Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Kutokana na hali ilivyo huenda CHADEMA ikakosa Mbunge ambaye ni kiongozi Mkuu katika chama kwani Mbowe ambaye ni Mwenyekiti nafasi yake kurudi bungeni ni finyu mno kwani Wananchi wa Hai wameshamtaka akabidhi Jimbo.
Kwa upande wa Mnyika yeye alishasoma alama za nyakati akaamua kujitoa kugombea ubunge, Tundu ambaye ni makamu mwenyekiti yeye amechagua kushiriki kugombea urais huku akijua hashindi. Salum Mwalim ambaye ni kiongozi kwa upande wa Zanzibar anashiriki kwenye uchaguzi kama mgombea mwenza wa Tundu Lissu.
Ni dhahiri hao wote baada ya uchaguzi wataishi kwa kutegemea posho kutoka chamani hapa ndipo patachimbika na ukizingatia ruzuku inaenda kupungua.
Wasipo kuwa wavumilivu tutegemee watu kugawana mbao.