Mbowe: Mbunge na Madiwani walioapa hawakutenda jinai, ila ni wakaidi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema Madiwani na Mbunge mmoja wa CHADEMA, ambao wameapa baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020 hawajatenda jinai.

Lakini amesema viongozi hao wamekaidi misimamo ya chama, hivyo chama kitatenda haki kwa kuwasikiliza kila mmoja wao kabla ya kuchukua uamuzi stahiki kwa muda muafaka.

Pia kuhusu wabunge 19 wa viti maalum amesema vikao maalumu vya chama vitakaa kusikiliza rufaa ya wabunge hao walifutwa uanachama na nyadhifa zao zote.

Mbowe ameyazungumza hayo jana katika mkutano wake na waandishi.
 
Back
Top Bottom