Mbowe,mrema,mbatia na maalim seif wanasumbuliwa na ulevi wa madaraka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe,mrema,mbatia na maalim seif wanasumbuliwa na ulevi wa madaraka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Dec 17, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Upepo wa Kuondoa viongozi mangi meza wa vyama sasa unaonekana kupamba moto. Ni dhahili kumekua na Udikiteta na Umangi meza wa kutaka kuongoza vyama vya siasa bila kikomo kwa kisingizio eti wao ndio waanzilishi wa vyama hivyo! Mrema mwaka jana amepambana na kumfukuza Katibu wake akikaataa mtu yoyote asiwe na sauti,hali kadhalika Mh Mbowe amekua na utawala wa mabavu kutaka sauti yake iwe ndio sauti ya mwisho kwa maamuzi kisa yeye ndie alie anzisha Chadema! ikumbukwe uchaguzi wa mwenyekiti ndani ya Chadema Mbowe alifanya kila hila ili aendelee kuwa Mwenyekiti wa Chadema kisa yeye ndie mwanzilishi wa Chadema! Hali kama hiyo imehamia sasa NCCR-Mageuzi na CUF ambako nako kuna sumu ile ile ya Udikteta ikiendelea kwa Viongozi hao wa wakuu wa vyama hivyo kuendeleza umimi! Kinacho onekana Chadema ni uvumilivu tu wa watu wenye busara kumvumilia mmliki huyo wa Chadema aendelee kuwa na sauti,lakini muda si mrefu atalazimika kupisha na kuacha kuonesha mabavu ya wazi eti kisa yeye ndie mwazilishi wa Chadema,sitaki kuongea mifano mingi hasa ya mbowe lakini ikumbukwe habari ya kukiuzia Chama magari mabovu kwa milioni 500,na wajumbe wa kamati kuu ya Chadema wataunga mkono hoja hii kuwa Mwenyekiti huyo asome alama za nyakati sasa. Upande wa Mbatia amekua kiongozi alie kosa aibu na hana busara kwani hataki kukosolewa kabisa na mtu yoyote,sababu kubwa yeye ndie mwanzilishi wa Chama. Upande wa CUF chama hicho kimepauka kimtizamo ndani ya Zanzibar na hata Bara kwa kukosa ushawishi,lakini kikubwa ni ndugu Maalim Seif Kuhodhi madaraka! Sababu ni ile ile ya kijinga eti yeye ndie mwanzilishi wa Chama.

  My take: ​
  Viongozi hawa wa vyama vya siasa ni lazima wajue na waelewe kuwa huu si wa kati wa kuendesha vyama kwa misingi ya kikampuni,ni bora wajue kua kuna wanachama wao ambao wana upeo mkubwa,maono ya mbali,shupavu na wana nia njema ya kuvipa nguvu na mtizamo mpya vyama hivyo,kama mtu anaona ana hati miliki ya chama basi atoe hesabu ya gharama zake ili arudishiwe na chama kisonge mbele na kuwe na demokrasia ndani ya vyama na ustawi mzuri wa vyama.
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The domineering tendency of many political organisations heads is not entirely happening by accident but chiefly attributed to exploitative leadership system which also has been exhibited by the governing CCM itself. And at large has something to do with the antiquated national constitution which gives immoderate powers to the head of state who is literally the last say in almost anything calling for the government attention. So what currently happens in the opposition is essentially a corollary to failure to put in place provisions in a constitution that would serve to draw the line at responsibilities assigned to party's heads. Therefore to preclude these needless contentions from ever resurge in a future we have to resort to the massive overhauling of the constitution by instituting certain laws that will limit party leaders powers so that much decisions to be executed at the level of the lower committees.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  njaa inakusumbua
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mbowe sio mwanzilishi wa chadema naomba ukajipange upya,na kwanza ukiniambia CCM ndo wameng'ang'ania madaraka hapo ndo kila mtu atakuelewa,maana CCM magamba wamejificha kwenye mgongo wa katiba inayompa raisi madara makubwa ya kufanya mambo yenye maslahi ya chama na yeye,kama tume ya uchaguzi ambayo ndo inatumika kuendeleza utawala wa CCM.
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  mbowe hana njaa kama hao wengine ambao pia wapo kwa maslahi yao binafsi na ni mawakala wa ccm A..period
   
 6. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  We hata ulichokiandika ukielewi,mbowe ni muanzilishi wa CHEDEMA?who told you?na edwin mtei?unajua hata katiba ya chadema inasemaje?huu ni mwaka wa ngapi mbowe kushikilia uenyekiti wa chadema taifa?nenda katawaze ukalale
   
 7. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona umezunguka lakini lengo lako lilikuwa ni kumpiga madongo mh mbowe huna lolote njaa tu inakusumbua. Ila kumbuka ccm mwaka jana walivyomfanya Shibuda bahada ya kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya ccm.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tunadai demokrasia ku[pitia vyama vingi lakini ndani ya vyama vyenmyewe hakuna demokrasia na kweli. lakini huu ni mwanzo, tutafika tu
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Unaharisha?
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ulichosema ni ukweli mtupu!
   
 11. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzee Mtei kakabidhi Chama kwa mume wa Mtoto wake! Kaazi kweli kweli!
   
 12. L

  Lowasa Namkubali Member

  #12
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui zito angekuwepo kwenye JF angetusaidia utata huu ambao wakati mwingine unaonekana kuwatafuna wanasiasa wengi wanaonyesha nia ya kugombea nafasi yoyote ya ndani ya chama na wakati mwingine hata ya mwenyekiti wa mtaa,kitongoji,kijiji,udiwani,ubunge, na hasa urais haya yapo.lakini kibaya zaidi wale walioko katika madaraka huwa wananafasi ya kuandika historia na kuwaacha wale walio nje ya madaraka wenye nia ya kugombea nafasi zao wakiwa waathirika wakubwa.ILA KWA LOWASA WATAGONGA MWAMBA NI MWANASIASA ANAYETAAMBA NA MAZINGIRA YA HALI HALISI KWA HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYE THIBITISHA UDHAIFU WAKE NA UWEZO WAKE KUONEKANA HAFAI VINAVYOTAWALA NI KASHFA,MATUSI,TUHUMA N.K ahsante
   
 13. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naheshimu uhuru wa kutoa maoni lakini hii taarifa haijakaa sawa itakuwa vema kama ingerekebishwa ili kuondoa upotoshwaji, pia ingependeza sana kama ungeandika kuhusu pande zote yaani tawala na upinzan hali zikoje hapo ungekuwa umefanya analysis nzuri ambayo haipobaised.
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,591
  Likes Received: 4,702
  Trophy Points: 280
  Wa mrengo wa Cameron mnajuana kweli na kupigana tafu.
   
 15. damper

  damper JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kuondoa msuguano mi nigeshauri hawa waanzilishi wa vyama wanapotengeneza katiba za vyama vyao wasiweke ukomo wa kuwa madarakani kwa mwanzilishi wa chama mpaka pale atakapotosheka ang'atuke taratibuuuuuuuu. "eti mi nihangaike kuunda chama halafu leo aje mtu tena amefukuzwa huko kwa ajili ya kutaka madaraka, alete mgogoro ndani ya chama nilicho kianzisha tena kwa pesa yangu binafsi, haiwezekani"
   
 16. L

  Luiz JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli umekulupuka nenda ukawambie waliokutuma kuwa nimewakosea sana watu wa humu jamvini kwa kuanza na NCCR & CDM mbatia na mbowe sio wanzalishi wa vyama vyao pili unaonekana unatumika sana na chama tawala kuja kuvuluga upinzani. Huu usulutani nenda ccm waliokutuma ukakosoe maana viongozi wote walioko huku ni ulithi toka kwa mababu zao hapo ndio utaona ulivyotumika vibaya.
   
 17. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wwe wala usitusumbue,huna lengo lolote na mbatia,seif wala tlp(mrema),ulizunguka tu ili upate angalau cha kuongea dhidi ya cdm na mwenyekiti wake.Cha kukusaidia naona hii cdm itakuua na presha bure,kawambie tu magamba wenzio kuwa hiyo kazi ya ujira mdogo waliyokupa ya kuichafua cdm imekushinda.
   
 18. k

  kimalando Senior Member

  #18
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakushauri mtoa mada ubadilishe topic yako maana naona umeorodhesha majina mengi lakini mashambulizi mengi ni kwa Mbowe. Just srike to the target hakuna haja ya kuweka majina mengi ili usionekane una upendeleo.
   
Loading...