiwa sana;
1.inasemekana Dk.1 unayo tumia kuzungumza kupitia mtandao wa simu sio sawa na Sekunde 60 ktk saa yako ya mkononi, kwa maaana mitandao inatuibia sisi watumiaji.

2. Inasemekana upikipiga sim kwa mtu hata kama haijapokelewa kuna SMS unatumiwa ikionyesha kuwa umetumia sekunde kadhaa!!
kuna udanganyifu mkubwa unao fanywa na baadhi ya mitadao ya simu. pamoja na kuikosesha serikali mapato halali.
TCRA Tafadhali chunguzeni myanya hii.
 
Kumbe watumiaji wa mitandao ya simu tunaibiwa sana;
1.inasemekana Dk.1 unayo tumia kuzungumza kupitia mtandao wa simu sio sawa na Sekunde 60 ktk saa yako ya mkononi, kwa maaana mitandao inatuibia sisi watumiaji.

2. Inasemekana upikipiga sim kwa mtu hata kama haijapokelewa kuna SMS unatumiwa ikionyesha kuwa umetumia sekunde kadhaa!!
kuna udanganyifu mkubwa unao fanywa na baadhi ya mitadao ya simu. pamoja na kuikosesha serikali mapato halali.
TCRA Tafadhali chunguzeni myanya hii.
Sasa haya ni makosa ya nani? Si kuna TCRA ina maana tuna serikali isiyofanya kazi yake.
Hizi tozo ni kubwa saa mimi sikujua impact yake mpaka juzi nilipomtumia mtu pesa 20,000 gharama ya kutuma ni1560, na yeye akienda kutoa anakatwa zaidi ya 20,000.
Yani muamala ela inayokatwa ni almost 23% hii haiwezekani.
Na watu wengi wanaotumia hii huduma wanatuma na kutoa pesa isiyozidi 40,000.
 
Back
Top Bottom