Mbowe mbaroni akidaiwa kutoa maneno yanayoashiria uchochezi, kuamsha hisia na chuki dhidi ya Serikali na Polisi. Aachiwa kwa dhamana

Asubuhi kabla sijaenda kanisani dhamiri yangu inanituma nijadili hili alilotewa Mhe. Mbowe kule Hai.

Hivi Kiongozi kama Mbowe, mtu mstaarabu, mtu mvumilivu alipaswa kutendewa kihuni vile tena Askari Polisi wetu?

Hivi mpaka mnafanya mambo yale ya kihuni mlimchukulia Mbowe kama jambazi au?

Askari mambo hayo mtendayo ni chukizo na yanaleta chuki katika jamii ya Kitanzania na hayana afya kwa taifa.

Binafsi kitendo kile kilinikumbusha matendo mabaya ya Askari wa makaburu dhidi ya raia kule Afrika Kusini na nchi ikawa mstari wa mbele kupinga matendo yale.

Leo sisi kutenda kama makaburu ni AIBU KUBWA SANA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi Kuna askari weledi
 
Hao tunaowaita polisi wala si polisi, ni kundi la majambazi waliopewa mafunzo na silaha kisha tunawaita polisi.

Polisi ni lazima wawe wakwanza kutii sheria, na kisha kuwaongoza wananchi kutii sheria. Kinyume na hapo tunawaona majambazi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati huwa najiuliza maswali mengi juu ya polisi wetu,naishia kusikitika tu.
 
Dah huu upumbavu utaendelea mpka lini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sehemu kubwa ya viongozi wa polis ni makada wa ccm

Hawa Polisi wa Magufuli wakiongozwa na kichaa mwenzao Ziro wanastahili hukumu ya Umma! Alichofanyiwa Mhe.Mbowe(MB),Mwenyekiti CHADEMA(T) na Kiongozi Kambi Rasmi ya Bungeni(KUB) ni UNYAMA,UKABURU,USHENZI na UDHALILSHAJI mkubwa...!
Nilitegemea Ziro au Simbachawene wakemee huu USHENZI hadharani na wamwombe radhi Mhe.Mbowe.....!
 
Kazi ya polisi ni kutii maagizo na sio kuhoji sasa mwanasiasa akikosa busara lazima jamii itaumia
 
Siku nyingine Mbowe akiwa na mkutano awaruhusu Polisi ndiyo wawe wahutubiaji kwenye mikutano hiyo. Wapuuzi kweli .
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom