Mbowe muige Raila Odinga shirikiana na Rais Magufuli kuijenga Tanzania yetu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,876
141,812
Ni ushauri tu kwa mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani Bungeni mh Mbowe kwamba afanye siasa za kushirikiana na serikali ili tuijenge nchi yetu.

Pale Kenya Kiongozi wa Upinzani mh Raila Odinga yuko mstari wa mbele akishirikiana kwa karibu na Rais Uhuru Kenyata katika kuwaletea wananchi wao maendeleo.

Ni vema Mbowe akaiga jambo hili jema kwa jirani zetu na siyo kupinga pinga tu kila jambo kama Zitto Kabwe wa ACT wazalendo.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wewe unawashwa na nini? Wewe si ushamuunga mkono unatosha. Wengine waache waamini njia nyingine ni kuwa kinyume nae kwa mambo mengine. Kwako wewe yote yanayotendeka Tanzania ni mazuri au? Maana sijakuelewa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uongozi unaanzia kwa Raisi ni lini Magu amejaribu kuwa kama Kenyatta na kutaka makubaliano! Tumekuwa na utamaduni wa kulalamikia upande mmoja wakati ukweli ni kwamba Mbowe ameongea siku ya uhuru wazi je Magu kafanya nini. Watu ambao wataumia ni Watanzania wote
Ajifuze maana ya 'Self image' hii ni tabia ambayo kila binadamu anayo hujijenga kwa muda mrefu kuibadirisha siyo rahisi
 
uongozi unaanzia kwa Raisi ni lini Magu amejaribu kuwa kama Kenyatta na kutaka makubaliano! Tumekuwa na utamaduni wa kulalamikia upande mmoja wakati ukweli ni kwamba Mbowe ameongea siku ya uhuru wazi je Magu kafanya nini. Watu ambao wataumia ni Watanzania wote
Mbona Mrema, Cheyo, Shibuda na Prof Lipumba wanashirikiana na serikali ya Rais Magufuli, yeye Mbowe anafeli wapi?!
 
Mbona Mrema, Cheyo, Shibuda na Prof Lipumba wanashirikiana na serikali ya Rais Magufuli, yeye Mbowe anafeli wapi?!

Labda utueleze kushirikiana una maana gani? na unavyosema kafeli kwenye mtihani upi? Kama nilivyosema ushirikiano ni pande mbili. Mbona wakati wa Kikwete matatizo ya sasa hivi hayakuwepo hivi
 
Siasa za Kenya ni tofauti sana na za kwetu...Sisi zetu zimetawaliwa na uimbaji wa mapambio ya kusifu then unaonekana Mzalendo.

Hadi kufikia marithiano ya Raila na Kenyatta kulikuwa na process ndefu sana...Kenyatta ni Gentleman...haya madaraka ni ya kupita tu kama yalivyo maisha ya mwanadamu ...why utese wakenya wenzako. ? Akaona bora yaishe....
Hapa kwetu Rais Magu ndiye kwa kwanza kuanzisha mambo haya na si mwingine yoyote yule.
 
johnthebaptist,
Bwashee hebu nikuulize - hicho unachokisema kinawezekana vipi endapo Rais Magufuli hataki kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani? Kwa upande wa Kenya hili liliwezekana kwa kuwa yeye hakuwa na kinyaa cha kukutana na wapinzani.
 
Back
Top Bottom