Mbowe, mkanye Lissu

Anajipiga spana mwenyewe! Sisi watanzania tutampiga spana nyingine 2025 chini ya Jemedari mama samia!
Jemedari kishakuwa mama samia tena! Siyo kile chuma mlichotwambia? Kwani imekuwaje kwa Chuma hicho! Jiwe! Nini kimetokea kwa hyo mtu mliyetuaminisha kama ni MUNGU vile?
 
Ukiacha uana harakati wake ukiacha u siasa wake lakini

lissu kasahau kabisa kuwa yeye ni BABA mwenye familia

anachokiandika huko mitandaoni watu wana screenshot tu

hizi screenshot watu watazi re-post itakapotokea Nae yakimfika

watanzania huwezi waelewa ukifanya upumbavu,wanakusubiri ujae kwenye 18 zao

Lissu hilo bado hajifunzi na hataki kujifunza,ni sawa ndio alivyoamua ila akumbuke yeye ni BABA.
 
Wewe nawe ulisherehekea kifo Cha JPM??...tuanzie hapo Kwanza...
Ujinga imekutawala kabisa; kwani Magufuli ni nani adi watu wasisherekee akifa? ni propaganda tu ndo inawasumbua ili mpate chochote kutoka kwa Samia.
 
Wengi mnamlaumu lissu kwasababu na kuto kut
Sema ana jua hawezi kuja kua Rais kashajikatia tamaaata reaction kwenye post zake sio nyingi san
Wengi mnamlaumu lisu ni kwa sababu ya kukosa maarifa na ubinafsi , hata ungekuwa wewe usingeweza kumpenda mtu aliye dhamiria kukuuwa akakukosa ila kakuachia kilema cha maisha eti kisa tu unaeleza madhaifu yake ,

Na hakika hata wewe usinge weza kumpenda mtu huyo , mzigo alio nao lissu moyoni kuhusu JPM yeye mwenyewe ndiye anaye jua, wengine mnaongea ongea sana sababu hamuujui mzigo na mateso aliyo yapitia chini ya utawala huu na kilema cha maisha baada ya dhamira ya kuuliwa kufeli

hata mimi siwez kuwa mnafiki ni haki yake lissu kuto mpenda magufuli mimi simlaumu.
 
Ukiwasikiliza watu wa kibiti walopoteza wapendwa wao ktk utawala wake huu.

ukiwasikiliza ndugu wa akina ben saa8, ndg wa akwilina, ndg wa azory, kangoye na wengine ndg wa walokuwa wakiokotwa coco beach ktk sandarusi, pia nduguze tundulisu aliyemiminiwa risasi 32 immediate baada ya raisi ktk kikao kudai kuwa watu wanaompinga ktk vita ya kulinda madini ni lzm kuuwawa sincerely watakuombea mabaya na kukulaumu kwa kuandika ugoro ulochanganywa na Mavi as if hujawai kufiwa au kuuguza.

Wape watu uhuru to celebrate.
Vaa uhusika wake na upigwe risasi 16, uvuliwe ubunge, unyimwe stahiki zako zilizopo kikatiba!!!. Bado mwenye mamlaka hakuguswa na lolote kuhusu yeye afu unataka ahuzunike na nini kuhusu yeye?? Tunaolia ni sisi tusiojua ubaya wa marehemu tuendelee kumlilia ila sio tulazimishe vilio nyeti viwe vya kila mtu.
Ivi alipigwa risasi ngapi?

16 au 32!!!??
 
Alaaniwe yeyote aliyehusika kuondoa Umoja na Mshikamano wetu Watanzania.

Mtu anapigwa Risasi, wengine wanashangilia

Mtu anafariki, wengine wanachinja Kuku na kufanya sherehe.

Bila hili kurekebishwa mapema, ikitokea Vita kama ile ya Uganda 1978 - 1979 nahisi kuna watu wata side na Uganda ili tupigwe na kushindwa Vita.

Mungu wa Rehema awasaidie Viongozi wetu kubaini Ufa huu na kuwapa maarifa ya kuweza kupatanisha pande hizi hasimu ili Watanzania tuishi kwa upendo na kupendana na kuendelea kuwa wamoja.

Maandiko yanasema " Heri wapatanishi kwa maana wataitwa wana wa Mungu" pia Maandiko yanasema Samehe saba mara sabini.
Let's be one forever
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Tundu lissu kasema nini mkuu? Maana navyomjua Tundu Lisuu akisema jambo lazima liwe na mantiki, Hawezi kubwabwaja tu kama RC Chalamila.
 
Ukipata taarifa za mtu aliyekosa kukuua mara kadhaa, haiwezi kuwa habari ya huzuni bali ni HABARI NJEMA.
Lisu naye ni binadamu kama ulivyo wewe, tena sikuwahi kukusikia ukinena mema juu ya IDD AMIN DADA wa Uganda, na hapo napata mashaka juu ya uwezo wako wa kufikiri
 
Pamoja na kwamba tupo msibani kuomboleza kifo cha mwanaAfrika na Mwanamajumui Hayati John Pombe Magufuli, imenilazimu kuhoji huyu ndiye Mh Lisu Wakili msomi aliyetaka kuwa Rais wetu 2020?

Nimesoma Twitter zake na maandiko yake mbalimbali baada ya msiba wa JPM. Nikajiuliza hivi huyu ndiye alipaswa kuwa Rais? Kwa tamaduni, mila na desturi za kitanzania na Afrika kwa ujumla si sawa kushangilia kifo hata Kama mtu alikuwa humpendi kwa kiwango chochote. Haturuhusu kumhukumu Marehemu, Mungu ndiye mwenye uwezo huo.

Tusiandike kama hatujawahi kufiwa au Kama sisi hatutakufa. Kila mtu duniani atakufa na atakufa kwa stahili yake. Kipindi hiki ambacho ndugu jamaa na rafiki wanapopitia kipindi kigumu sisi sote tunapaswa kuwafariji kwa kuwa hakuna anayejua kesho yake.

Nimpongeze Mh Mbowe ambaye statement yake inaonesha namna alivyoiva na anavyothamini uhai. Mh Mbowe ameonyesha nguvu yake ya maarifa na uhodari wa kuchambua maneno kulingana na mkutadha. Kwa mazingira haya simuoni mtu wa kuvaa viatu vya Mh Mbowe Kama mh Lisu ambaye nilidhani ni matured naye anaweza kuandika vitu vya kitoto ambavyo walau vingeandikwa na BAVICHA.

Tunatambua Lisu alipigwa na kuumizwa, lakini tunamshukuru Mungu mwingi wa rehema alimponya na sasa yupo hai, lakini kitendo cha kupona kwake hakiondoi ubinadamu na kupandikiza umbumbumbu kwenye argument na reasoning.

Lakini pia hii ni indicator kwenu CHADEMA Kama munadhani Lissu will be a good candidate for 2025, basi aingie darasani kwa mzee Mbowe kujifunza hekima na kuchambua mambo kabla ya pablicity.
Mlitukaririsha nyimbo kwamba Iddi Amin akifa sisi hatuwezi kulia, tutamtupa Kagera awe chakula cha Mamba.
Sasa Leo kafa Iddi Amin wa Tanzania mnataka watu walie?
 
Ni wapi mila za afrika zilisema watu washangilie mtu kuuawa
Pamoja na kwamba tupo msibani kuomboleza kifo cha mwanaAfrika na Mwanamajumui Hayati John Pombe Magufuli, imenilazimu kuhoji huyu ndiye Mh Lisu Wakili msomi aliyetaka kuwa Rais wetu 2020?

Nimesoma Twitter zake na maandiko yake mbalimbali baada ya msiba wa JPM. Nikajiuliza hivi huyu ndiye alipaswa kuwa Rais? Kwa tamaduni, mila na desturi za kitanzania na Afrika kwa ujumla si sawa kushangilia kifo hata Kama mtu alikuwa humpendi kwa kiwango chochote. Haturuhusu kumhukumu Marehemu, Mungu ndiye mwenye uwezo huo.

Tusiandike kama hatujawahi kufiwa au Kama sisi hatutakufa. Kila mtu duniani atakufa na atakufa kwa stahili yake. Kipindi hiki ambacho ndugu jamaa na rafiki wanapopitia kipindi kigumu sisi sote tunapaswa kuwafariji kwa kuwa hakuna anayejua kesho yake.

Nimpongeze Mh Mbowe ambaye statement yake inaonesha namna alivyoiva na anavyothamini uhai. Mh Mbowe ameonyesha nguvu yake ya maarifa na uhodari wa kuchambua maneno kulingana na mkutadha. Kwa mazingira haya simuoni mtu wa kuvaa viatu vya Mh Mbowe Kama mh Lisu ambaye nilidhani ni matured naye anaweza kuandika vitu vya kitoto ambavyo walau vingeandikwa na BAVICHA.

Tunatambua Lisu alipigwa na kuumizwa, lakini tunamshukuru Mungu mwingi wa rehema alimponya na sasa yupo hai, lakini kitendo cha kupona kwake hakiondoi ubinadamu na kupandikiza umbumbumbu kwenye argument na reasoning.

Lakini pia hii ni indicator kwenu CHADEMA Kama munadhani Lissu will be a good candidate for 2025, basi aingie darasani kwa mzee Mbowe kujifunza hekima na kuchambua mambo kabla ya pablicity.
 
Tulieni Lissu awanyooshe na yeye ni binadamu atoe machungu yake moyoni,huu msiba usiwafanye mna huruma sana
Msiba wa jirani ni wetu sote kama alikuwa jirani mwema vinginevyo ni wao hukohuko na yeyote anayejaribu kulazimisha watu wahudhurue kwa wingi matokeo yake ndio hayo yanaongeza misiba na machungu.
 
kama ni kweli Mungu kamlipia Tundu lissu sasa yeye anahangaika na nini???
No ukweli wazi asingeweza kabisa kumfanya lolote Hayati...
Ni kweli watanzania Wala mabeberu hata mmoja aliyemsaidia....
If so why he keep insult people especially marehemu??
Akae akijua Mungu Hana upendeleo kama alimuadhibu Meko basi atamuazibu na yeye Kama atafanya upuuzi arejee kisa Cha Musa alipopewa adhabu ya kifo baada ya kukiuka maagizo ya Mungu, hivyo mumshauri asipotoke.
Meko kafa huku Lissu (aliyekuwa amepangiwa na kina farao afe) bado yu hai. Huyo ndiye Mungu!
 
Alivyoshambuliwa kwa maelekezo zile risasi 38 huku jeshi la Polisi likikataza hata kumuombea dua ulikuwa uko wapi ?
Risasi, risasi mpaka lini? unapigwa risasi tukiwa watoto hadi tunapata umri wa kupiga kura, wewe bado unasimulia risasi! Kila siku kulia-lia tu! Mbona Ulimboka hatusikii akilia-lia na mkasa wa kutaka kuuwawa? Mandela je?

Hao ndo wakomavu! Hakuna kusimulia mambo ya kifungo, ni uimara wa akili na kuwa President. Hiyo akili ya Lissu ya kutaja risasi kila siku kwa miaka ya uhai wake haituoneshi uimara wa akili anayestahili kuwa President. Yeye ni mtu wa mitaani tu, akitafuta kulipiza kisasi.
 
Back
Top Bottom