Mbowe, mashambulizi dhidi ya Mwigulu Nchemba kwa memo hii kulikoni?

manieno makali yako wapi kwenye hiyo memo?!! tena amemuita kwa heshima sana na kwa utaratibu sana...na amemuonya juu ya tabia yake ya uongo!!!
 
ungefanya la maana sana kama kila memo utakayo ileta hapa iambatane na memo za majibu la sivyo haya ni majungu tu. tafuta kazi nyingine
 
Watawala wanatafuta njia ya kuendelea kutawala kwa kuwachafua wale wenye nguvu ya umma. Cha ajabu ni kuwa impact ya haya mambo yanatokea katika level ya juu tu. HuKu uswazi kwetu watu wanaamini kila baya linalosemwa dhidi ya wapinzani ni mpango mahsusi kuwachafua. Sasa sijui ni nani atawasikiliza watawala ambao ni waongo wa kutupwa wanaoendesha nchi kwa propaganda zisizotatua matatizo yetu:yawn:. Kifupi ni kwamba wazee wa mabwepande watafute njia nyingine zaidi ya kashfa za kufoji kwani huku mtaani hatuamini neno kutoka kwenu. HUO NDO UKWELI NA KWELI TUPU!
 
Mama porojo

Kwani hiyo memo ina tatizo gani? Mwingulu anamchangia Mbowe kiasi gani kusomesha watoto wake? Maneno ya Nchemba ni ya mfa maji.
 
Very fair allet!. Kwanza mwingine angeanza na tusi na kumaliza na tusi.
 
Jamani msishangae kutukanwa,kukejeliwa na kushambuliwa pale utakaposema ukweli kuhusu chadema na viongozi wake, wanaofanya kazi hiyo ni vijana wa chadema wasiojitambua wako pale makao makuu ni kikosi kazi kinaongozwa na Mnyika hawa vijana wanapewa Posho kwa kazi ya kuitetea chadema na kuisemea mazuri mitandaoni wakati huo huo wanaishambulia CCM na serikali yale lendo kuui kuidhoofisha kwa wananchi ili waichukie na kuja kuipa madaraka ya utawla chadema yani wanapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya CCM na serikali yake usifikiri wako vijana wengi hapana ni vijana wachache wanejisajili kwa IDs tofauti tofauti hiyo ndiyo chadema yenye mikakati michafu ya kushika dola ukionganisha na ule mkakati wa kushawishi,kudhamini na kuchochea migomo na fujo zote hapa nchini kwa Madaktari,Wanafunzi vyuoni na walimu! SHAME ON U CHADEMA Kwa mbinu chafu zinazoumiza watanzania!
 
WANAJF.kwanza niombe radhi kupost sehemu ambayo si sahihi kwani nimeshindwa kupost kama post mpya.nia yangu nikupata kutoa kero yangu na kuwaomba watu ambao wanaweza kutusaidia sisi walimu tulioajiriwa kama walimu wa lesen.kwani tulikuwa tunalipwa 80% ya mshahara wa diploma na bila makato yeyote kama sheria zinavyo sema.lakini cha ajabu serikali imeamua kutukata tunaombeni msaada wenu.najua kuna watu wengi ambao watakuwa na uelewa na hili suala hasa tunawaomc wabunge watusaidie katika kipindi hichi cha bajeti ya wizara ya elimu.pia tunapojiendeleza uzoefu wetu kazini hauzingatiwi.tunahitaji msaada wenu.
Okay, JF senior member!! ukitaka kupost uzi mpya, nenda sehemu inayoitwa home bofya hapo then utaona vitengo tofauti tofauti kama jukwaa la siasa nk, chagua unaloona linakufaa bofya hapo, then kwa chini kabla ya maada kuna sehemu inaonyesha "post a new thread" utaweza kuturushia hii maada. kama nimekosea maelezo mnisaidie wakuu.
 
Watawala wanatafuta njia ya kuendelea kutawala kwa kuwachafua wale wenye nguvu ya umma. Cha ajabu ni kuwa impact ya haya mambo yanatokea katika level ya juu tu. HuKu uswazi kwetu watu wanaamini kila baya linalosemwa dhidi ya wapinzani ni mpango mahsusi kuwachafua.....

Mkuu,

CCM kweli imechoka.

Silaha zao wanazotumia zimechuja....kila mtu anajua kuwa ni propaganda....lakini hawabadili mbinu!!

Ni chama mfu!

Mbinu hii wanayotumia nashangaa hata Anna makinda nea anaitumi!

Hivi kweli hawajajua kuwa mbinu imeshtukiwa na watz wote wanaotaka mabadiliko!!
 

My take: vita ya maneno makali ndani yabunge yanatupeleka wapi kisiasa?

Je kuandikiana vi-memo na kutupiana manenomakali mbungeni kuna athari za moja kwa moja na kutupiana maneno makali kwenye majukwaa ya kisiasa nje ya mbunge?

Je hakuna athari za mauaji ya kisiasa yanayotokea katika uwanja wa siasa nchini?

Nini kifanyike kuondoa hali hii????????

vita ya maneno makali ndani ya bunge yanatupeleka wapi kisiasa?

Yanatupeleka kubaini Pumba na mchele

Je kuandikiana vi-memo na kutupiana maneno makali mbungeni kuna athari za moja kwa moja na kutupiana maneno makali kwenye majukwaa ya kisiasa nje ya mbunge?

Ndio na bado ukali hautoshi, ukali ni ukweli unapowekwa bayana po pote; HAKUNA SULUHU

Je hakuna athari za mauaji ya kisiasa yanayotokea katika uwanja wa siasa nchini?

Mauaji yanayoendeshwa na CCM kisiasa ni mengi yamekithiri, ila wanabambikiwa wengine. Bahati mbaya Mungu halali na ukweli haufichiki.

Nini kifanyike kuondoa hali hii???????


CCM ikubali matakwa ya wananchi IONDOKE madaraka salama
 
Huyu Mwigulu ni mtu mdogo sana Tanzania,anatafuta cheap popularity kwa umbea na kujifanya mjuaji.Dunia ya leo ujuaji na ubabe havina tena nafasi,kinachotakiwa ni kujenga hoja na kuwa upeo mpana wa kuona mambo.Ajitahidi kuacha majungu na siasa uchwara za mitaani.
 
Ndugu zangu,

Unaweza kukaa kimya kwa muda mrefu ukiangalia 'mpambano' hatimaye uzalendo ukakushinda na ukaona bora upaze sauti yako kufafanua mtafaruku.

Nimesoma sms za kifo cha Nchemba; nazinukuu,

1. 'Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatuzonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya ccm milele? Utajutia kimbelembele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini hata kama kweli kwa nini kututia aibu? Hata ufanyeje 2015 tunaingia ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?'

2. 'Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja'

3. 'Fahari yako itageuka kilio kwako. Utatutambua'

SOURCE: Tanzania Daima July 17, 2012.


Nitachambua sms zote kwa kadri ya mtazamo wangu.

Ujumbe wa kwanza hauna mantiki isipokuwa kukumbusha mambo yasiyofahamika hata leo. Unaposema 'unatuzonga' napata shida kuamini kwamba huo mi mzongo wa hoja maridhawa ama mzongo wa ubishi na hoja mfu, ilimradi makelele tu. Kwa mtu kujiamini hilo ni sawa, lakini kujiamini kwa mtu hakuwezi kumsababishia usumbufu wowote mtu mwingine kwa kuwa wote tunaendeshwa na akili zetu. Kuiacha hisia ifanye kazi bila kuwa na coordination baina ya ubongo na mdomo yaani coding unaweza kujikuta unaongea vituko sana mbele ya wenzio na ukaambulia kuvuna aibu.

Ukabila unaodaiwa kwenye sms ya 1 hauna uthibitisho kwa kuwa kwanza baadhi ya senior figures CDM sio wa kaskazini, lakini pia CDM imeandikishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kama Political Party na sio chama cha wachagga ama wanyamwezi. Kama kuna mwenye uhakika kwamba CDM ni chama cha Wanyamwezi basi awasilishe kwa Tendwa ili CDM kichukuliwe hatua stahili akiwemo Tendwa mwenyewe kwa kuruhusu ukabila utinge Bungeni. Hakuna hata kada mmoja wa CDM anayeweza kuandika akitetea ukabila hata kama kawehuka kiasi gani. Maneno ya vijiweni ni mengi, huwezi kuyaamini kirahisi. Na kama ni kweli imesemwa mitaani kwamba CDM ni chama cha ukabila basi ni aibu ipi CDM imevuna zaidi ya kuendelea kuungwa mkono kila kukicha na sote ni shahidi? Basi tuseme wana CDM wote Tanzania wajiandaa kubadili makabila yeo ili wote wageuke Wanyamwezi gurudumu lisonge.

Ujumbe, sms, wa pili ni mawazo finyu ambayo mwanafunzi wa kidato cha kwanza hawezi kuandika. Bendera ya Taifa kuvaliwa na Mwigulu kwangu sioni tatizo ikiwa humohumo bungeni inakanyagwa hovyo na viatu vichafu kila siku. Ni bendera hii hii ambayo inapepea kwenye mahoteli yaliyo na makasino, na ni bendera hii hii ambayo siku hizi hata ikifika saa 12 jioni wakati ishukapo watu hawana habari, wanatembea tu. Tundu Lissu (Mh Mb) aliwahi kuguswa na uvaaji wa skafu wa Mwigulu lakini sote tunajua Mh Simbachawene alivyotoa muongozo. Kama mwandishi ni mbumbumbu wa haya nashindwa kuamini kwamba Mh Mwingulu alishindwa vipi kumfafanulia. Labda niseme tu kwamba mwandishi hana busara na ni mchochezi. Suala la sanda sijui hata linahusiana vipi na kitambaa ambacho ukubwa wake hauzidi 1x1'.

SMS ya mwisho iko too general kwamba 'itageuka kilio kwako' pengine alikusudia kusema 'itageuka msiba kwako' maana ifike wakati tuyasome mawazo ya mwandishi. Mwigulu sidhani kama anafurahia akitafsiriwa kwamba ni 'fahari' katika medani za siasa ama jamii. Sidhani kama kuna politician yeyote anayependa kuwa fahari wakati nchi yake inamegwa bila huruma, na wakati wapiga kura wake kutwa kucha wanaomba hisani kwake. Siamini hilo. Pengine angesema 'kujulikana kwako' hapo angeeleweka. Mimi binafsi nimeshindwa kuamini kwamba mwandishi alikusudia nini kwa msg hii.

Mwisho niseme wazi kwa wazoefu wa kusoma hapa na pale, unaweza tu kugundua kwamba kwanza sms hizi zimeandikwa na mtu mmoja, zimeandikwa katika hali ya hasira na husuda, hazina ujumbe ulio wazi (zinaacha maswali mengi) na haziendani na hali halisi ya wimbi la upinzani nchini. Zimekosa uzito.

Lakini na tuwaachie maafande wetu wachunguze hili ili kubaini chanzo na makusudi hasa ya sms hizi tata.

Nawasilisha,

G Kassanga
Tabora.
 
Sioni ubaya wa hio memo ila kama kweli ni ya Mbowe basi wewe Mama Porojo ni Nchemba au mmoja wa Mistress wake maana iliandikwa kwa Nchemba na umeipataje??
 
Jamani msishangae kutukanwa,kukejeliwa na kushambuliwa pale utakaposema ukweli kuhusu chadema na viongozi wake, wanaofanya kazi hiyo ni vijana wa chadema wasiojitambua wako pale makao makuu ni kikosi kazi kinaongozwa na Mnyika hawa vijana wanapewa Posho kwa kazi ya kuitetea chadema na kuisemea mazuri mitandaoni wakati huo huo wanaishambulia CCM na serikali yale lendo kuui kuidhoofisha kwa wananchi ili waichukie na kuja kuipa madaraka ya utawla chadema yani wanapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya CCM na serikali yake usifikiri wako vijana wengi hapana ni vijana wachache wanejisajili kwa IDs tofauti tofauti hiyo ndiyo chadema yenye mikakati michafu ya kushika dola ukionganisha na ule mkakati wa kushawishi,kudhamini na kuchochea migomo na fujo zote hapa nchini kwa Madaktari,Wanafunzi vyuoni na walimu! SHAME ON U CHADEMA Kwa mbinu chafu zinazoumiza watanzania!
Are you sure with what you have just posted buddy?
Inshu siyo kuchochea migomo, unajua kabisa hali ilivyo. Ila kwa sababu unaweza kupata mkate wako wa kila siku bila kutoka jasho, bila kufuata haki, bila kulipa kodi isivyo halali kutokana na mitandao ulivyo nayo umeamua kukomaa.

Sawa, ila ukweli unaujua na ipo siku utaukubali kwa maneno yako!

Kama CCM/serikali mtaweza kutujengea mashule yenye maabara na walimu huku kukiwa hakuna ubadhirifu kwenye halmashauri zetu, hospitali zetu angalau vifaa vinavyoweza kutengenezwa kwa zao la pamba ziwepo ili kuokoa maisha ya watanzania wenzako wasioweza kwenda india, vyuo vikuu kuwepo na vifaa vya kutosha pamoja na walimu ili mtoto wako na wangu wasome katika hali isiyo ya kulala watu wawili kitanda kimoja,

Mtatue magumashi yote ya uonevu wa viwanja vya wazi kwa ajili ya michezo kwa watoto wetu achilia mbali mfumo mbovu wa aliyenacho ndiyo anafaa kuwa kiongozi ndani ya CCM/serikali hata kama ni mtupu kichwani. Pamoja na hayo mfumo mzuri wa angalau kila mmoja aweze kupata milo mitatu kwa siku bila shida kama atafanya kazi kama ilivyo kwenye nchi nyingi za asia, miundo mbinu kama reli iwepo na kila mmoja apate kile anachostahili, police wetu wafanye kazi na kuheshimu mipaka ya kazi zao!!

Why not you guys keep ruling our country? We gonna keep challenging you and if you don't wanna change, we will fight for our survive!!
Sikiliza hii hapa BEST SPEECH EVER.
 
Du MAMA POROJO kwanza pole na safari za toka Majuzi, Singida - Kigamboni na kurudi tena kwenye Mazishi ya kada wa Chama huko Singida jana.

Kweli wewe kiboko umewezaje kufukunyua kwenye mifuko ya Nchemba mpaka ukakikuta hicho ki-Memo au ni Dry Cleaner wake? Aaa ni nyumba nd mmmm haiwezekani sasa tuwekee na zile sms alizotishiwa kifo Mwigulu na nakala anazo Spika.


Halafu mwambie Mwigulu sasa kakua kwa nini analeta vurugu asizoziweza maana ana ugomvi usio na mwanzo, Siasa za majimoto zina mwisho, na baadae Historia itamhukumu
 
- Naona mkakati wako kisiasa ndani na nje ya bunge umekuwa ‘ more and more attack onmyself ( personal) and my family’!

-
‘ mindyou i don’t mind being criticised, but not on ficticious accusations withmalice intentions targetting, my personal life and my family!



My take: vita ya maneno makali ndani yabunge yanatupeleka wapi kisiasa?

1. Je kuandikiana vi-memo na kutupiana
manenomakali mbungeni kuna athari za moja kwa moja na kutupiana maneno makali kwenye majukwaa ya kisiasa nje ya mbunge?

2. Je hakuna athari za
mauaji ya kisiasa yanayotokea katika uwanja wa siasa nchini?

3. Nini kifanyike kuondoa hali hii????????
@MAMA POROJO, Ikiwa ulikusudia kupiga porojo ninakusamehe bure, vye3nginevyo naomba ujibu 1 na 2:


1. Kuna maneno makali gani kwenye hiyo memo?

2. Je, hayo mauaji ya kisiasa yanayoendeleayanatokana na hizo 1.memo, 2.mashambulizi kwa masuala ya kifamilia, au nini kwa mtizamo wako?

3. Nini kifanyike kuondoa hali hii? Kama mauaji yanatokana na 1 na/au 2, cha kufanya ni kuacha kuandikiana vimemo na kuacha kushambuliana kwa mambo binafsi.
 
Jamani msishangae kutukanwa,kukejeliwa na kushambuliwa pale utakaposema ukweli kuhusu chadema na viongozi wake, wanaofanya kazi hiyo ni vijana wa chadema wasiojitambua wako pale makao makuu ni kikosi kazi kinaongozwa na Mnyika hawa vijana wanapewa Posho kwa kazi ya kuitetea chadema na kuisemea mazuri mitandaoni wakati huo huo wanaishambulia CCM na serikali yale lendo kuui kuidhoofisha kwa wananchi ili waichukie na kuja kuipa madaraka ya utawla chadema yani wanapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya CCM na serikali yake usifikiri wako vijana wengi hapana ni vijana wachache wanejisajili kwa IDs tofauti tofauti hiyo ndiyo chadema yenye mikakati michafu ya kushika dola ukionganisha na ule mkakati wa kushawishi,kudhamini na kuchochea migomo na fujo zote hapa nchini kwa Madaktari,Wanafunzi vyuoni na walimu! SHAME ON U CHADEMA Kwa mbinu chafu zinazoumiza watanzania!
nimeamua kuandika kwa kusoma uongo na umbea wako eti wapo vijana wachache wewe sijui unaishi nchi gani wewe eti id tofauti ivi una akili kweli kaka kuwa makini watanzania si wa kudanganywa
 
CDM mmejiumbua wenyewe kwa hizi sms, na huo utetezi wako hata mtoto wa chekechea huwezi kumzuga, anzisha jukwaa lako uweke propaganda zako, JF ni jukwaa huru na kile ukiletacho huchambuliwa kwa kina.

 
Back
Top Bottom