chaboo
Member
- Dec 11, 2013
- 78
- 26
MWENYETI wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) Freeman
Mbowe, amewataka wanachama wa
chama hicho wamuulize Mbunge Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe wapi alikomtoa
hadi kufikia ngazi na hadhi aliyonayo
sasa katika medani ya siasa nchini.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika
kongamano la miaka 52 ya Uhuru wa
Tanzania Bara, lililoandaliwa na Umoja
wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chaso)
kwa kushirikiana na Baraza la Vijana la
Chama hicho (BAVICHA)
Katika kongamano hilo lililofanyika
katika Hoteli ya Land Mark, Mbowe
ambaye alianza kwa kutaja historia yake
kama mwasisi kijana wa CHADEMA na
mwenyekiti wa kwanza, alisema mwaka
2003 akiwa katika harakati za kukijenga
chama, alipita katika vyuo mbalimbali ili
kupata vijana wasomi wajiunge na
CHADEMA na ndipo alipompata Zitto,
akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Nikiwa katika harakati zangu za
kukijenga chama, nilipita Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam nilibahatika kuwapata
kina John Mrema, Halima Mdee, Zitto
Kabwe, John Mnyika wakiwa viongozi
ambao walipenda siasa ya mabadiliko,
nami nikaondoka nao bila ya kusita,
alisema.
Alisema nia ya kuwachukua vijana hao ni
kujenga chama kama taasisi ili kisonge
mbele tofauti na ilivyo sasa na siyo
kujenga jina la mtu kama watu
wanavyotaka iwe au wanavyodhani.
Mbowe alisema akiwa na vijana hao
pamoja na viongozi wengine, walifanya
kazi kama timu ili kuhakikisha
wanakiingiza chama hicho Ikulu,
akiamini kuwa asingeliweza peke yake
kukipeleka mbele chama hicho.
Aliwataja viongozi aliowachukua kutoka
katika vyama vingine vya siasa kuwa ni
pamoja na Mkurugezi wa Fedha wa
chama hicho, Antony Komu, Tundu
Lissu, Mabere Marando ambao walitoka
NCCR Mageuzi.
Wengine ni Godbless Lema, Saidi Arfi na
Mchungaji Peter Msigwa ambao
walikuwa TLP na Ezekia Wenje aliyetoka
Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa
mwenyekiti wa tawi moja la chama hicho
huku Mwanza.
Alisema safari ya kukijenga chama sio
lelemama kwani ni sawa na treni
inayotoka Dar es Salaam kuelekekea
Kigoma huku akiamini wote watafiki,
lakini imekuwa tofauti kwani wapo
walioshuka njiani.
Safari yetu ya Kigoma toka Dar es
Salaam ilikuwa ndefu sana wapo
walioshuka katika kituo cha kwanza tu
Pugu, wengine Morogogo na vituo
vingine vilivyofuata na kupata vilevile
lakini tutafika tu, alisema.
Akitoa historia fupi ya maisha yake
katika siasa, Mbowe alisema aliingia
akiwa kijana mdogo muasisi ambaye
alipata nafasi ya kukiongoza chama kama
mwenyekiti wa kwanza wa vijana,
baadaye kupata nafasi mbalimbali
ikiwamo uenyekiti.
Alisema aliingia katika chama hicho na
kuchanguliwa kuwa kiongozi, lengo
likiwa kufanya mabadiliko kwa vitendo
na si kwenda kupata faida kama watu
wengine wanavyofikiria.
Lakini nilifanya kazi yangu ya kuijenga
CHADEMA hatua kwa hatua kwa maana
nyingine nimefanya kazi ya chama kwa
miaka 23 sasa bila kulipwa mshahara
wowote kwa sababu mimi ni
mfanyabiashara, alisema.
Alisema chama akitatoa maamuzi ya
kumwonea mtu yeyote bali
kitamhukumu mtu kutokana na makosa
yake.
na Maendeleo (CHADEMA) Freeman
Mbowe, amewataka wanachama wa
chama hicho wamuulize Mbunge Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe wapi alikomtoa
hadi kufikia ngazi na hadhi aliyonayo
sasa katika medani ya siasa nchini.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika
kongamano la miaka 52 ya Uhuru wa
Tanzania Bara, lililoandaliwa na Umoja
wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chaso)
kwa kushirikiana na Baraza la Vijana la
Chama hicho (BAVICHA)
Katika kongamano hilo lililofanyika
katika Hoteli ya Land Mark, Mbowe
ambaye alianza kwa kutaja historia yake
kama mwasisi kijana wa CHADEMA na
mwenyekiti wa kwanza, alisema mwaka
2003 akiwa katika harakati za kukijenga
chama, alipita katika vyuo mbalimbali ili
kupata vijana wasomi wajiunge na
CHADEMA na ndipo alipompata Zitto,
akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Nikiwa katika harakati zangu za
kukijenga chama, nilipita Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam nilibahatika kuwapata
kina John Mrema, Halima Mdee, Zitto
Kabwe, John Mnyika wakiwa viongozi
ambao walipenda siasa ya mabadiliko,
nami nikaondoka nao bila ya kusita,
alisema.
Alisema nia ya kuwachukua vijana hao ni
kujenga chama kama taasisi ili kisonge
mbele tofauti na ilivyo sasa na siyo
kujenga jina la mtu kama watu
wanavyotaka iwe au wanavyodhani.
Mbowe alisema akiwa na vijana hao
pamoja na viongozi wengine, walifanya
kazi kama timu ili kuhakikisha
wanakiingiza chama hicho Ikulu,
akiamini kuwa asingeliweza peke yake
kukipeleka mbele chama hicho.
Aliwataja viongozi aliowachukua kutoka
katika vyama vingine vya siasa kuwa ni
pamoja na Mkurugezi wa Fedha wa
chama hicho, Antony Komu, Tundu
Lissu, Mabere Marando ambao walitoka
NCCR Mageuzi.
Wengine ni Godbless Lema, Saidi Arfi na
Mchungaji Peter Msigwa ambao
walikuwa TLP na Ezekia Wenje aliyetoka
Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa
mwenyekiti wa tawi moja la chama hicho
huku Mwanza.
Alisema safari ya kukijenga chama sio
lelemama kwani ni sawa na treni
inayotoka Dar es Salaam kuelekekea
Kigoma huku akiamini wote watafiki,
lakini imekuwa tofauti kwani wapo
walioshuka njiani.
Safari yetu ya Kigoma toka Dar es
Salaam ilikuwa ndefu sana wapo
walioshuka katika kituo cha kwanza tu
Pugu, wengine Morogogo na vituo
vingine vilivyofuata na kupata vilevile
lakini tutafika tu, alisema.
Akitoa historia fupi ya maisha yake
katika siasa, Mbowe alisema aliingia
akiwa kijana mdogo muasisi ambaye
alipata nafasi ya kukiongoza chama kama
mwenyekiti wa kwanza wa vijana,
baadaye kupata nafasi mbalimbali
ikiwamo uenyekiti.
Alisema aliingia katika chama hicho na
kuchanguliwa kuwa kiongozi, lengo
likiwa kufanya mabadiliko kwa vitendo
na si kwenda kupata faida kama watu
wengine wanavyofikiria.
Lakini nilifanya kazi yangu ya kuijenga
CHADEMA hatua kwa hatua kwa maana
nyingine nimefanya kazi ya chama kwa
miaka 23 sasa bila kulipwa mshahara
wowote kwa sababu mimi ni
mfanyabiashara, alisema.
Alisema chama akitatoa maamuzi ya
kumwonea mtu yeyote bali
kitamhukumu mtu kutokana na makosa
yake.