Mbowe: Mtanzania yeyote ana uhuru wa kutoa maoni, polisi na serikali wasitufunge midomo

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Habari wakuu,

CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari leo tarehe 29/06/2017. Watazungumza na waandishi wa juu ya masuala kadhaa yanayoendelea nchini.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama wakiwemo Viongozi Wastaafu Serikalini.

Nitawapa updates ya kilichojiri
Stay tuned

=======
Updates

Moja ya masuala yaliyojiri kwenye mkutano huo ni;

=>Kitendo cha polisi kuzuia waandishi wa habari kwenye tukio la kuhojiwa Edward Lowassa kuripoti habari kwa uhuru, na kwamba urafiki umekuwepo wakati wakiwa na habari ya kuwapendeza wao tuu.

=>Kuhusu alichozungumza Lowassa, Mh. Mbowe anasema; viongozi wa kidini waliokuwa mahabusu kwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani na mtanzania yeyote ana uhuru wa kutoa maoni.

=>Mh Mbowe anasisitiza polisi na serikali wasiwafunge midomo. Na kama kuna hoja yoyote ambayo hao viongozi wa kiroho wanashtakiwa nayo basi shughulikiwe mapema


Lowassa ambaye aliwania urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga kupitia chama hicho, Mwita Waitara.

Katika hafla hiyo, Lowassa anadaiwa kumtaka Rais John Magufuli kutafakari upya hatima ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu maarufu ‘Uamsho’ wanaoshikiliwa mahabusu kwa zaidi ya miaka minne, wakikabiliwa na tuhuma za ugaidi.

Kwenye hafla hiyo, Lowassa alisema ni jambo la fedheha kwa nchi iliyopata uhuru zaidi ya miaka 50 kuwaweka mahabusu viongozi wa dini bila kesi kusikilizwa mahakamani.

Kutokana na matamshi hayo, Juni 27 mwaka huu ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), ilimwandikia barua ya kumtaka afike katika ofisi za makao makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es Salaam ambako alihojiwa kwa saa nne kisha kuachiwa na kuhitajika kuripoti tena jana.

Aripoti Polisi

Lowassa aliitikia wito wa kuripoti jana katika ofisi ya DCI majira ya saa sita 6:00 mchana akisindikizwa na Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibalata. Ilipofika saa 6:15 mchana Lowassa aliondoka katika ofisi hizo kupitia mlango wa nyuma na kwenda moja kwa moja nyumbani kwake.

Baada ya kufika nyumbani kwake, Lowassa alizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa hakuhojiwa chochote zaidi ya kuambiwa aripoti tena Julai 13, mwaka huu, kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Alipoulizwa endapo maneno aliyoyazungumza wakati wa futari alikuwa ameteleza, Lowassa alisema anaamini alikuwa sahihi na anasimamia kile alichokizungumza.

“I stand on what I said (Ninasimamia kile nilichokizungumza), ninaamini niko sahihi. Watu hawa waondolewe gerezani na mwenye mamlaka ya kuwatoa mbali na mahakama ni Rais,” alisema Lowassa.

Alisema demokrasia imeshaanza nchini inaendelea na ni vigumu kuizuia huku akiwataka wananchi kutokuwa na hofu.

Kauli ya Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema matamshi hayo yaliyotamkwa na Lowassa wakati wa futari ni ya Chadema na kwamba Lowassa alitumika kupeleka ujumbe tu.

Mbowe alisema hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, kukamatwa kwa Masheikh ilikuwa sehemu ya Ilani ya Chadema.

“Tangu uchaguzi umalizike ni miaka miwili sasa imepita na Masheikh bado wako mahabusu. Chama kinamuunga mkono Lowassa, ni uchunguzi gani usiokamilika kwa miaka minne? Ma- DCI wengi wameondoka, Ma- IGP wengi wameondoka,” alisema Mbowe.

Alisema Chadema itaendelea kupaza sauti na asitokee mtu wa kuwaziba mdomo hadi pale haki itakapopatikana dhidi ya viongozi hao wa kidini.

Azungumzia ya Kibiti Kadhalika, Mbowe alisema Chadema inasitishwa na matukio ya mauaji yanayotokea katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani na kwamba hawaungi mkono, lakini wanasikitika namna Serikali inavyoshughulikia suala hilo.

Mbowe alisema Serikali inapaswa kuacha majigambo bali busara itumike zaidi katika kutokomeza mauaji mkoani Pwani.

“Kauli za majigambo yanachochea mauaji, viongozi wa kisiasa waache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi. Nguvu haisaidii, busara zitumike, wazee watumike, viongozi wa dini watumike, ‘Resistance by collaboration’ itumike kwa kushirikiana na wananchi,” alisema Mbowe.

Kadhalika, Mbowe alisema Serikali inapaswa kubadilisha mbinu ya kupambana na wauaji hao na kuacha vitendo vya kuwakamata wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) na kuwatesa ili wawataje wahusika.

Alisema akiwa kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amepelekewa malalamiko kutoka kwa wabunge wa CUF kuwa askari wamekuwa wakiwatesa wanachama wa chama hicho.
 
Tupo tupo tunasubiria mkutano uanze

19420693_875516032616308_8792731192522403680_n.jpg
 
ukiona mambo yanaenda kwa vitisho namna hiyo ujue demokrasia hapi na ni dalili ya uogo wa kusema kweli
 
Utashangaa utasikia wanaongelea kuhusu kauli ya Mzee Mwinyi aliyoitoa kwenye sherehe ya Eid El Fitri kuhusu Rais Magufuli kutawala miaka yote kama sio matakwa ya katiba.

Badala ya kutafuta mbinu za kumshinda Rais Magufuli kwenye sanduku la kura, wao wanahangaika na kauli za wanaCCM.

Kauli za wanaCCM haziwezi kuwa ni kauli za watanzania wote labda kama wapinzani wanafahamu hawawezi kushinda Uchaguzi Mkuu 2020.

In fact, wapinzani kuhangaika na kauli za wanaCCM kuhusu Rais Magufuli kutawala ''milele'' ni dharau kwa upinzani.
 
2020 CHADEMA watachezewa kama alivyo chezewa fisadi Jamal Malinzi kama watamsimamisha mgombea urais Lowassa kesi ya Richmond itaanza upya na TAKUKURU watamshikilia Lowassa....

Kwa hiyo unawashauri wasimsimamishe Lowassa ? Kwa nini Takukuru wangojee hadi Lowassa awe mgombea badala ya kumkamata sasa hivi kama ushahidi upo ? Kumbe Malinzi kachezewa game I thought ni takukuru kuwa kazini kama kawaida ?
 
Utashangaa utasikia wanaongelea kuhusu kauli ya Mzee Mwinyi aliyoitoa kwenye sherehe ya Eid El Fitri kuhusu Rais Magufuli kutawala miaka yote kama sio matakwa ya katiba.

Badala ya kutafuta mbinu za kumshinda Rais Magufuli kwenye sanduku la kura, wao wanahangaika na kauli za wanaCCM.

Kauli za wanaCCM haziwezi kuwa ni kauli za watanzania wote labda kama wapinzani wanafahamu hawawezi kushinda Uchaguzi Mkuu 2020.

In fact, wapinzani kuhangaika na kauli za wanaCCM kuhusu Rais Magufuli kutawala ''milele'' ni dharau kwa upinzani.


Kwenye Free and Fair election iko wazi kwamba kuna mtu anaweza kushangazwa ndiyo maana hata Tume huru ya Uchaguzi ni issue kupatikana bara . Kwa anaye bishana juu ya hili basi ashauri mambo 2 yawe sawa
1. Mgombe huru
2.Tume huru ya Uchaguzi .
 
2020 CHADEMA watachezewa kama alivyo chezewa fisadi Jamal Malinzi kama watamsimamisha mgombea urais Lowassa kesi ya Richmond itaanza upya na TAKUKURU watamshikilia Lowassa....
Hiyo ni sera mpya, maana KGM alitumia mitandao kumdhalilisha mpinzani wake huku kwao. Hapa tunatumia Polisi, JW nk kujaribu kuwafunga midomo wapinzani.
 
Back
Top Bottom