Mbowe mgeni rasmi uzinduzi wa kampeni za CDM arumeru

Ni upotezaji tu wa pesa hata kanuni za kutafuta soko zinataka kampeni ya kutafuta wateja ulenge wateja husika.Uchaguzi unafanyika arumeru unahutubia taifa hiki nini nini kama si kupoteza pesa tu ilibidi Chadema ilenge Arumeru tu.

Pili nakumbuka niliwahi kukutana na Kiongozi mmoja mwanamizi wa CCM mahali nikamuuliza kwa nini CCM waligoma Mgombea Uraisi wa CCM asifanye mdahalo na wagombea uraisi wengine kwenye TV ili watu wawapime na wawahoji live akasema uzoefu wake wa kisiasa watu wenye TV ni watu wenye maisha mazuri na wengi wao huwa hawaendi kupiga kura. Hawapendi kushinda juani kwenye mistari kusubiri wapige kura hivyo si kundi kubwa la maana la kukusaidia ushinde akasema sisi tunaenda vijijini ma-tv tunawaachia vyama vya upinzani wanaozura mijini na matajiri wao wasiopiga kura wanaowalenga.Hatuwezi kumwanika mgombea wetu kwenye TV ashambuliwe na maprofesa na wasomi wachache walioshiba wenye nyumba zenye A/C ,Feni na TV ambao kazi yao kuzomea au kushangilia lakini kwenye kura hawaendi.Akasema CCM wako makini kutumia pesa kwenye kampeni.

Arumeru wenye TV na radio na muda wa kusikiliza hizo TV na Radio majumbani ni wachache mno na hawana muda kufuatana na aina ya maisha ya watu wa Arumeru.Ni upotezaji tu wa hela.Anyway ngoja tusikilize hiyo hotuba kwa Taifa badala ya hotuba kwa Arumeru.
Ushauri wa enzi za mawe, rais anapoongea na wazee wa Dar kwa ajili ya masuala ya madaktari kwani hao wazee ni madaktari? ile ni njia mojawapo ya kufikishia ujumbe lakini target ni madaktari. Hata Mh. Mbowe kesho kuongea na taifa kupitia kampeni ni njia hiyo hiyo, hata hivyo lengo lake si kupata kura za AM tu lakini pia kukitangaza chama na kuuza sera za chama kwa watanzania wengi zaidi.
 
harakati za mbowe kunyang'anya dr.slaa nafasi ya kugombea urais 2015 zinaendelea. Kazi ipo
 
Kesho kuanzia saa tisa kamili shilika la umeme litazima mitambo yake nchi zima kwa ajili ya kukata matawi ya miti yaliyo karibu na nyaya za umeme, zoezi hilo litachukua takribani saa moja na nusu.
Hahahahahaaa......ngoja nimtume kijana akanunue kabisa mafuta ya jenereta, isije ikafika kesho tukaambiwa na vituo vyote vya mafuta vimefungwa kwa kukosa umeme/mafuta. Asante kwa kunikumbusha
 
[h=2]Friday, March 9, 2012[/h][h=3]MH. FREEMAN MBOWE KUHUTUBIA TAIFA KESHO..[/h]


Katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa kambi rasmi bungeni, atalihutubia taifa kesho.

Hotuba hiyo itarushwa LIVE na STAR TV, RADIO SUNRISE na RADIO JM.
Katika siku ya uzinduzi wa kampeni.

Watanzania wote wanaombwa kutazama Star tv kusikiliza hotuba hiyo yenye mustakabali wa Taifa letu.
 
angalau tutaona na kusikia hotuba nzuri baada ya mda mrefu. Mbowe Mungu akulinde tu
 
Back
Top Bottom